Ada Ya mitihani kufutwa Je ni Sahihi?

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
806
426
Wakuu kama mnavyokumbuka serikali imefuta ada za mitihani kwa shule za serikali tu. Je hii ina maana kua anayesoma private schools ni lazima awe na uwezo? Sii kwamba amekosa nafasi ya kujiunga ba shule ya serikali? Sii kwamba shule za serikali huduma hafifu? Je kwa nini kuwe na ubaguzi?
Habari za Kitaifa

Waraka kurudisha ada za mitihani watoka
Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 26th February 2010 @ 23:59 Imesomwa na watu: 468; Jumla ya maoni: 7





SERIKALI imeagiza wanafunzi waliolipia ada za mitihani itakayofanyika baada ya Julai mosi mwaka huu warejeshewe fedha zao.

Uamuzi huo umo katika Waraka Namba Moja wa Elimu wa mwaka 2010 ambao unasisitiza tamko la Serikali la kufuta ada za mitihani kwa wanafunzi wa kidato cha pili, nne na sita wa shule za sekondari za Serikali.

Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Kamishna wa Elimu, Aminieli Mrutu, ilieleza kuwa Serikali imeamua kutowatoza wanafunzi watakaofanya mitihani hiyo Septemba mosi mwaka huu.

“Kuanzia mwaka wa fedha 2010/11 Serikali itatenga fedha katika bajeti yake ya elimu kwa ajili ya uendeshaji wa mitihani. Wakuu wote wa shule za sekondari za Serikali wanaagizwa kutotoza ada za mitihani,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, utaratibu huo hautawahusu wanafunzi wa shule zisizo za Serikali na watachangia kwa kiwango kitakachowekwa na Baraza la Mitihani la Taifa na Idara ya Ukaguzi wa Shule.

Waraka huo unarekebisha Waraka namba 5 wa mwaka 1999 sehemu zinazohusu ada za mtihani wa kidato cha pili. “Kwa waraka huu, Baraza la Mitihani Tanzania linaagizwa kurekebisha kanuni zake zinazohusu malipo ya ada ya mitihani iliyotajwa,” ilisema taarifa.

Mwaka 1999 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ilitoa waraka namba 5 ulioelekeza kuwa sehemu ya gharama za uendeshaji wa mtihani wa kidato cha pili zitatokana na michango ya wanafunzi wanaofanya mtihani huo pamoja na shule.

Wanafunzi wa vidato vya nne na sita hutozwa ada ya mitihani kulingana na kanuni za Baraza la Mitihani za mwaka 2006 kama ilivyochapwa kwenye Gazeti la Serikali namba 16 la Februari 2006.

Kaimu Kamishna wa Elimu kupitia waraka huo, alisema Serikali itatenga fedha katika bajeti yake ya elimu ya mwaka ujao kwa ajili ya uendeshaji wa mitihani. Kwa mujibu wa taarifa iliyowahi kutolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, Serikali italazimika kutumia takribani Sh bilioni 20 katika mwaka ujao wa fedha, kwa ajili ya kuendesha shughuli za mitihani baada ya kutangaza uamuzi wa kufuta ada ya mitihani ambayo ilikuwa ikigharimia shughuli hizo.

Uamuzi wa Serikali wa kubeba mzigo huo wa gharama, umetokana na kile kilichoelezwa na Mahiza, kuwa ni kutokana na kubaini kwamba maelfu ya wanafunzi walikuwa wakishindwa kufanya mitihani kutokana na kukosa ada au fedha zao kutowasilishwa na wakuu wa shule.

Mahiza alisema kulingana na takwimu zilizopo za wanafunzi walioshindwa kufanya mitihani katika miaka ya nyuma, endapo uamuzi huo wa kufuta ada usingechukuliwa, zaidi ya wanafunzi 50,000 wa shule za serikali wasingefanya mitihani.

“Miaka ya nyuma tumepoteza maelfu ya wanafunzi. Tusipofanya hivi zaidi ya wanafunzi 50,000 watapotea,” alisema. Katika hatua nyingine, Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi imetoa vitabu viwili teule vya kiada kwa shule za elimu ya awali na msingi kwa darasa la kwanza hadi la tano na kufuta utaratibu wa sasa wa kutumia kitabu zaidi ya kimoja cha kiada.

Kwa upande wa vitabu vya darasa la sita na saba havitahusika kwa sasa na utaratibu uliokuwapo utaendelea kutumika ambapo Mrutu alisisitiza, “vitabu vyote vyenye ithibati ambavyo havikuchaguliwa kutumika kama vya kiada, vitatumika kama vitabu vya rejea na ziada katika kujifunza na kufundishia”.

Mrutu alisema mbali na kutoa vitabu hivyo, wizara inaendelea kupitia upya utaratibu wa matumizi ya kitabu zaidi ya kimoja cha kiada, ili kuhakikisha mabadiliko hayaleti athari katika utoaji elimu nchini.

Alisema utaratibu wa kuteua vitabu vya kiada kwa darasa la sita na la saba na kwa ngazi ya sekondari na vyuo vya ualimu, unaandaliwa.

Uamuzi huo upo katika waraka namba mbili wa mwaka 2010 unaofuta uamuzi wa mwaka 1991 kupitia sera ya upatikanaji na usambazaji wa vitabu shuleni na vyuoni, uliokuwa ukiruhusu matumizi ya zaidi ya kitabu kimoja
 
Serikali ni serikali, na Private nayo kadhalika ni ya binafsi!. Kufuta ada kwa shule za serikali kunamaanisha kwamba serikali ita'subsdise difference, sasa je huko private nani atafanya hivyo?
Tukubaliane na ukweli tu, mpaka itakapoamuliwa tofauti!
 
Back
Top Bottom