kulyunga
JF-Expert Member
- Oct 19, 2011
- 230
- 423
Salaam na fanaka za msimu huu wa sikukuu ziwe pamoja nanyi nyoote..
straight kwenye mada, nikiwa kama mtanzania wa kawaida, mzazi na mdau wa elimu nadhani tamko la kusitishwa ada na michango yote katika kile kilichopachikwa jina la "elimu msingi" pamoja na kuonekana kina faida lukuki usoni lakini naamini kabisa kilifanyika bila utafiti wa madhara yake hususani katika shule maarufu za KATA ambazo ndizo zinazotengeneza sehemu kubwa ya shule za umma au za kina "sie" tunaofurahishwa na tamko hili la Mzee wa "hapa kazi tu"
kuondolewa kwa michango hii no dhahiri kutapunguza mzigo kwa wazazi na walezi na hivyo kufanya idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika sekondari kuwa kubwa.
lakini kwa upande mwingine madhara ystakayotokana na agizo hili ni mengi sana has a kwa mazingira halisi ya nyingi ya shule hizi kimazingira.
kwa mfano shule nyingi za KATA zilijengwa ili kuhudumia KATA nzima na KATA nyingi zina vijiji zaidi ya vinne na hivyo ujengwaji wa nyingi kati ya shule hizi ulifanyika katikati ya KATA hizo na kufanya umbali kwenda na kurudi shule kuwa mkubwa kiasi ambacho kinaweza kumuathiri mwanafunzi kama atalazimika kwenda shule ba kurudi nyumbani kila Siku.
kwa mantiki hiyo wazazi wengi waliridhia na kukubaliana wanafunzi wawe wanakaa shuleni katika hosteli "bubu" ambazo madarasa yalitumika kama mabweni na wazazi walitoa michango ya mahitaji muhimu ikiwemo chakula na vifaa vya nalazi kwa mujibu wa makubaliano yao. hii ilisaidia kupunguza idadi ya watoto hasa wa kike wanaoacha shule kutokana na ujauzito na mazingira yasiyo rafiki hasa umbali wa nyumbani na shuleni.
sasa rasmi serikali imekataza michango yote ya namna hii na tayari wakuu wa shule waliokuwa na hosteli bubu za aina hii wameamriwa kutoziendesha tena.
naona tunarudi kule kule kwa kupoteza watoto wa kike kutokana na mimba, utoro utarudi kule kule kutokana na umbali na hatari ya watoto kufanyiwa ukatili njiani itakuwa ni kubwa zaidi.
kama kweli serikali imedhamiria hili basi hatukuwa tayari tulihitaji utafiti wa kina ambao ungeenda sambamba na ujenzi wa mabweni ili kuepuka kutengeneza matatizo mengine ambayo yataturudisha nyuma hatua nyingi zaidi na kufanya elimu yetu izidi kudorora badala ya kwenda mbele kama tunavyotarajia..