nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
Chama Gani Duniani kinafanya hivyo? Huu hautakuwa Wizi?
Tuesday, 26 April 2011 12:35 newsroom
NA KHADIJA MUSSA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeazimia kujiimarisha kiuchumi, ambapo sasa wanachama watalipa ada zao kulingana na vipato vyao. Sambamba na hilo kitafanya mapitio ya vitega uchumi vyake na miradi mbali mbali kwa kuangalia umiliki wake na mikataba ya upangishwaji kama ina tija kwa Chama. Hayo yalisemwa jana na Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba, alipokuwa akielezea mipango iliyowekwa na Chama ya kuboresha na kuimarisha vitega uchumi vyake. "Moja ya ajenda kubwa ni kuhakikisha naboresha vitega uchumi vyote vya Chama ili kuwa na mapato ya uhakika, hivyo nitakipatia Chama nyavu na si samaki," alisisitiza.
Nchemba ambaye pia ni mbunge wa Iramba Magharibi mkoani Singida alisema katika kufanikisha suala hilo wataangalia uwezekano wa kutenganisha ada kulingana na kipato cha mwanachama mmoja mmoja, ambapo suala la hilo linaweza kurudishwa kwa mabalozi. Hata hivyo, alisema kuwa wana mpango wa kutathmini vitega uchumi vyote vya Chama, ambapo vitakavyoonekana kukosa tija vitauzwa na vinavyofaa vitaboreshwa. Aidha, alisema kuwa mikataba mbalimbali ya upangishaji katika vitega uchumi vya Chama nayo itaangaliwa umiliki wake na kama kutakuwa na dosari zozote watapata ushauri kutoka kwa mwanasheria wa Chama. Kwa mujibu wa Nchemba, watashirikiana na mwanasheria wa Chama kuangalia mtu alivyoingia mkataba kwenye vitega uchumi hivyo na kama hailipi mwanasheria atashauri juu ya hatua za kuchukuliwa ili kuiboresha. Katika mapitio hayo, Chama kinatarajia kupanua wigo wa maeneo ya uwekezaji, hususan kwa kutumia viwanja mbalimbali vinavyomilikiwa na Chama kwa kujenga majengo yatakayokiongezea mapato ya uhakika. Nchemba alitolea mfano viwanja vya mpira wa miguu ambavyo vingi vinamilikiwa na Chama, lengo likiwa ni kutaka kufahamu vinachangia kwa kiasi gani katika kukuza uchumi ili kuangalia kama vinahitaji kufanyiwa marekebisho.