ACT–Wazalendo Yauvalia Njuga Mgogoro wa Ardhi Chasimba Bunju.

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
ACT–Wazalendo Yauvalia Njuga Mgogoro wa Ardhi Chasimba Bunju.

ACT Wazalendo kupitia Msemaji wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Ndg. Bonifasia Mapunda, kimetoa msimamo wa kuunga mkono mapambano ya wananchi ili kukabiliana na wimbi kubwa la migogoro ya ardhi nchi.

Akielezea msimamo huo jana tarehe 28 Septemba 2022 baada ya kukutana na baadhi ya wakazi wa kata ya Bunju iliyopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam ambao wapo kwenye hofu, wasiwasi na kupoteza matumaini kufuatia mgogoro wa ardhi dhidi Kampuni ya Wazo. Baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi alisema kuwa;

“Changamoto ya migogoro ya ardhi nchini kwetu inazidi kuwa kubwa, ipo migogoro katika wafugaji na wakulima, wananchi dhidi ya Serikali, wananchi dhidi ya wawekezaji kwa nyakati zote waathirika ni wananchi, wao ndio wanapoteza haki zao za kutumia ardhi, Sisi ACT Wazalendo tunasema popote penye mgogoro tutasimama na wananchi.”

Aliendelea kusisitiza kwa kuwaeleza wakazi hao kuwa “Kwa hiyo hili jambo lenu wakazi wa Basihaya, Chasimba, Chatembo na Chachui sisi kama chama tunalichukua kwa uzito mkubwa na tutachukua hatua zote hadi haki yenu ipatikane.”

Mgorogoro huo umekuwa ukichukua sura tofauti tofauti kila mara kufuatiwa na mabadiliko ya uongozi wa kinchi hususani mabadiliko ya mawaziri, makubaliano yatakayofikiwa na Waziri wa kipindi fulani yanaweza kubadilishwa anapoingia Waziri mwingine. Kutokana na maoni na taarifa hiyo Ndg. Bonifasia Mapunda alieza hatua zitazochukuliwa katika kuongeza jitahada za wananchi kupata haki zao.

Moja, ACT Wazalendo itaenda kukutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kupaza sauti zao na kuona hatua ambazo Serikali imezichukuwa. Pili, kukutana na wadau wengine wanahusika na suala hilo moja kwa moja. Tatu, kuendelea kushirikiana nao kwenye hatua zingine za kisheria ili kupinga dalili za kudhulumiwa.

Mwisho, Msemaji aliwaeleza kuwa changamoto kubwa inayoikumba sekta ya ardhi na maendeleo ya makazi ni kasi ndogo ya utatuzi wa migogoro. Hivyo, tutalifuatilia suala hili hadi liishe kwa kuwapatia haki zenu.


Imetolewa na;
Ofisi ya utafiti ya baraza la mawaziri kivuli (SCaRo)
ACT Wazalendo
Twitter: @ACTBarazaKivuli
29 Septemba, 2022.
IMG_20220928_141431_040.jpg
 
Back
Top Bottom