ACT-Wazalendo yafafanua kuhusu uteuzi wa RC Kilimanjaro, Bi. Anna Mghwira

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,257
2,000
*MASWALI TATA YANAYO ULIZWA JUU YA UTEUZI WA ANNA MGHWIRA NAFASI YA RC NA MAJIBU YAKE*

Lazima Awe Mjumbe Wa Chama Tawala Yaani CCM Ngazi Ya Mkoa Je? Atabaki ACT Au Itakuwaje?

Jibu
Hapana katiba ya CCM imeweka wazi kuwa atakuwa mjumbe kama ni mwanachama wa Ccm, pia hata spika atakuwa mjumbe kama ni mwanachama wa ccm, hivyo hata kuwa mjumbe wa kamati kuu sababu sio mwanachama wa Ccm lkn ataendelea nafasi yake ya ukuu wa mkoa.

Lazima Asimamie Ilani Ya Chama Tawala CCM Ngazi Ya Mkoa, Je? Atasimamia Ilani Yake (ACT) Au Ya CCM?

Jibu.
Ilani ya vyama vyote huwa Ni kwa maslahi ya wananchi, ilani ya vyama vyote ukisoma zimeelekeza nguvu kuletea wananchi maendeleo, hivyo sio kosa kutekeleza yale ambayo yanalenga kuleta maendeleo kwa wananchi.hata kama akifanya kwa kufuata ilani ya CCM .pia hata shikishwa bendera ya Ccm wala ilani ya chama cha mapinduzi.

Je? Bado Atasimama Kidete Kumkosoa Bosi Wake (JPM)?

Jibu
Dah bahati mbaya hata pata nafasi kumkosoa waziwazi sababu atakuwa na nafasi ya kumwambia moja kwa moja sabababu wakuu wa mikoa wana nafasi kubwa ya kuwasiliana na Mh. Raisi.

Je? Atajiuzulu Uenyekiti Wa ACT Taifa?

Jibu.
Hapana hata jiuzulu sababu nafasi aliyopata ni yakisiasa, inamruhusu awe mwenyekiti wa chama bado, ila kuna nafasi ambazo angetakiwa ajiuzulu kama ukatibu sio nafasi ya kisiasa, ila professionalism.

Baada Ya Kitila Mkumbo (GS), Anna (RC) Nani Atafuata Kupewa Ulaji Na JPM Kutoka ACT?

Jibu.
Hakuna ajuaye sababu maamuzi ni ya Mh Raisi.

Ni Kweli Zitto Zuberi Kabwe Ni Pandikizi La CCM Na Ndiye Mrithi Wa Profesa Muhongo Nishati Na Madini?
[HASHTAG]#Mwenye[/HASHTAG] Jibu.

Zitto sio pandikizi, zitto ni kiongozi wa ACT WAZALENDO. ukiwa pandikizi maana yake Ni puppet (kibaraka)sifa kuu ya kibaraka Ni kutii yote unayoambiwa na aliyekupandikiza, lakini Zitto amekuwa akiikosoa na kuishauri serekali kwa maslahi ya watanzania amekuwa "active opposition leader zaidi hata ya wapinzani wengine, ukitaja wapinzani imara Tundu Lisu, msigwa, mnyika,, mbowe huwezi acha mtaja Zitto.

Zitto ndiye aliyepinga kwa nguvu mswada wa habari, na alifukuzwa bungeni na hakushiri vikao vya bajeti alitaka kuichambua akiwa nje, alitaka kamatwa, Zitto ndiye aliyepinga kukamatwa kwa Lisu bila kufuata sheria, zitto ndiye aliyepinga mbowe kutaja kushiriki madawa ya kulevya, Zitto ndiye alisemea watanzania kuhusu njaa bila uwogo, bila kupepesa macho hakuna kibaraka Au pandikizi la Ccm wa namna hii.

Kuhusu Zitto kushika nafasi ya mhongo, Waziri WA nishati na madini, hakuna ukweli, sababu hayo Ni maamuzi ya Raisi.

Jambo linalotuumiza watanzania ni political culture yetu na wala sio katiba yetu ya nchi , kuwa mtu akiteuliwa ukuu wa mkoa, katibu mkuu, basi ni Ccm hapana, mfano Raila odinga kiongozi mpinzani chama cha ODM leo kenya aliwahi teuliwa kuwa Waziri wakati akiwa mpinzani, lakini hadi leo Ni mpinzani mkubwa, na anagombea uraisi kwa ushawishi mkubwa.

ACT WAZALENDO, ni chama pinzani imara ingawa ndio Chama kinapitia mitihani ya kutazamwa kwa mtazamo tofauti sababu ya uteuzi, uteuzi sio dhambi na utakuwa Ni unafiki siku zote unapiga kelele siku unapewa nafasi ukafanye alafu ukatae ili ubaki kupiga kelele, hawa hawa wanaokukosoa, watakukosoa utakapoendelea piga kelele kuwa kwanini hukwenda kufanya ulipo teuliwa,

Hivyo jambo la msingi, na la maana Ni kwenda kuwatumikia watanzania, kuliko kukataa.

Mfano. Leo msigwa anateuliwa kuwa Waziri wa mambo ya nje atakataa ?, kwanini akatae wakati anaenda fanya yale ambayo anayapigia kelele, hivyo akatae ili aendelee kuwa mkosoaji na sio mtekelezaji na mfanyaji ??

Chama cha ACT WAZALENDO, kipo imara kwa maslahi ya wananchi wote.

Imetolewa na

Abdul Omary Nondo
 
mshumbue-soi

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
1,846
2,000
Rais alisema hatachagua wapinzani na mpaka sasa ktk Tanzania ya viwanda sijaona akichagua mpinzani siku akichagua tutasema au amechagua??
Nani mpinzania amemchagua sijaona wala kusikia wizarani wala mkoani naona wote ni walewale chama Tawala
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
23,673

Chama gani upuuzi, chama kinapata kura 98,763= 0.65% ya kura zote za urais! Unakaa unasema nina chama! Sema Zito amepata pa kujishikza kwenye siasa za Tanzania, lazima watu wake wakipata kuteuliwa waitikie! Ajaribu kwa Lisu!
 
Word

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
1,355
2,000
Njaa mbaya sana..nmeamin njaa haina mtoto wa mkubwa....anna nlikuwa nakuona kama mama yangu ambaye hawezi niacha mwanae nikafa na njaa jangwani lakin kwasasa umeonyesha wazi wew ni mchawi wa maendeleo yangu.
Yani umeongea mashudu matupu hata ukiyachanganya na pumba pumba zitajitenga kivyake. Aibu.. et mchawi we maendeleo yako kaaah
 
MASEETO

JF-Expert Member
Dec 7, 2013
261
225
Hapo jibu lipo wazi, kama Rais alisema hatateua waoinzani katika seeikali yake, nidhahili kuwa walioteuliwa wote ni wanachama wa ccm regardlesa wamesajiliwa chama cha upinzani. kinachoangaliwa hapo ni dhamira. ila kwa upande mwengine watanzania tuache uongo na unafiki, Rais anateua watu anaoona wanafaa kwa maslahi ya taifa siyo ya chama kwa hiyo mm sioni tatizo kama mtu kateuliwa kutoka chama cha upinzani na siyo mtu anayepinga sera za maendeleo
 
Ngosha255

JF-Expert Member
Mar 29, 2013
364
500
Kuna Jamaa humu JF alisema SIASA NI KAMA MPIRA TU ukifikia dau unamsajili yeyote unaemtaka

Ile ni ajira Mtu anapotumia Mali zake hadi na kukopa kwa ajili ya Kampeni anawekeza

Hebu wasilipwe kwenye hvyo vyama kama wataendelea kuvipigania
 
ancillary

JF-Expert Member
May 30, 2017
564
1,000
Njaa mbaya sana..nmeamin njaa haina mtoto wa mkubwa....anna nlikuwa nakuona kama mama yangu ambaye hawezi niacha mwanae nikafa na njaa jangwani lakin kwasasa umeonyesha wazi wew ni mchawi wa maendeleo yangu.
ulitaka afanyeje mkuu,hapo ndiyo pakuonesha uwezo wake
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,590
2,000
Kuna Jamaa humu JF alisema SIASA NI KAMA MPIRA TU ukifikia dau unamsajili yeyote unaemtaka

Ile ni ajira Mtu anapotumia Mali zake hadi na kukopa kwa ajili ya Kampeni anawekeza

Hebu wasilipwe kwenye hvyo vyama kama wataendelea kuvipigania
ACT hawalipwi mkuu, wanafanya kazi kwa kujitolea
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
8,427
2,000
Njaa mbaya sana..nmeamin njaa haina mtoto wa mkubwa....anna nlikuwa nakuona kama mama yangu ambaye hawezi niacha mwanae nikafa na njaa jangwani lakin kwasasa umeonyesha wazi wew ni mchawi wa maendeleo yangu.
Kumbe njaa ndo tatizo??? Mfate huko KLM usife njaa jangwani. Kumbe ACT ni jangwani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom