ACT-Wazalendo yafafanua kuhusu uteuzi wa RC Kilimanjaro, Bi. Anna Mghwira

Swali langu ni moja tu; ACT Wazalendo wana msimamo gani kuhusu vyeo vya wakuu wa wilaya na mikoa?
 
Hapo jibu lipo wazi, kama Rais alisema hatateua waoinzani katika seeikali yake, nidhahili kuwa walioteuliwa wote ni wanachama wa ccm regardlesa wamesajiliwa chama cha upinzani. kinachoangaliwa hapo ni dhamira. ila kwa upande mwengine watanzania tuache uongo na unafiki, Rais anateua watu anaoona wanafaa kwa maslahi ya taifa siyo ya chama kwa hiyo mm sioni tatizo kama mtu kateuliwa kutoka chama cha upinzani na siyo mtu anayepinga sera za maendeleo

Mna akili ndogo sana.

Haalafu roho zinawauma sana ndugu zetu.

Maendeleo hayana chama acha mama akawapiganie wana Kilimanjaro.
 
Umefanya vizuri kuwajibu lakini nilikuwa sioni umuhimu wowote wa kuwajibu.
ACT ni chama makini na kitaendelea kuwa makini. Wacha wapige kelele ambazo kimsingi hazina tija kwa chama.
*MASWALI TATA YANAYO ULIZWA JUU YA UTEUZI WA ANNA MGHWIRA NAFASI YA RC NA MAJIBU YAKE*

Lazima Awe Mjumbe Wa Chama Tawala Yaani CCM Ngazi Ya Mkoa Je? Atabaki ACT Au Itakuwaje?

Jibu
Hapana katiba ya CCM imeweka wazi kuwa atakuwa mjumbe kama ni mwanachama wa Ccm, pia hata spika atakuwa mjumbe kama ni mwanachama wa ccm, hivyo hata kuwa mjumbe wa kamati kuu sababu sio mwanachama wa Ccm lkn ataendelea nafasi yake ya ukuu wa mkoa.

Lazima Asimamie Ilani Ya Chama Tawala CCM Ngazi Ya Mkoa, Je? Atasimamia Ilani Yake (ACT) Au Ya CCM?

Jibu.
Ilani ya vyama vyote huwa Ni kwa maslahi ya wananchi, ilani ya vyama vyote ukisoma zimeelekeza nguvu kuletea wananchi maendeleo, hivyo sio kosa kutekeleza yale ambayo yanalenga kuleta maendeleo kwa wananchi.hata kama akifanya kwa kufuata ilani ya CCM .pia hata shikishwa bendera ya Ccm wala ilani ya chama cha mapinduzi.

Je? Bado Atasimama Kidete Kumkosoa Bosi Wake (JPM)?

Jibu
Dah bahati mbaya hata pata nafasi kumkosoa waziwazi sababu atakuwa na nafasi ya kumwambia moja kwa moja sabababu wakuu wa mikoa wana nafasi kubwa ya kuwasiliana na Mh. Raisi.

Je? Atajiuzulu Uenyekiti Wa ACT Taifa?

Jibu.
Hapana hata jiuzulu sababu nafasi aliyopata ni yakisiasa, inamruhusu awe mwenyekiti wa chama bado, ila kuna nafasi ambazo angetakiwa ajiuzulu kama ukatibu sio nafasi ya kisiasa, ila professionalism.

Baada Ya Kitila Mkumbo (GS), Anna (RC) Nani Atafuata Kupewa Ulaji Na JPM Kutoka ACT?

Jibu.
Hakuna ajuaye sababu maamuzi ni ya Mh Raisi.

Ni Kweli Zitto Zuberi Kabwe Ni Pandikizi La CCM Na Ndiye Mrithi Wa Profesa Muhongo Nishati Na Madini?
[HASHTAG]#Mwenye[/HASHTAG] Jibu.

Zitto sio pandikizi, zitto ni kiongozi wa ACT WAZALENDO. ukiwa pandikizi maana yake Ni puppet (kibaraka)sifa kuu ya kibaraka Ni kutii yote unayoambiwa na aliyekupandikiza, lakini Zitto amekuwa akiikosoa na kuishauri serekali kwa maslahi ya watanzania amekuwa "active opposition leader zaidi hata ya wapinzani wengine, ukitaja wapinzani imara Tundu Lisu, msigwa, mnyika,, mbowe huwezi acha mtaja Zitto.

Zitto ndiye aliyepinga kwa nguvu mswada wa habari, na alifukuzwa bungeni na hakushiri vikao vya bajeti alitaka kuichambua akiwa nje, alitaka kamatwa, Zitto ndiye aliyepinga kukamatwa kwa Lisu bila kufuata sheria, zitto ndiye aliyepinga mbowe kutaja kushiriki madawa ya kulevya, Zitto ndiye alisemea watanzania kuhusu njaa bila uwogo, bila kupepesa macho hakuna kibaraka Au pandikizi la Ccm wa namna hii.

Kuhusu Zitto kushika nafasi ya mhongo, Waziri WA nishati na madini, hakuna ukweli, sababu hayo Ni maamuzi ya Raisi.

Jambo linalotuumiza watanzania ni political culture yetu na wala sio katiba yetu ya nchi , kuwa mtu akiteuliwa ukuu wa mkoa, katibu mkuu, basi ni Ccm hapana, mfano Raila odinga kiongozi mpinzani chama cha ODM leo kenya aliwahi teuliwa kuwa Waziri wakati akiwa mpinzani, lakini hadi leo Ni mpinzani mkubwa, na anagombea uraisi kwa ushawishi mkubwa.

ACT WAZALENDO, ni chama pinzani imara ingawa ndio Chama kinapitia mitihani ya kutazamwa kwa mtazamo tofauti sababu ya uteuzi, uteuzi sio dhambi na utakuwa Ni unafiki siku zote unapiga kelele siku unapewa nafasi ukafanye alafu ukatae ili ubaki kupiga kelele, hawa hawa wanaokukosoa, watakukosoa utakapoendelea piga kelele kuwa kwanini hukwenda kufanya ulipo teuliwa,

Hivyo jambo la msingi, na la maana Ni kwenda kuwatumikia watanzania, kuliko kukataa.

Mfano. Leo msigwa anateuliwa kuwa Waziri wa mambo ya nje atakataa ?, kwanini akatae wakati anaenda fanya yale ambayo anayapigia kelele, hivyo akatae ili aendelee kuwa mkosoaji na sio mtekelezaji na mfanyaji ??

Chama cha ACT WAZALENDO, kipo imara kwa maslahi ya wananchi wote.

Imetolewa na

Abdul Omary Nondo
 
huu utetezi hauna maana yoyote baada ya mama mgwira kujuvua uwanachama wa ACT leo mchana.
 
Hii response ya ACT inapotosha. Huyu mkuu wa mkoa anatakiwa atekeleze ilani ya CCM, sio ya vyama vingine eti kwa sababu ya maslahi ya wananchi. Wananchi waliichagua CCM 'kutokana' na ilani yao, hivyo lazima ilani yao itekelezwe.
 
Kabudi alipiga kelele kuhusu katiba mbovu weee akabwatabwata mpaka akawa bwatax weee sasa Magufuli akampa palepale anapobwatabwata leo ukimuuliza kuhusu hiyo katiba mbovu na ipi ni nzuri uipendekeze anakwambia kuwa Magufuli anapita mulemule kwenye katiba aliyokuwa akiipigania hivyo hakuna haja tena ya kuipigania.

Humphrey Polepole naye akapiga yowe kususu vyeo vya wakuu wa mikoa na wilaya wee akabwatabwata weeeee Magufuli akampa hichohicho cheo cha ukuu wa wilaya na akaufyata kwelikweli! Yan akaukunja mkia ukakunjika haswaaa.

Huyu mama Anna alipiga kelele kuhusu mwenge wa Uhuru weee akasema hauna maana kwa watanzania Mungu siyo Athumani kesho kutwa ataupokea atauheshimu atauimbia "kuwasha mwengeee.... kuwasha mwengeee na kuuweeekaaaa Kilimanjaroooo.... umulikeee hata wanafiki.. uleteee tumainiii.... " kisha atawakabidhi ma-dc wake waukimbize Kilimanjaro nzima na atatoa neno la kuupongeza vilevile.
Hahaha dah njaa mbaya sana kaka.
 
Lazima Asimamie Ilani Ya Chama Tawala CCM Ngazi Ya Mkoa, Je? Atasimamia Ilani Yake (ACT) Au Ya CCM?
Jibu.
Ilani ya vyama vyote huwa Ni kwa maslahi ya wananchi, ilani ya vyama vyote ukisoma zimeelekeza nguvu kuletea wananchi maendeleo, hivyo sio kosa kutekeleza yale ambayo yanalenga kuleta maendeleo kwa wananchi.hata kama akifanya kwa kufuata ilani ya CCM...........

mfano Raila odinga kiongozi mpinzani chama cha ODM leo kenya aliwahi teuliwa kuwa Waziri wakati akiwa mpinzani, lakini hadi leo Ni mpinzani mkubwa
 
JPM AIDUWAZA CCM, ACT UTEUZI WA MGHWIRA

IMGL1110-300x200.jpg

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam,
MTANZANIA

RAIS Dk. John Magufuli jana amemteua Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, mwenyekiti huyo wa chama cha upinzani, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Said Meck Sadiki.

Mbali na Mghwira, Rais Magufuli pia amewateua Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi (DIGP), Abdulrahman Kaniki na Meja Jenerali Issah Nassor kuwa mabalozi.

Kabla ya uteuzi huo, Meja Jenerali Nassor alikuwa Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Katika uteuzi huo wa watu watatu, uliozua mjadala na hata kuleta mshituko mkubwa ndani ya siasa za vyama vya upinzani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni ule wa Mghwira.

Ingawa hii si mara ya kwanza kwa Rais anayetokana na CCM kuwateua wapinzani katika nafasi mbalimbali, kinachozua maswali zaidi katika uteuzi huu wa sasa wa Mghwira, ni kumpeleka katika mkoa ambao ni ngome ya chama cha upinzani cha Chadema.

Itakumbukwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa wakati wa utawala wake aliwahi kumteua kada wa CUF, Hamad Rashid kuwa mbunge, huku Rais mstaafu Jakaya Kikwete akimteua kiongozi wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia katika nafasi hiyo hiyo.

Mghwira ambaye amepewa cheo tofauti na kile cha ubunge, uteuzi wake umewafanya baadhi ya makada wa vyama vya pande zote kuanza kuhoji na hata kufikiri kwamba huenda ama kuna usaliti au ajenda za kiutawala wasizozijua.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya makada wa CCM wamekwenda mbali zaidi na kutafuta katiba ya chama chao na kuangalia kama cheo alichopewa Mghwira hakina madhara katika siasa zao.

Mghwira ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi aligombea urais kupitia ACT- Wazalendo na kushika nafasi ya tatu, akipata kura 98,763 nyuma ya Rais Magufuli aliyepata kura 8,882,935 na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wa Chadema aliyevuna kura 6,072,848, sasa atalazimika kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM.

Si hilo tu, licha ya kuwa ni mwanasiasa wa upinzani, atabeba jukumu la kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Mghwira ndiye aliyekuwa mpinzani wa kwanza kumpongeza Magufuli baada ya kushinda urais, pia miongoni mwa wapinzani wachache waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa cheti cha ushindi wa uchaguzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Uteuzi wake pia umekuja zikiwa zimepita siku kadhaa baada ya Rais Magufuli Aprili 4, mwaka huu kumteua mshauri wa ACT- Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Uteuzi wake unaelezwa na baadhi ya wachambuzi wa siasa za kishindani nchini kama ni mwendelezo wa wimbi la viongozi wa chama hicho ama kuondoka katika majukumu yao ya kichama au kuondoka jumla.

Mbali na Mghwira na Profesa Kitila, wengine walioondoka ndani ya chama hicho ni Katibu Mkuu wake, Samson Mwigamba ambaye aling’atuka Mei, mwaka jana na kusema anakwenda masomoni.

Wengine ni aliyekuwa Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali ambaye amejiunga CCM na aliyekuwa Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa wa sekretarieti wa chama hicho, Habibu Mchange, ambaye aliondoka Desemba 10, mwaka jana.

Miongoni mwa watu wa mwanzo kuondoka ndani ya chama hicho ni aliyekuwa mgombea ubunge wa Morogoro Mjini, Selemani Msindi maarufu Afande Sele.

Afande Sele alitangaza uamuzi huo Desemba 15, mwaka jana baada ya kudai kutoridhishwa na viongozi wa chama hicho, akisema msimamo wao umekuwa haueleweki na anashindwa kujua iwapo msimamo wao ni kuunga mkono upinzani au CCM.

Mwingine aliyetangaza kujiondoa hivi karibuni ni aliyekuwa Mshauri wa chama hicho, Wakili Albert Msando, baada ya video yake akiwa ndani ya gari na msanii wa kupamba video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Gigy Money huku wakitomasana kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumzia uteuzi wa Mghwira, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema hawezi kutoa maoni.

“Siwezi kutoa maoni kwa sasa kwa sababu bado sijawasiliana na mwenyekiti (Mghwira) ambaye kwa sasa yuko Marekani,” alisema Zitto.

Akijibu swali kwa nini anashindwa kutoa maoni kwa sasa tofauti na ilivyokuwa wakati wa uteuzi wa Kitila, alisema: “Tofauti ni kwamba Kitila alikuwa nchini wakati uteuzi unafanyika na tulipata muda mrefu wa kuzungumza na kujadiliana na kukubaalina kabla sijatoa maoni.”

Naye Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu, alisema kuna mambo mawili ya msingi yakijumuisha suala binafsi na la kichama.

“Mtu unapoteuliwa, linateuliwa jina la mtu kwamba Kitila Mkumbo, Anna Mghwira umeteuliwa kwenye nafasi fulani, kwa hiyo wao kwa mtu mmoja mmoja wanayo nafasi ya kufanya uamuzi wanaoona unafaa kwa wao wenyewe,” alisema.

Shaibu alisema pamoja na chama hicho kuwa na wanachama wengi, lakini katika ngazi ya chama uteuzi huo ni changamoto kwa kuwa wanaondoka viongozi wakubwa waliokuwa mihimili.

“Lakini katika ngazi ya chama, sisi ni chama cha siasa cha upinzani na Rais Magufuli aliyefanya teuzi hizi ni Rais wa Jamhuri, lakini pia Mwenyekiti wa CCM, kwa hiyo mbali na wao kuwa na uamuzi wao na kwamba nafasi wanazoteuliwa ni za kwenda kuhudumia wananchi, lakini kwetu ni changamoto kwa maana mnaondokewa na viongozi wakubwa ambao walikuwa mihimili, ukitazama watu wanne, watano waliokuwa mihimili ya ACT, huwezi kuwatoa Mghwira na Kitila,” alisema Shaibu.

Kuhusu uteuzi huo ulivyopokewa, alisema kumekuwa na dhana mbalimbali ambazo si rahisi kuzikwepa.

“Mfano uteuzi wa sasa, imezoeleka, nasema ni mazoea tu kwamba Mkuu wa Mkoa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, lakini pia ndani ya CCM wao wenyewe walishajipangia kwa taratibu zao kuwa mmoja wa wajumbe wa vikao vya mkoa ni pamoja na RC, kwa hiyo wamezoea hivyo kuwa ukiwa mkuu wa mkoa unakuwa sehemu ya CCM. Hilo nasema ni mazoea kwa kuwa katiba na taratibu za CCM hazibani watu wote Tanzania, zinawaongoza wana CCM,” alisema.

Hata hivyo Shaibu alisema jambo hilo linabaki kuwa mtego kwa upande mwingine na kushauri asubiriwe Mghwira mwenyewe azungumzie uteuzi wake.

Gazeti hili lilimtafuta Mghwira kwa simu ya mkononi, lakini hakupatikana kutokana na namba zake kutopatikana na Shaibu alisema kiongozi huyo alikuwa nje ya nchi kuhudhuria kongamano la wanawake.

Shaibu alisema Mghwira angekuwapo tayari viongozi wangekutana na kulijadili na kungekuwa na mwafaka.

Akizungumzia wimbi la wanachama wao kuondoka, alisema suala hilo lilikuwa la lazima kwa sababu lilikiweka chama hicho sehemu nzuri na huo ndiyo uadilifu.
 
Njaa mbaya sana..nmeamin njaa haina mtoto wa mkubwa....anna nlikuwa nakuona kama mama yangu ambaye hawezi niacha mwanae nikafa na njaa jangwani lakin kwasasa umeonyesha wazi wew ni mchawi wa maendeleo yangu.
Pole kama wewe una utumbo wa plastiki nijuavyo hakuna kiumbe hana njaa
 
Njaa mbaya sana..nmeamin njaa haina mtoto wa mkubwa....anna nlikuwa nakuona kama mama yangu ambaye hawezi niacha mwanae nikafa na njaa jangwani lakin kwasasa umeonyesha wazi wew ni mchawi wa maendeleo yangu.

Kweli kuna watu hawafundishiki! Hata baada ya maelezo yoote hapo juu bado hujaelewa maana ya maendeleo na maslahi ya taifa?
 
Lazima Asimamie Ilani Ya Chama Tawala CCM Ngazi Ya Mkoa, Je? Atasimamia Ilani Yake (ACT) Au Ya CCM?
Jibu.
Ilani ya vyama vyote huwa Ni kwa maslahi ya wananchi, ilani ya vyama vyote ukisoma zimeelekeza nguvu kuletea wananchi maendeleo, hivyo sio kosa kutekeleza yale ambayo yanalenga kuleta maendeleo kwa wananchi.hata kama akifanya kwa kufuata ilani ya CCM...........

mfano Raila odinga kiongozi mpinzani chama cha ODM leo kenya aliwahi teuliwa kuwa Waziri wakati akiwa mpinzani, lakini hadi leo Ni mpinzani mkubwa
Ilani ya Uchaguzi inakuzwa kisiasa tu; haina nguvu yoyote kisheria. Ilani ina kazi ya kushawishi kura; chama kinachoshinda kinapata mwongozo wa ilani kutengeneza sera na sheria, au hata kutekeleza ilani kama kuna mwanya huo kupitia sheria iliyopo tayari. Yote haya yanaonyesha kuwa ilani inapata uhai na uhalali pale tu inapopitishwa KISERIKALI kuwa sheria. Jibu la huyu Nondo lilitakiwa kuwa Mghwira atatekeleza sheria, siyo ilani. Pili, Odinga hakuwahi kuwa waziri akiwa mpinzani. Mara ya kwanza kuwa waziri alikuwa Katibu Mkuu wa KANU, na baadaye akiwa chama kimoja na Kibaki, na baadaye tena akiwa katika serikali mseto.
Lazima Asimamie Ilani Ya Chama Tawala CCM Ngazi Ya Mkoa, Je? Atasimamia Ilani Yake (ACT) Au Ya CCM?
Jibu.
Ilani ya vyama vyote huwa Ni kwa maslahi ya wananchi, ilani ya vyama vyote ukisoma zimeelekeza nguvu kuletea wananchi maendeleo, hivyo sio kosa kutekeleza yale ambayo yanalenga kuleta maendeleo kwa wananchi.hata kama akifanya kwa kufuata ilani ya CCM...........

mfano Raila odinga kiongozi mpinzani chama cha ODM leo kenya aliwahi teuliwa kuwa Waziri wakati akiwa mpinzani, lakini hadi leo Ni mpinzani mkubwa
 
Njaa mbaya sana..nmeamin njaa haina mtoto wa mkubwa....anna nlikuwa nakuona kama mama yangu ambaye hawezi niacha mwanae nikafa na njaa jangwani lakin kwasasa umeonyesha wazi wew ni mchawi wa maendeleo yangu.
Mkuu muache mama apige kazi tafadhali
 
Hahahahahahaha ACT bhana...... eti kila Ilani ya chama ipo kuleta maendeleo ya wananchi??? Wakati juzi ti walisema hakuna chama chenye ilani bora kma ACT na wakaenda mbali kusema ilani ya CCM ipo kuwahadaa watu maana vitu vingi hawawezi tekeleza ssa sijui muujiza gani umetokea wanaona leo hii ILANI ya CCM inatekelezeka!!!!!

Upinzani wa TZ nje ya UKAWA dah una safari ndefu sana
 
Mna akili ndogo sana.

Haalafu roho zinawauma sana ndugu zetu.

Maendeleo hayana chama acha mama akawapiganie wana Kilimanjaro.
Sawa mkuu ila ni maajabu kwa Mwenyekiti wa chama cha upinzani na aliyewahi kugombea uraisi uchaguzi uliopita anateuliwa kuwa RC. Ili uwe RC kwa mkoa kama huo lazima uwe kada kwelikweli wa chama tawala, labda wangempeleka mikoa isiyo na upinzani mkubwa.
 
Back
Top Bottom