ACT-Wazalendo wampokea rasmi Moses Machali Julai 21

ACT-Wazalendo wampokea rasmi Moses Machali Julai 21

saidi kindole

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2012
Posts
311
Reaction score
796
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ,kesho julai 21 atampokea Mbunge wa Kasulu, mjini Moses Machali(NCCR-Mageuzi), ambaye atajiunga atatambulishwa rasmi kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo.

Machali ataambatana na Madiwani wawili,Kamishna wa mkoa mmoja na katibu wake pamoja na wenyeviti na makatibu wa kata 12 zilizo katika jimbo la Kasulu mjini

Pia katika mapokezi hayo kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe atawapokea na makatibu uenezi 9 wa jimbo la Kasulu mjini yenye jumla ya kata 15 za uchaguzi

Mbali na viongozi hao wengine watakaoambatana na Machali kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo siku ya jumanne julai 21/2015 ni pamoja na wenyeviti wa matawi 101 na makatibu 98, watakaoambatana na wanachama wa awali 648.wanachama na viongozi wote hao wanatoka katika Chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Kasulu mjini

Baada ya Mapokezi hayo ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo, Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe ataelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuwapokea viongozi na madiwani kutoka vyama mbali mbali zoezi litakalofanyika siku ya Jumamosi julai 25.

Julai 26 Kiongozi wa Chama atakutana na watia azma wa nafasi ya Ubunge katika majimbo ya jiji la Dar esSalaam kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi.

Wakati kiongozi wa Chama akiwa mikoani kwa ajili ya kuwapokea wanachama wapya, jijini Dar esSalaam siku ya jumatano julai 22 viongozi wengine watakuwa na jukumu la kuwapokea wanachama na waliokuwa madiwani katika vyama tofauti.

================================
UPDATES

attachment.php
attachment.php
 
Kwahiyo kule monduli nayo yalikuwa makapi toka ccm? Vipi kwa lembeli

Nilikua napita tu kuwa sabahi mimi huyoooooo.
 
Ni mwaka wa mavuno ukikosa kuvuna kipindi hiki basi tena.
 
ukipokea wapinzani wakati muda wa kurudisha form ccm ukiwa umeisha jua kuwa ni kapi kuu, ukija mapema hapo sawa.
 
ni wakati wa kuwa wazalendo ndio maana ACT wapo hapa kuikomboa Tanzania
 
saidi kindole

Haya kazi hiyo, chama cha upinzani kinabomoa chama kingine cha upinzani badala ya kubomoa chama tawala. Watu wakisema chama hiki kinafanya kazi kwa niaba ya chama tawala watu watakataa.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: 999
saidi kindole

Vipi ahadi aliyotoa zzk kuwa atampokea lowasa bado ipo?
 
Last edited by a moderator:
Huko kasulu sasa mnaelekea kupoteza jimbo kwa ccm. Machali umepotea mkubwa
 
Kiongozi wa Chama cha ACT-WAZALENDO Ndugu Zitto Kabwe leo anatarajiwa kumpokea Mbunge Moses Machali ktk Chama cha ACT-WAZALENDO.

Machali anapokelewa na Wanachama wapya kutoka NCCR-MAGEUZI wanachama 798 na Viongozi wote wa Kata wa Jimbo la Kasulu Mjini.

Machali anapokelewa na Kiongozi wa ACT-WAZALENDO Zitto Kabwe ktk Mkutano wa Hadhara unafanyika Viwanja vya Kiganamo leo.

Tutawaletea kinachojiri ktk Mkutano Huu
 
Back
Top Bottom