SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Chama cha ACT Wazalendo kimefuta ukomo wa uongozi kwenye marekebisho ya katiba yake ya Machi, 2020.
Kwa mujibu wa marekebisho hayo ibara ya 111(4) mwanachama anaweza kuwa kiongozi kwa muda wa miaka mitano (5), na anaweza kuchaguliwa tena kwa muda wowote kama wanachama wanamkubali.
Hivyo kwa mabadiliko haya viongozi waliochaguliwa wanaweza kukaa madarakani milele ili mradi wanachama wanawakubali.
Katiba ya Zamani ya ACT WAZALENDO ya mwaka 2015, iliweka ukomo wa uongozi kwa nafasi moja kwa muda wa vipindi viwili vya miaka mitano-mitano (5) tu, yaani miaka kumi (10).
Kwa msingi huo Kiongozi wa chama hicho Zitto Zuberi KABWE hii ilitakiwa kuwa ndio awamu yake ya pili na ya mwisho kwa nafasi ya kiongozi wa chama, lakini kwa mabadiliko hayo ataendelea kwenye nafasi hiyo milele na milele ili mradi wanachama wamkubali.
Ni nchini kwetu Tanzania ndo utakutana na utitiri wa viongozi wa vyama vya upinzani wa kudumu lakini waigizaji wakubwa kuwa ni watetezi wa Demokrasia..
Kila siku huwa nasema , vyama vya upinzani nchini kwetu Tanzania ni mifumo ya utafutaji fursa za maisha tu na wala si vinginevyo.
Eti wanapigania demokrasia, katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Zitto aliyemshambulia Freeman Mbowe kwa kuondoa ukomo wa uongozi kwenye katiba ya CHADEMA yeye leo kaiga!
#WaigizajiWaDemokrasia #corona #covid19
Sent using Jamii Forums mobile app