Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,502
- 51,098
Tumebakisha miezi mitano ya uchaguzi. Muda haupo upande wenu, wananchi tunangoja kwa hamu kuona mnatuletea mgombea bora, makini, mzalendo, mweledi na anayeweza kurekebisha makosa makubwa mno yaliyofanywa na serikali ya awamu hii ili. kuirudisha nchi katika msitari sawasawa kstika nyanja za kiuchumi na kisiasa. Katika muktadha huu mnapaswa kufanya maamuzi magumu, bila kuchelewa, Muda wa kusimama na kufanya maamuzi ni sasa, kesho mtakuwa mmechelewa.
1. Ipo haja ya kumchallenge rais Magufuli kwa nguvu zote kwenye uchaguzi wa october 2020
Si vyema kumpa rais Magufuli ushindi wa mezani, ushindi lainilaini ushindi wa kupewa, Ni lazima awekwe mtu mwenye charisma zaidi, mwenye historia ya kutukuka zaidi katika utumishi wa wananchi ili ashindane naye, Ili raisi Nagufuli naye aumize kichwa, atumie muda wake kutafuta kura za wananchi, aende kwa wananchi awaangalie machoni na kuwaambia kuwa niliahidi kadha wa kadha na nimetekeleza moja, mbili, tatu. Kutomchallenge Magufuli ni kumfanya ajihisi invinsible na hii inaweza kuathiri utendaji wake iwapo atashinda uchaguzi kwa kuamini kuwa alikuwa entitled kwenye uraisi badala ya kujua kuwa yeye kuwa hapo ni kwa sababu ya ridhaa za watu. Kwa sasa sioni mtu aliyejiandaa kumkabili raisi Magufuli kwenye sanduku la kura kuliko Membe
2. Upo umuhimu wa kupata uungwaji mkono wa kimyakimya kutoka kwa makundi yasiyomkubali Magufuli ndani ya CCM (Latent support)
Rais Magufuli anao mahasimu wake wa kisiasa ndani na nje ya CCM. The best thing cha kufanya sasa hivi ni kuunganisha nguvu hizi mbili, moja ya dhahiri na nyingine ya siri. Ili kuerode cohesion ya CCM katika kuelekea uchaguzi mkuu, ipo haja ya kukifanya chama kizima kisiwe united firm chini ya Magufuli, kuna haja ya kuwa na support ya mtandao wa kimya kimya, Kwa sasa sioni hata kidogo mtu kutoka upinzani anayeweza kuexploit ufa huu ndani ya CCM zaidi ya mtu aliyekuweko ndani ya CCM, anayeijua CCM na ambaye ameonyesha nia ya kuchallenge status quo. Katika hili sioni mtu mujarrabu anayeweza kuifanya kazi hii kuliko Membe
3. Msiogope Lowasa precedence (kuhama kisha kurudi CCM)
Lowasa na Membe ni stori mbili tofauti, mmoja alikatwa kugombea urais, hakufukuzwa chamani akaamua kukimbilia upinzani kutafuta urais, huyu wa pili kafukuzwa humohumo ndani ya Chama kwa hila kisa tu kasimama kidete kumchallenge bwana mkubwa na pia kaonyesha nia thabiti ya kugombea uraisi ili aje awatumikie Watanzania. Kwa hiyo katika kumuevaluate Membe inabidi mumuone kama mtu shujaa aliyekuwa tayari kusimama na kumwambia mfalme kuwa hautoshi, umetukwamisha sana, umetuingiza chaka sana, umetupeleka maboya sana, sasa tunataka kuingia hapo ulipo ili turekebishe mambo. Huyu mtu ni mtu jasiri, ameonyesha ujasiri hata pale ndani ya chama chake walipoufyata, kwa hiyo huyu mtu siyo wa kuacha hivi hivi. Huyu mtu anafaa kushika bendera ya ACT na kuipeperusha vyema kumng'oa bwana mkubwa. Msiogope kelele za hofu kuwa akija Membe itakuwa kama ilivyokuwa Lowasa alipohamia CHADEMA. Lowasa na Membe kihulka ni watu wawili tofauti
4. ACT Wazelendo ni chama cha Wahanga wa kisiasa, Ni Tanga la kunusuru waliotoswa baharini kionevu
Kuanzia kuondoka kwa Kiongozi mkuu wa Chama mheshimiwa Zitto Kabwe kwenye chama chake cha awali, Kuja kwa Maalimu Seif na wengineo, Kwa nini iwe nongwa kumchukua Membe?. Membe siyo liability, Membe ni assett, Na asset yake kubwa ni uzalendo na utumishi uliotukuka kwa nchi hii. Membe hana hela, lakini ana plan ya kuwaondoa wananchi katika mserereko wa uchumi, katika limbwi la siasa za hofu, siasa za kununua watu utafikiri tupo kwenye slave trade, kufeli kwa diplomasia, kuonea watu, kudhalilisha watu na siasa za one man show
5. Membe ana sifa, vigezo na uwezo wa kuwa raisi mzuri kwa nchi yetu
Hapa tulipo tunahitaji mtu atakayeunganisha Taifa, kuponya majeraha, kurekebisha uchumi wa nchi na kuturudishia siasa za utu. Kwa kweli sioni mtu nje na ndani ya CCM mwenye uwezo huu kwa sasa isipokuwa Membe
ACT Wazalendo, tuleteeni Membe aturekebishie nchi yetu, Tunaweza kumvumilia Membe kuja Upinzani na kutuongoza kumg'oa Magufuli kuliko kuendelea na miaka mingine mitano ya aina ya uongozi wa utawala huu uliofeli wa awamu ya tano!