jembe afrika
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 7,602
- 3,782
Kwa hali niliyoiona na matamshi ya huyu meneja wa kampeni Mungu amsamehe tu. Sidhani kama kuna mtu mwenye bima ya kudumu ya afya chini ya hili jua. sikatai siasa ni kuchafuana na si kumcheka na kumdhihaki eti ana degedege au kifafa, juzi nikiwa hospital nilimuona mtoto anaanguka kifafa na akakauka hii hali ilinitoa machozi. Lakini mtu mwingine ndo mtaji wa kujizolea sifa huo ni upumbavu.
Ni heri angemuita Lowassa fissadi na si suala la afya, CCM siipendi ila Magufuli kampeni ya naisifia maana hatukani mtu yeye anatangaza sera ingawaje yeye hakutakiwa kutangaza sera alichotakiwa atueleze wezi wa Escrow wamewafanyaje, mpaka sasa uchumi wa nchi ukoje na si kutangaza sera mpya na za awali hujazimaliza.
Suala hapa wananchi tunataka sera. Hongera Lowasa, Magufuli na Zitto kwa kutumia jukwaa kistaarabu bila matusi. Narudia tena afya ya mtu mwachie Mungu, mkosoe mtu kwa matendo.
Nakupa pole Zitto Kabwe kwa kuwa na meneja anayetamani hasira ya Mungu kwa kulazimisha.
Jembe Afrika..