GE2025 ACT Wazalendo inakwenda kuwa Chama Cha pili kuongoza Dola Tanzania

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo Luhaga Mpina, amesema kuwa uteuzi wake kuwa mgombea urais kupitia chama hicho ni mwanzo rasmi wa safari ya kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani, akisisitiza kuwa Watanzania wanataka katiba mpya na haki ya kweli ya kuamua hatima ya nchi yao.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa ACT Wazalendo uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam muda mchache kabla ya wajumbe hao kumchagua kuwa mgombea wa chama hicho, Mpina alisema: “Mkimpata Luhaga Mpina akawa mgombea wa kuipeperusha hii bendera ya ACT Wazalendo kazi imekwisha, safari ya kwenda kuing’oa CCM itakuwa imeiva leo na leo hii chama hiki kinaenda kuandika historia ya kuwa chama cha pili kuongoza dola nchini Tanzania.”

Mpina alilaani vikali kile alichokiita “danadana zisizo na msingi” kuhusu mchakato wa katiba mpya, akisema serikali iliyopo madarakani inawanyima Watanzania haki yao ya msingi.
 
Na anafikiri chama chake alichokikimbia (sisiemu) watakubaliana nae kiwepesi? Ana kazi ya ziada ~ Wacha tuone
 
Hivi humu jamii forums hakuna wanasiasa , watuelezee jinsi wanavyotuchukulia au kutuona wananchi wa kawaida.?
Maana wengi ukitafakari mambo yao hupati jibu wanatuchukuliaje.
 
Labda wamfukuze Zito. Maadam Zito anendelea kuwa mwenye sauti ndani ya ACT, sawa na ilovyo kwa Msoga ndani ya CCM, ACT itaendelea **** mamluko cha CCM. Mchana ACT watakuwa wanapanga mipango yao, mwenzao Zito jioni atakuwa na Saa 100 akimweleza walichopanga.
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo Luhaga Mpina, amesema kuwa uteuzi wake kuwa mgombea urais kupitia chama hicho ni mwanzo rasmi wa safari ya kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani, akisisitiza kuwa Watanzania wanataka katiba mpya na haki ya kweli ya kuamua hatima ya nchi yao.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa ACT Wazalendo uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam muda mchache kabla ya wajumbe hao kumchagua kuwa mgombea wa chama hicho, Mpina alisema: “Mkimpata Luhaga Mpina akawa mgombea wa kuipeperusha hii bendera ya ACT Wazalendo kazi imekwisha, safari ya kwenda kuing’oa CCM itakuwa imeiva leo na leo hii chama hiki kinaenda kuandika historia ya kuwa chama cha pili kuongoza dola nchini Tanzania.”

Mpina alilaani vikali kile alichokiita “danadana zisizo na msingi” kuhusu mchakato wa katiba mpya, akisema serikali iliyopo madarakani inawanyima Watanzania haki yao ya msingi.
View attachment 3435245
Sawa ndugu dua za,bibi,ila sijajua dua za babu zinasemaje je kwa maslahi ya taifa au wanamtandao.
 
Luhaga ni mwanasiasa muadilifu ila bahati mbaya amejiunga kwenye kikundi cha wahuni. ACT Wazalendo na ccm lao moja.

Hata marehemu Membe alisema hivyo hivyo ila alipoa upesi kutokana na uhalisia aliokumbana nao.

#KataaWahuni
 
Mpina umepoteza heshima yako bora ungeunda chama chako,yaani amejipaka tope la ajabu.
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo Luhaga Mpina, amesema kuwa uteuzi wake kuwa mgombea urais kupitia chama hicho ni mwanzo rasmi wa safari ya kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani, akisisitiza kuwa Watanzania wanataka katiba mpya na haki ya kweli ya kuamua hatima ya nchi yao.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa ACT Wazalendo uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam muda mchache kabla ya wajumbe hao kumchagua kuwa mgombea wa chama hicho, Mpina alisema: “Mkimpata Luhaga Mpina akawa mgombea wa kuipeperusha hii bendera ya ACT Wazalendo kazi imekwisha, safari ya kwenda kuing’oa CCM itakuwa imeiva leo na leo hii chama hiki kinaenda kuandika historia ya kuwa chama cha pili kuongoza dola nchini Tanzania.”

Mpina alilaani vikali kile alichokiita “danadana zisizo na msingi” kuhusu mchakato wa katiba mpya, akisema serikali iliyopo madarakani inawanyima Watanzania haki yao ya msingi.
View attachment 3435245
kwa tume hii hii ya Bi Kizimkazi?

Keep Dreaming mwabeja
 
JWTZ wanatuangusha sana Watanganyika, nchi imeiva kwa mapinduzi ya kijeshi kwani njia za kistaarabu na kidemokrasia zimefungwa kuwaondoa wakoloni weusi CCM madarakani.
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo Luhaga Mpina, amesema kuwa uteuzi wake kuwa mgombea urais kupitia chama hicho ni mwanzo rasmi wa safari ya kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani, akisisitiza kuwa Watanzania wanataka katiba mpya na haki ya kweli ya kuamua hatima ya nchi yao.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa ACT Wazalendo uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam muda mchache kabla ya wajumbe hao kumchagua kuwa mgombea wa chama hicho, Mpina alisema: “Mkimpata Luhaga Mpina akawa mgombea wa kuipeperusha hii bendera ya ACT Wazalendo kazi imekwisha, safari ya kwenda kuing’oa CCM itakuwa imeiva leo na leo hii chama hiki kinaenda kuandika historia ya kuwa chama cha pili kuongoza dola nchini Tanzania.”

Mpina alilaani vikali kile alichokiita “danadana zisizo na msingi” kuhusu mchakato wa katiba mpya, akisema serikali iliyopo madarakani inawanyima Watanzania haki yao ya msingi.
View attachment 3435245
Japo muda ndio mwamuzi, la msingi hoja zake, ndani na nje ya Bunge, zitatikisa kwenye majukwaa ya kampeni
 
kwa tume hii hii ya Bi Kizimkazi?

Keep Dreaming mwabeja
Mbinu zitatumika kumweka madarakani lakini hatoweza kumaliza muda wake wa utawala, kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake
 
Back
Top Bottom