ACT-Wazalendo Dar kufanya maandamano ya amani kumuunga mkono Rais Magufuli

Hiki chama kimejaa uzalendo mtupu. Zitto atleast tunaona kwenye makosa anakosoa kwenye mazuri anasifia hizi ni siasa mpya kabisa za upinzani Tanzania na nna uhakika kwa uongozi huu wa Magufuli Zitto ndio mpinzani atayeeleweka na raia.

Mlisimamisha Wagombea Ubunge kila Jimbo hivi mlishinda Majimbo mangapi vile? na Urais mgombea wenu alipata kura asilimia ngapi vile?
 
ACT-frr.jpg

CHAMA cha ACT- Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, umeandaa maandamano ya kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika mapambano yake dhidi ya rushwa, ufisadi na kusimamia ukusanyaji kodi kama ilani ya chama hicho inavyosema.

Katibu wa chama hicho, mkoani humo, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, aliyasema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuongeza kuwa, wamemuandikia barua Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadiki ili kumuomba ayapokee maandamano hayo ya amani.

"Tumepanga kufanya maandamano hayo Desemba 16 mwaka huu, tukianzia katika ofisi zetu za Mkoa eneo la Keko Maduka Mawili na kuishia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ilala Boma," alisema.

Alisema lengo lingine la kufanya maandamano hayo ni kumtaka Rais asimamie uongozi bora wenye lengo la kuirudisha nchi kwenye misingi iliyoasisiwa na wazee Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume.

Aliongeza kuwa, ilani ya chama chao ukurasa wa saba inaelezea ndoto ya ACT-Wazalendo ni kuona Taifa linajitegemea kiuchumi, kiutamaduni, kudumisha usawa, ustawi wa jamii, uwajibikaji, demokrasia, uongozi bora.

Mhandisi Ngulangwa alisema chama hicho kinaamini kuwa, mambo hayo yatatekelezwa vizuri kama nchi itajiwekea miiko ya uongozi kama inavyoelezwa na Azimio la Tabora lililohuishwa kutoka Azimio la Arusha.

"Lengo lingine ni kumuomba Rais ahakikishe nchi kupitia mamlaka husika, inasimamia mfumo wa matumizi ya fedha kama inavyosema katika ilani ya chama chetu ukurasa wa 23.

"Hata hivyo, yote hayatakuwa na maana kama mfumo wa fedha kupitia benki utakuwa umeshikwa na wageni kwani nchi yetu haiwezi kuendelea ikiwa benki kubwa zitakuwa zimebinafsishwa," alisema.

Alisema uanzishaji benki uliofanyika mwaka 1967 na kuundwa kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benki ya Nyumba na Benki ya Maendeleo Vijijini ni maamuzi ya msingi kwa maendeleo ya nchi.

nchi nzima mbunge mmoja hata aibu zito aoni msaliti
 
Kuna uzalendo na kuna unafiki. Uzalendo ni kuandamana kushinikiza majibu juu ya suala la Zanzibar. Unafiki ni kuunga mkono mambo ambayo tayari yanafanywa. Wangekuwa wapo serious wangeandama kabla. Hii inaitwa...."jumping on the bandwagon"
 
ndio tunataka upinzani wa kweli sio upinzani wa uhasama na kununuliwa kwenye ukweli semeni kwenye matatizo semeni
 
Hivi jeshi la polisi limeshaanza kuruhusu mikusanyiko ya kisiasa? Maana tuliambiwa imepigwa marufuku hadi itakapotangazwa maana hali nchini bado ni tete kufuatia uchaguzi mkuu wa Oktoba 25.

Imekatazwa ya wapinzani bali ya ccm na wapambe wao ni ruksa.
 
Act wazalendo kinacho ongozwa na MH.Zitto kabwe ni chama kisicho kuwa na Msimo hasa kwa kiongozi wake Mkuu Zitto Kabwe ambae maranyingi amekua akikaririwa na Kuonekana Nimtu wakubadilika badilika Hasa kwa Issue kama ya Urais Zanzibar

Nirahisi sana kwa Act kufanya Maandamano ya kumpongeza makufuli ila siyo rahisi kwa Act kufanya Maandamano ya kumtaka Magufuli atatue Mgogoro wa Kisiasa unaoendelea Zanzibar

Kwakua wao hufanya jambo kwa kuipendeza ccm ila siyo kuiwajibisha serikali.
Hivyo napenda kumshauri Zitto ajiandae kisaikolojia kupokea kikombe kama cha mrema cheyo na sibuda.
 
ACT-frr.jpg

CHAMA cha ACT- Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, umeandaa maandamano ya kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika mapambano yake dhidi ya rushwa, ufisadi na kusimamia ukusanyaji kodi kama ilani ya chama hicho inavyosema.

Katibu wa chama hicho, mkoani humo, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, aliyasema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuongeza kuwa, wamemuandikia barua Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadiki ili kumuomba ayapokee maandamano hayo ya amani.

"Tumepanga kufanya maandamano hayo Desemba 16 mwaka huu, tukianzia katika ofisi zetu za Mkoa eneo la Keko Maduka Mawili na kuishia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ilala Boma," alisema.

Alisema lengo lingine la kufanya maandamano hayo ni kumtaka Rais asimamie uongozi bora wenye lengo la kuirudisha nchi kwenye misingi iliyoasisiwa na wazee Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume.

Aliongeza kuwa, ilani ya chama chao ukurasa wa saba inaelezea ndoto ya ACT-Wazalendo ni kuona Taifa linajitegemea kiuchumi, kiutamaduni, kudumisha usawa, ustawi wa jamii, uwajibikaji, demokrasia, uongozi bora.

Mhandisi Ngulangwa alisema chama hicho kinaamini kuwa, mambo hayo yatatekelezwa vizuri kama nchi itajiwekea miiko ya uongozi kama inavyoelezwa na Azimio la Tabora lililohuishwa kutoka Azimio la Arusha.

"Lengo lingine ni kumuomba Rais ahakikishe nchi kupitia mamlaka husika, inasimamia mfumo wa matumizi ya fedha kama inavyosema katika ilani ya chama chetu ukurasa wa 23.

"Hata hivyo, yote hayatakuwa na maana kama mfumo wa fedha kupitia benki utakuwa umeshikwa na wageni kwani nchi yetu haiwezi kuendelea ikiwa benki kubwa zitakuwa zimebinafsishwa," alisema.

Alisema uanzishaji benki uliofanyika mwaka 1967 na kuundwa kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benki ya Nyumba na Benki ya Maendeleo Vijijini ni maamuzi ya msingi kwa maendeleo ya nchi.

ccm-act= concubinage
 
ACT na CCM ndio wale wale, watanzania msidanganywe na tofauti ya kijani na zambarau!
 
Kila chama kina misingi yake yakufikisha hisia zake kwa wananchi, pia si lazima ukubali wanalolifanya act, maana wako huru nje kabisa ya ukawa...zitto lazima awe mbunifu kukitangaza chama...
 
Back
Top Bottom