ACT-Tanzania yang'ara vijijini zaidi

ACT-Tanzania yang'ara vijijini zaidi

ACT-Tanzania Vijijini na thabiti.

Chama cha Tanu kilifanikiwa haraka kwa sababu kilijikita vijijini zaidi kuwaelimisha wananchi kukijua na kulitambua taifa lao, nimeanza ziara rasmi maeneo tengevu ya nchi yetu kueneza chama chetu cha ACT-Tanzania,
Nimefarijika sana kuona chama cha ACT-Tanzania kimemea na kuanza kuchipua maeneo tengevu (remote areas) tunaungwa sana mkono maeneo ya kando kuliko vyama vyote ikiwemo chama tawala,
Tuna wagombea wengi zaidi maeneo ya kando kuliko mijini,
Yapo maeneo tunawagombea wanaopambana na ccm wala hakuna wagombea wa vyama vingine.
Na kwa sababu chama chetu kimeanza na misingi sio malengo na madhumuni kama vingine ndio sababu ya sisi kukubalika haraka na kueleweka vyema.

Idara ya ITIKADI, UENEZI NA MAHUSIANO YA JAMII inawapongeza wanachama wote wa ACT - Tanzania na watanzania wote kwa kazi nzuri ya kueneza chama.
Idara ya uenezi inawaasa kuhakikisha juhudi hizi zinazaa matunda, nahimiza tujitokeze kupiga kura na kuzilinda.
Nyakarungu Grayson
Katibu Itikadi,Uenezi na mahusiano ya jamii.
+255 755 023 503





Bosi mkubwa wa ACT Tanzania vipi kuhusu kuwavua gamba Mkumbo na team yake imeishia wapi? Hebu tuweke sawa kwanza kabla ya hizi mbwembwe za vijijini wakati magamba yamegomea kutoka!
 
Safari njema kuelekea maeneo tengefu.
Kwani haujahitimu chuo mwaka huu Mzumbe?
 
Act-Tanzania inamea vijijini, angalieni isijekuwa mmepanda mbegu janfwani mkitegemea zitamea na kukita mizizi ardhini pasipo na unyevu
 
Nyakurungu zile risit feki za malipo ya bank uliyofanya mzumbe umemalizanaje? Na kwanini hujagraduate mwaka huu? Unafikiri kwa uliyofanya mzumbe unatosha hata kupost hili bandiko hapa?

Mkuu hebu funguka nimependa hii
 
Hivyo vijiji vipo wapi? Na je,havina majina? Mimi nafanyia shughuri zangu vijijini hapa Magu,toka KISESA hadi MAHAHA sijaona wala kuskia mgomboa wa ACT.Au mleta mada alimaanisha vijiji vya Burundi?
 
Back
Top Bottom