ACT-Tanzania , Taarifa Mkononi mwako

ACT-Tanzania , Taarifa Mkononi mwako

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
643
Reaction score
1,603
Ndugu watanzania wote, tunawasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi.

Katika kusimamia dhana ya uwazi na kuhakikisha kwamba kila anayependa kupata taarifa mbali mbali kuhusu chama cha ACT-Tanzania, anazipata kikamilifu, kwa haraka, kwa ufanisi na bila usumbufu mkubwa, tunawaomba watanzania wote wanaopenda kupata taarifa mbali mbali za chama cha ACT- Tanzania, watutumie barua pepe zao au namba zao za simu.

ACT-Tanzania tunatumia na tutaendelea kutumia mbinu mbali mbali ili kujitahidi kuwafikia watanzania wengi iwezekanavyo (ikiwezekana watu wazima wote na wenye akili timamu), kwa haraka, kwa ufanisi, bila usumbufu mkubwa na kwa kujaribu kutumia njia ambazo ni za gharama nafuu zaidi.

Miongoni mwa mbinu ambazo baadhi tumeanza kuzitumia na tutakuwa tunazitumia kuwafikia watanzania ukiacha mikutano ya hadhara, ni pamoja na hii ya kupitia simu zenu, barua pepe zenu, tovuti ambayo tutaifungua karibuni, vitabu, vipeperushi (brochures), mitandao ya kijamii na kadhalika.Tutakuwa tukiboresha mifumo yetu ya mawasiliano kila mara kulingana na uwezo wetu ili watanzania waweze kuyafaidi matunda ya chama chao wakati wote.

NB. Kwa sasa kuna vijitabu vidogo (Brochures) tunagawa vinavyoeleza mambo muhimu yanayohusiana na ACT-Tanzania kwa muhtasari.Kama mtu anahitaji "soft copy", atatutumia e-mail yake na kama anataka "Hard Copy" atasubiria kidogo hadi tutakapoingia mtaani kwake.

ACT-Tanzania.................Taifa kwanza leo na kesho!,
Mabadiliko na Uwazi.........Chukua Hatua!.

Tuwasiliane kwa acttanzania@yahoo.com au acttanzania@gmail.com.
 
Asante comred kwa hizi taarifa njema kuna wahuni watakuja hapa lakini sisi tuwajibu kwa adabu.
 
Last edited by a moderator:
ACT Ni chama cha kisasa zaidi..kinaendesha mambo yake kidigitali...chama makini cha ACT NI MKOMBOZI WA MTANZANIA
 
ACT Ni chama cha kisasa zaidi..kinaendesha mambo yake kidigitali...chama makini cha ACT NI MKOMBOZI WA MTANZANIA
Hebu tuambie itkadi ya ACT ni ipi?Na pia kwa faida ya Wana JF tuambie wewe ni mwanachama wa chama gani?
 
Hebu tuambie itkadi ya ACT ni ipi?Na pia kwa faida ya Wana JF tuambie wewe ni mwanachama wa chama gani?
mkuu wewe unaijua itikadi ya ACT-Tanzania, maana hatari iliyopo ni kwamba kama utakuwa unamuuliza mwenzako wakati nawe hujui, hata ikitokea ukidanganywa; itakuwa ni vigumu kugundua.Kama wewe tayari unaelewa jibu la swali ulilouliza, basi hamna shida kaka!
 
waizi tu siibiwi tena.
kweli kabisa ndugu, usiwape namba yako kabisa maana ukiwapa namba yako ya simu watakuibia simu yako, halafu ukiwapa parua pepe watakuibia E-mail yako. Yaani ni hatari sana! usikubali kabisa mkuu!
 
Hiki chama mlichemka mlipoanza kujenga msingi wa uhalali wenu kwa ku-attack Chadema.

I am not a politician but I know one when I see one. Wote ni wale wale wenye njaa tuu.

Baadala ya kujenga hoja mnakuja na nyimbo zile zile zilizochoka za kuattack personalities. My point is, Chadema might be weak and a failure in its agenda (by the way, I dont agree with many of their approach to politics). Lakini hiyo haiwahusu. Kikubwa kwenu ni kuhakikisha wananchi wanaelewa mnachosimamia. Kusimama jukwaani na kuanza kuwatukana CHADEMA naona ni ukosefu wa fikra. Na I suspect you are simply marceneries paid to spoil things.

Mimi Masanja naona hiki chama ni reactionary. Just losers kwenye vyama vingine. Basically you are trying to show Chadema na wengineo kwamba na nyinyi mna chama kwa hiyo hata kama waliwafukuza..you can as well establish your own party. No roots. No values..simply to confuse us poor wananchi.

I will be pleasantly surprised if you prove me wrong.

Masanja
 
Asante comred kwa hizi taarifa njema kuna wahuni watakuja hapa lakini sisi tuwajibu kwa adabu.
Mkuu, mtu yeyote mwenye akili anapokutana na mtu mshari, humjibu kwa salama! mara nyingi mtu mwenye hekima hapayuki payuki bali huongea kauli thabiti kwa sauti ya chini na yenye utulivu mkubwa lakini huwa mara nyingi inakuwa nzito (kama anayezungumza ni mwanaume). Basi hapo utakuta watu wote kimyaaa! ni hivyo tu mkuu, kwa kawaida haki inaposimaa batili hujitenga kwa kuwa haki na batili daima hazichangamani.je! ni kwa vipi tunaweza kumtofautisha yule anayejua jambo dhidi ya yule asiyefahamu jambo?

Hiki chama mlichemka mlipoanza kujenga msingi wa uhalali wenu kwa ku-attack Chadema.
Mtu mwenye akili ni yule ambaye pale anapokuwa hafahamu jambo lakini apatapo kufahamishwa, huelewa na akakifanyia kazi kile alichokielewa ikiwa ni pamoja na kuwaelewesha wengine, lakini mtu mjinga, ni yule asiyejua kitu ila hata anapofahamishwa kitu haelewi wala hana nia ya kuelewa, lakini ataelewaje na wakati hajui, na hajui kwamba hajui!?

riziki magembe amepewa kazi ya kuichafua act mitandaoni...unajisumbua tu utashindana lakini utashindwa
 
riziki magembe amepewa kazi ya kuichafua act mitandaoni...unajisumbua tu utashindana lakini utashindwa
Kila ajaye kwa shari,

Kwa hakika Mungu aijua vyema yake siri,

Na ana uwezo wa kuivunja yake dhamiri,
Na wala asiweze kusimama!

Ndugu watanzania wote, tunawasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi.

Katika kusimamia dhana ya uwazi na kuhakikisha kwamba kila anayependa kupata taarifa mbali mbali kuhusu chama cha ACT-Tanzania, anazipata kikamilifu, kwa haraka, kwa ufanisi na bila usumbufu mkubwa, tunawaomba watanzania wote wanaopenda kupata taarifa mbali mbali za chama cha ACT- Tanzania, watutumie barua pepe zao au namba zao za simu.

ACT-Tanzania tunatumia na tutaendelea kutumia mbinu mbali mbali ili kujitahidi kuwafikia watanzania wengi iwezekanavyo (ikiwezekana wat u wazima wote na wenye akili timamu), kwa haraka, kwa ufanisi, bila usumbufu mkubwa na kwa kujaribu kutumia njia ambazo ni za gharama nafuu zaidi.

Miongoni mwa mbinu ambazo baadhi tumeanza kuzitumia na tutakuwa tunazitumia kuwafikia watanzania ukiacha mikutano ya hadhara, ni pamoja na hii ya kupitia simu zenu, barua pepe zenu, tovuti ambayo tutaifungua karibuni, vitabu, vipeperushi (brochures), mitandao ya kijamii na kadhalika.Tutakuwa tukiboresha mifumo yetu ya mawasiliano kila mara kulingana na uwezo wetu ili watanzania waweze kuyafaidi matunda ya chama chao wakati wote.

NB. Kwa sasa kuna vijitabu vidogo (Brochures) tunagawa vinavyoeleza mambo muhimu yanayohusiana na ACT-Tanzania kwa muhtasari.Kama mtu anahitaji "soft copy", atatutumia e-mail yake na kama anataka "Hard Copy" atasubiria kidogo hadi tutakapoingia mtaani kwake.

ACT-Tanzania.................Taifa kwanza leo na kesho!,
Mabadiliko na Uwazi.........Chukua Hatua!.

Tuwasiliane kwa acttanzania@yahoo.com au acttanzania@gmail.com.

Sawa!!
 
Tunaomba ACT muishi kadri ya msingi wa UWAZI ambao utawatofautisha na vyama vingine.

Kwa kuanzia wekeni wazi mambo ya pesa zilizogharimia usajili.

Nani walichangia, na kwa kiasi gani, na zilitumikaje.

UWAZI mkiuweka katika matendo mtatupata wanachama wengi.
 
Mimi sio mtaalamu sana wa mambo ya uhasibu lakini nilishawahi kuambiwa na mtaalam mmoja wa mambo ya fedha kwamba mara nyingi taarifa za mapato na matamizi ya taasisi, hutolewa katika vipindi vya robo mwaka, nushu mwaka, robo tatu na mwaka.Sasa sijui kama alichokuwa ameniambia kilikuwa ni ukweli au laa! nadhani wataalam wa mambo ya uhasibu wanaweza kutusaidia ujuzi katika eneo hili, ila kama ilikuwa ni ukweli na kama ACT-Tanzania watakuwa wanafuata utaratibu huo wa kitaalam (kama itakuwa kweli ndivyo unavyotakiwa uwe), basi bila shaka wanaweza wakatoa baada ya kufikisha robo mwaka! pengine tusubiri kidogo halafu tuone kama ACT- Tanzania itafanya hivyo au laa!

Au una taarifa tofauti na hiyo, juu ya muda ambao taasisi hutakiwa kutoa taarifa zake za mapato na matumizi ili tuweze ku-share ujuzi?

Back
Top Bottom