ACT-Tanzania na Msingi wa Utu

mimi najua neno moja 2 kuwa hili nigege la wasaka madaraka 2 basi
 
ulikuwa unamaanisha neno utu wanrifaa propaganda za kijinga walizokuwa wanafanya watu kwa msiba uliotokea kama ni hivyo kweli watakuwa mabogasi....................

Ndio kaka, hujawasoma in between the lines, si umesikia wakisema chadema hawana utu, sijui hawakwenda kumwona mgonjwa sijui hawakwenda msibani, na hawa jamaa wakaja na bandiko lao hapa eti kujionesha kwamba wao wana msingi wa utu! Utu gani huo? Wangekuwa na utu wangemdhalilisha Mbowe kiasi kile kwenye waraka wao wa siri? Kiongozi wao Zitto angemtukana mwenyekeiti wake?
 
ungependa wafe eh! ok! watakufa tu hamna shida.wala usiwe na wasiwasi,wewe Endelea kuomba tu mkuu! kuna siku maombi yatakubaliwa.
betlehem nimependa unavyowajibu hawa wahuni wa ufipa nendanao taratibu wataelewa somo.
 
Last edited by a moderator:
Binafsi mimi sio mwanachma wa ACT na sitarajii kujiunga nacho hivi karibuni, but iam impressed na Jinsi ulivyojibu bila jazba, nawaomba sana ninyi mnaohusika na uenezi kujitahidi kutumia lugha nzuri hata pale inapotokea mmekashifiwa au vyoyote
 
Kule duru za siasa tumeongelea jinsi ambavyo chama hiki kinaanza kwa matatizo.https://www.jamiiforums.com/great-t...a-cha-act-mpini-wa-ccm-kumaliza-upinzani.html

Ukisoma kwa juu juu sana, unaweza kudhani hawa jamaa wanaanza kueneza sera au taratibu zao.Hapo mwisho anasema ''Tutakuwa tukitolea ufafanuzi misingi ya chama....' ili kuwafumba watu macho kwa kile walichodhamiria.

Sina tatizo na maoni yao au misimamo yao. Wana haki ya kueleza na kujieleza katika jamii na hilo si kosa.

Tatizo ninaloliona kwa ACT ni wao kusema ni wa WAZI wakati amabapo wanawafanya Watanzania wapuuzi na mazuzu.
Hapa ndipo ninaposimamia.

Mada yote hiyo haizungumzii misingi ya ACT, kinachozungumziwa ni tukio la msiba la 'mwanachama' wa ACT na tofauti za kisiasa zilizojitokeza miongoni mwa mfiwa na wanasiasa wa chama chake. Hapo ndipo nasema hakukuwa na sababu za kuzunguka na kuwafanya watu wajinga.

ACT wangeweza kusema Zitto kafiwa na mama yake na viongozi kadhaa hawakuhudhria. Straight foward na hilo lisingekuwa tatizo kwasababu wanatoa maoni yao na wana haki hiyo.

Walichokifanya si uwazi, ni kutaka kutufanya mazuzu. Hiki chama nimesema kimeanza na matatizo makubwa ya kuwa na kitu kinachoitwa 'PR'. Mahusiano katika jamii ni jambo muhimu sana. Haionekani kama wana hicho kitu katika chama chao.

ACT katika wakati huu ingejiepusha sana na mizozo au sintofahamu ikizingatiwa kuwa viongozi wake wamebeba mafurushi machafu migongoni mwao. Wana bifu na sehemu ya jamii na ili kuondoa sintofahamu na kutoa nafasi kwa chama kujieneza, ACT wanapaswa kujikita katika siasa na si migongano isiyo na tija.

ACT wanapokuwa na mambo rahisi au majitaka namna hii, hata siku watakapoeleza jambo la maana litatiliwa shaka kwasababu hawasimami katika misingi na kauli mbiu ya chama chao, UWAZI

Ningewaelewa kama mngetoka na ku-criticise CDM moja kwa moja. Pengine tungekuwa tunawaunga mkono kwa mambo mawili, moja,uwazi wenu na pili mada yenu. Huo ndio ukomavu.

Hizi siasa za Waraka zime prove kuwa failure kubwa, hamuonekani kujifunza.

Please go back to the drawing board. Mnafanya siasa za mwaka 1905. Kinjekitile anaonekana smart zaidi yenu
.

UWAZI wenu upo wapi? Mtaendelea na siasa za kujificha ficha hadi lini? kwanini mnazidhulumu nafsi zenu kuongea, mkibana punzi na kuongelea matumboni?
 

Kaka umeongea maneno ya maana sana. Nia aibu kwa chama kuhubiri utu bila kujua kuwa wanachofanya ni kumtumia marehemu kujitafutia umaarufu. Je ni utu kumtumia marehemu kujitangaza sera zenu? Hapa ACT mmepotoka.
 
Jana hamkuonekana kwenye maziko Kigoma
 
betlehem nimependa unavyowajibu hawa wahuni wa ufipa nendanao taratibu wataelewa somo.

mkuu, vitabu vitakatifu vinatufundisha kwamba unapokutana na mtu mshari,mjibu salama kwani historia inatuonesha kwamba kuna watu waliwahi kuwa wabaya sana ila hatimae wakauona mwanga na wakabadilika kuwa watu wazuri.
 
Last edited by a moderator:
Nyie mtakuwa kama kile chama cha sijui CCK au sijui CCJ.

Mtakufa karibuni tu.

vyovyote iwavyo, kikubwa na jambo la msingi ni vema ukaelewa somo hili,,,suala la CCK au CCJ halitakusadia wewe wala sisi,,,,ila ukitambua umuhimu wa kuulinda "utu" wako na kuuthamini utu wa wenzako itakuwa ni jambo lenye faida kwako wewe binfsi na jamii yetu kwa ujumla,,,Mwenezi amefafanua vizuri sana.

 
Nguruvi3

Tatizo lako unasukumwa na mawazo yako yalichanganyika na chuki binafsi,ushauri wangu kwako usiwalishe watu maneno ambayo hayajasemwa.

ACT-Tanzania ni chama kidogo sana kuliko vyama vyote unavyovijua chakushangaza nyie wafuasi wa Chadema povu linawatoka,lakini siwashangai hata CUF mlikuwa mnasema ni CCM B leo vipi?Unafiki ni kitu kibaya sana mara bendera ina nyota hichi chama ni cha kiislamu zile zile sera za CCM mmezibeba.
Nguruvi3 wewe ni katika "great thinker" lakini kwa ulichoandika hapo juu kajipange upya....
 
Last edited by a moderator:

bandiko halijataja chama chochote cha siasa zaidi ya ACT-TANZANIA,, ni ujahili si kama wazimu kuingiza mambo ya misiba na mambo ya vyama vingine katika bandiko ambalo maudhui yake hayahusiani na mambo hayo...pamoja na hayo,,kama kuna vyma havitambui "utu" wa mtu hilo ni tatizo la hivyo vyama na si tatizo la misingi ya ACT-TANZANIA ambayo kila mwana ACT inabidi aape kuiilinda.

 
chama cha mitandao ya jamii, sound nyingi kuliko utekelezaji... hata bendera sijawahi ona, huwa nakiona jf tu...

Ww haupo tz au na ww ulifungiwa kwenye box habari za mujini hujui act ni chama cha kizalendo namini kitaleta mageuzi tena makubwa
Vuwa gamba vuwa gwanda vaa uzalendo
 

Mnaona watu ni wajinga sana eti eh?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…