ACT mkikomaa hivi, mtatoa mfano wa namna mtu kujipatia anachoamini ni chake. Chake mtu, haombi!

ACT mkikomaa hivi, mtatoa mfano wa namna mtu kujipatia anachoamini ni chake. Chake mtu, haombi!

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
Kunaanza kuchangamka. Kwamba?

Gzay7ziXcAAJnIK.jpeg

Mkikaza hii mbona leo tu mtapigiwa simu? Tena na chigogo yule mwenyewe kabisa, ili kama vipi kuwasilisha forms zenu mapema kesho asubuhi na kulikwaa ndinga pendwa la kampeni, kwa raha zenu?

Huu unaweza kuwa wakati mzuri zaidi kwenu kutoa somo kwa vitendo na hasa kwa zile nafsi njoga njoga kama zile za kwetu, zinazotegemea haki kwenye visahani vya fwedha?

Shime shime waungwana, shamba darasa hilo, kwa wote waliopokwa vyao!
 
Kama Mpina ndiye katamka hivyo,itakua hajawasiliana na KIONGOZI MKUU MSTAAFU,maana ZZK hawezi eti akakubali ACT isishiriki uchaguzi,ataishije sasa?

Kwa vile malaika wenye kuandika humu hawapo tuipe muda.

Ila kama wakikomaa, chake mtu haombi!
 
Kunaanza kuchangamka. Kwamba?

View attachment 3456412

Mkikaza hii mbona leo tu mtapigiwa simu na Tena na kigogo yule mwenyewe kuwasilisha forms zenu mapema kesho asubuhi na kulikwaa ndinga lenu pendwa la kampeni tena kwa raha zenu?

Huu unaweza kuwa wakati mzuri zaidi kwenu kutoa somo kwa vitendo na hasa kwa zile nafsi njoga njoga za kwetu zinazotegemea haki kwenye kisahani cha fwedha?

Shime shime shamba darasa hilo, kwa wote waliopokwa vyao!
Kuna wanaosema Mpina alizuiwa kwa sababu alikuwa na mpango wa kumwekea Samia pingamizi, hivyo wakasubiri mpaka muda wa mapingamizi uishe na sasa watamrudisha bila masharti yoyote.
 
Kuna wanaosema Mpina alizuiwa kwa sababu alikuwa na mpango wa kumwekea Samia pingamizi, hivyo wakasubiri mpaka muda wa mapingamizi uishe na sasa watamrudisha bila masharti yoyote.

Iwe isiwe. Wakikomaa na karata hiyo, INEC watake wasitake, mapema asubuhi Mpina kesho anakwaa ndinga la kampeni Kiroho safi.

Haki haiombwi!

Zawadini Panje kule au nasema uongo?
 
Kuna wanaosema Mpina alizuiwa kwa sababu alikuwa na mpango wa kumwekea Samia pingamizi, hivyo wakasubiri mpaka muda wa mapingamizi uishe na sasa watamrudisha bila masharti yoyote.

Wauona mwendelezo huu?

GzcoYocXgAAkOUu.jpeg

Awaye yote aweza kusema atakavyo, ila msingi wa hoja, chake mtu haombi!

Kama si staged basi rungu nyuma ndiyo siri nzima ya mafanikio.

Hata sisi ingekuwa steadfast mboni Simba anangekuwa ana vinjari kwa raha zake?

Haipo ngoma bila ultimatum tena thabiti kweli kweli.

Zawadini kwa utambuzi.
 
Wauona mwendelezo huu?

View attachment 3456502

Zawadini kwa utambizi.
Ndiyo maana nikasema walichokuwa hawataki kitokee kimeshapita, watamrudisha. Hakuwa ameondolewa moja kwa moja. Wanajua hana madhara.
 
Ndiyo maana nikasema walichokuwa hawataki kitokee kimeshapita, watamrudisha. Hakuwa ameondolewa moja kwa moja. Wanajua hana madhara.

Hayo ni maoni yako ila ukweli ni kuwa na rungu nyuma TAL angekuwa nje, reforms zingefanyika na uchaguzi ingekuwa huru na wa haki.

Ninakazia:

Chake mtu, haombi!
 
Hayo ni maoni yako ila ukweli ni kuwa na rungu nyuma TAL angekuwa nje, reforms zingefanyika na uchaguzi ingekuwa huru na wa haki.

Ninakazia:

Chake mtu, haombi!
CCM* kamwe hawatakubali hasa kwenye huu uchaguzi, kufanya marekebisho. Wanajua pasi na shaka kuwa Samia anachukiwa mno mno hivyo hawawezi kucheza na moto. Halafu sasa: kuna ufisadi na madhambi mengi kweli kweli kiasi ambacho kamwe hawakubali mtu asiye kwenye circle yao aingie. (CCM* = sasa hivi ni mtandao unaoongozwa na JK, na wako macho CCM asiye kwenye huo mtandao asije shika urais. Ila 2030 panapo uzima kuna kazi kubwa sana)
 
Wauona mwendelezo huu?

View attachment 3456502

Awaye yote aweza kusema atakavyo, ila msingi wa hoja, chake mtu haombi!

Kama si staged basi rungu nyuma ndiyo siri nzima ya mafanikio.

Hata sisi ingekuwa steadfast mboni Simba anangekuwa ana vinjari kwa raha zake?

Haipo ngoma bila ultimatum tena thabiti kweli kweli.

Zawadini kwa utambuzi.
Kule kwetu huwa tunasema "ngoma ya kitoto haikeshi". Ila niseme tu "kuishi kwingi ni kuona mengi".
 
Kule kwetu huwa tunasema "ngoma ya kitoto haikeshi". Ila niseme tu "kuishi kwingi ni kuona mengi".

Funguka zaidi mkuu, unadhani huu ni mchezo tu? Je Mpina atarejeshwa na mahakama? Mahakama ikidinda, rungu hili la wazalendo waliona je?
 
Back
Top Bottom