Wakuu chama cha ACT kilipomchagua ndugu Zitto kuwa Kiongozi Mkuu wa Chama, tuliletewa hapa Jamvini, Fomu zinazodaiwa kujazwa na kutiwa sahihi na yeye ku-declare mali zake! Tuliambiwa kuwa hiyo ndio sera ya chama na kwamba kila kiongozi atapaswa kufanya hivyo na mambo yatawekwa hadharani! Sina uhakika kama viongozi wengine waandamizi wa chama walishatekeleza hilo au bado wako kwenye mchakato wa kulifanyia kazi! Kwa sasa niombe kama tunaweza kupewa updates juu ya fedha & mali za chama, vyanzo vya chama vya mapato, pamoja na hesabu za mapato na matumizi ya chama kufikia Juni 30, 2015.