Achinja kwa Wivu wa Kimapenzi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,714
2,000
Yametokea mauwaji ya kutisha ktk Kijiji cha Migoli ktk wilaya ya Iringa vijijini,mauwaji hayo yametokana na wivu wa Kimapenzi.
Akiongea na Radio Ebony Fm ya mkoani Iringa,Mwenyekiti wa kijiji cha Migoli ndugu Alamu Mbilinyi amesema mauwaji hayo yametokea siku ya Jumamosi 27/12/2013,ambapo mwanaume anayejulikana kwa jina la Alex Mwanawandembo(34) mkazi wa kijiji hicho amemchinja mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la Anna (23) na kutenganisha kolomeo na kiwiliwili na kisha kumfunika marehemu na blanketi kitandani kwa sababu tu ya wivu mapenzi.
Wakielezea tukio hilo mashuhuda na wakazi wa kijiji cha Migolo,wamesema ndugu Alex alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke huyo kwa mda,baada ya mwanamke huyo kuachika kwa mume wake,mahusiano yao yalikuwa na ugomvi wa hapa na pale baada ya mara kadhaa ndugu Alex kumtuhumu mpenzi wake kukosa uaminifu,hali hiyo ilimuumiza mwanaume aliyeonekana kumpenda kwa dhati.
Siku ya tukio,ndugu Alex ambaye na yeye kwa sasa ni marehemu,alimchinja mpenzi wake wakiwa chumbani,ambapo alimpitishia kisu shingoni na kukata koromeo na tena kumkata sehemu ya mdomoni hadi usawa wa taya,kisha kumfunika na kuingia mtaani.
Aliondoka hadi kwa mama yake na kumwachia kiasi cha pesa ya sikukuu,akamtembelea bibi yake na kumpa kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya kupata kinywaji cha komoni na baadae kuaga kuwa anaenda mtoni kuoga,baadae alipita kwa marafiki zake akiwalalamikia kuwa kuna mtu amemuudhi na atamfanyia kitu kibaya,wakati hayo yakiendelea maiti ya mwanamke ilikuwa chumbani bila majirani kujua.
Baadae Marehemu Alex alirudi nyumbani kwake alipopanga,akawaaga majirani kuwa anahama na kwenda mjini Iringa,anaenda kufunga ndoa ya milele na mpenzi wake Anna...na hawezi kurudi tena na kufanya kazi ya uvuvi ktk bwawa la Mtela,baadae akaenda dukani akanunua dawa ya panya,viroba aina ya vodka na konyagi akanywa huku akijifungia na maiti.
Majirani walishtushwa na sauti ya kukoroma,wakavunja mlango na kujaribu kumnywesha maziwa lkn haikusaidia,na ktk kufunufunua wakagundua na mwili wa mwanamke uliochinjwa kama kuku,marehemu wote wamezikwa ktk makabuli ya kijiji cha Migoli.
Akiongea Mwenyekiti wa Kijiji cha Migoli bwana Alamu Mbilinyi amesema tukio hilo ni la aina yake na halijawahi kutokea kijijini hapo,wamezoea kupatwa na majanga ya watu kuliwa na mamba au viboko ndani ya maji,watu kujinyonga au kuuliwa na tembo poerini na si kuchinjana.Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa RAMADHANI MUNGI amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na upelelezi unaendelea
 

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,919
2,000
Dah! Haya mapenzi hayana mtaalamu kwakweli,wataenda kufunga ndoa huko walikoenda wameona wapambe wengi duniani
 

Heaven on Earth

JF-Expert Member
Mar 21, 2013
37,136
2,000
Aisee............
She was everything to me. She was my soul. You don't always kill a woman or feel jealousy about a woman or shout at a woman because you hate her. No. Because you love her, that's love. My wife was the kind of woman you'd never murder in your life, unless it was for love, because of madness, at that moment, at that moment a person loses everything, he doesn't think, it's a moment of madness. ...

The only thing that I can say is that she was more honest than a Torah Scroll. So why murder someone like that? ... At that moment, you don't remember. You don't remember anything. You don't know what you're doing. Love makes a person stupid. Or maybe, maybe it's not worthwhile loving a woman so much. Maybe you have to love less, less madly, that's the madness of love. ...
 

byb sac

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
910
500
ee mungu tuokoe wana wako.tupe uwezo wa kufikiri na uvumilivu...R.I.P marehemu Anna..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom