Achilia mbali ruzuku na michango, CCM ina vyanzo gani vya mapato?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,784
20,155
Hivi ccm wana vyanzo gani vya mapato vya kujenga kumbi za mikutano, kugharamia mabango, kuendesha chama kwa anasa wakati watanzania wakifa kwa njaa
Karibuni nyote tujadili
Haiwezekani maviwanja hata hayaingizi mapato waseme ndo huko wanapata no, no
Wanapata fedha za kufuru hivyo?
Lumumba nataka jibu
 
Wapiga dili kila uchaguzi ukikaribia wanatengeneza kashfa na watu za kupiga hela.ESCROW,LUGUMI,kabla ya hapo Deep Green,EPA,zote ni dili za kupata pesa ya kuendeshea chama.
 
Hivi ccm wana vyanzo gani vya mapato vya kujenga kumbi za mikutano, kugharamia mabango, kuendesha chama kwa anasa wakati watanzania wakifa kwa njaa
Karibuni nyote tujadili
Haiwezekani maviwanja hata hayaingizi mapato waseme ndo huko wanapata no, no
Wanapata fedha za kufuru hivyo?
Lumumba nataka jibu
Watanzania gani wamekufa kwa njaa?
 
viwanja vya mipira + open space (parkining) + majengo yao makubwa yalioko town wanakodisa.
Chadema vyanzo vyao utata bado cjajua .
 
Labda usishangae wanapata gawio la nyeti kutoka serikalini wao ndio chama wao ndio serikali. Kwani cabineti ya wizara ya fedha ina wapinzani, kule bandarini kwani kuna ukawa.
 
Nimekulia Arusha, acha nizungumzie hapa. Ofisi yake ya wilaya ni jengo la ghorofa moja lina wapangaji ambao ni ofisi za watu binafsi. Ofisi ya mkoa ni jengo la ghorofa tatu, hivyo hivyo lina wapangaji ambao ni ofisi za watu binafsi. Mtaa huo zilipo ofisi za mkoa kuna fremu nyingi sana za maduka na zinamilikiwa na CCM pia, nazo hizi zimekodishwa kwa wafanyabiashara.

Katika ofisi za kata panakuwa na angalau fremu moja au mbili ambazo zinakodishwa kwa wafanyabiashara.

Kwa Arusha wana majengo ambayo yanaonekana na ni dhahiri yanawaingizia kipato.
 
MISIBA MIKUBWA SASA HIVI IMEKUWA YA CCM. HUWEZ KWENDA LUCKY VICENT KUTOA RAMBI RAMBI BILA KUACHA HELA KWENYE MIKONO YA CCM. TUNAKOELEKEA WATAANZA KUTENGENEZA AJALI ILI WPATE HELA ZA KULISHA FAMILIA ZAO NA KUJENGA MIUNDO MBINU
tunakoelekea, mfano kwa bahati basi likadondoka likaua watu. Haraka haraka ccm wanajisomba wakapige hela. Rambi rambi zitatolewa lkn zinaishia kweny mifuko yao.
Siku hizi ccm imewekeza kweny misiba km Lucky vicent
 
ccm ni chama kikubwa sana na wameanza kuwekeza siku nyingi sana, wanamiradi mingi mno.
 
ccm ni chama kikubwa sana na wameanza kuwekeza siku nyingi sana, wanamiradi mingi mno.
Chadema mabilioni yote wanayopata kila mwezi hawana hata biashara ya genge la kuuza nyanya .chadema kuna mchwa wala ruzuku
 
Hebu mnaoichukia CCM muitishe mikutano mjiulize kama MNA akili sawasawa ikiwezekana mkapimwe akili zenu,mnamaansha hamjui mapato ya CCM yanakotoka??hamuon kuwa inawanachama wengi na karbia kila mkoa ina kiwanja cha mpira? Hakika nyie ni waseng..- (wasengenyaji)
 
Back
Top Bottom