lnspector CP
Member
- Apr 28, 2016
- 76
- 30
habar wanajukwaa,
Leo nimeona nitoe hofu yangu kwenu. Hofu yangu imekuja baada ya kuona kufifia katika kutafuta uwezekano wa upatikanaji wa mafao kwa mfanyakazi baada ya kuacha ama kuachishwa kazi. Hapo nyuma nilikuwa nashuhudia vijana wengi wakiacha kazi ili wawe wenye sifa ya kuchukua mafao yao na kwenda kutumia kwa mambo mbalimbli ikiwemo kuendelea na elimu za shule ama vyuo,leo hii hamna anayecha kazi kwa sababu hiyo.
Hatua ya kuacha kazi kwa vijana ili kwenda kukamilisha malengo yao ilikuwa ndo sababu tosha na makampuni nayo kuajiri vijana kila siku sasa imekuwa tofauti. Walio kazini wanang'ang'ania na kazi, walio mitaani wanakosa fursa ya kupata kazi.
Huko tuendako mabosi kazi wataanzisha biashara ya kufukuzisha watu kazini ili wawapekeke wakwao ama walio na maslahi nao.
Ombi kwa wahusika:
Achieni hizo pesa tukamilishie malengo yetu na tuwaachie wengine hii fursa ya kuajiriwa. Wengine mmetusahau hatuna posho wala mikopo, achieni pesa zetu tukafanyie biashara zetu.