Acheni uoga wa kipuuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Acheni uoga wa kipuuzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kaisa079, Oct 14, 2010.

 1. kaisa079

  kaisa079 Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Jana wakati nimekaa sina hili wala lile ikaingia sms katika kibofya changu toka katika namba '+3588108226' ikisema,'SLAA NI MROPOKAJI NA MGOMVI ANATUKANA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA.ANATAKA DAMU IMWAGIKE ILI MRADI AINGIE IKULU.TUMKATALIE KUIGEUZA NCHI YETU SOMALIA'. Baada ya kusoma sms hii nilighafilika sana.Kwa harakaharaka nilijua aliyeituma ni Mpumbavu,Muoga,hana uwezo wa kufikiri au ametoroka hospitali ya vichaa japo nachua chama anachotokea.Nilipojaribu kuipiga namba hii wala kuijibu sms nikashindwa.
  Ninazo sababu nyingi za kumuita mtuma sms mjinga,myoga au Mpunbavu na Punguani,Kwanza kabisa;
  KUMWITA SLAA MROPOKAJI NA MGOMVI
  Ni mropokaji huyuhuyu ndiye aliyeweza kufichua kashfa kibao za Ufisadi ambazo wabunge kibao 'Mabubu' Waliogopa Kuropoka. Matokea ya kuropoka kwake tukayaona,Akina Lowasa wakawajibika. Angalau tukaona kesi kadhaa Japo za 'Vimeo vya ufisadi'.Tunamtaka huyu huyu 'MROPOKAJI' awe Raisi wetu...awaseme watendaji wasiotimiza wajibu wao.Tunamtaka Huyuhuyu 'Mgomvi' ambaye akiwaambia watu wasiotimiza wajibu wao Ukweli anaonekana Mgomvi...Mimi huyuhuyu Mropokaji na Mgomvi ndiye RAIS WANGU!

  SLAA KUTUKANA VYOMBO VYA USALAMA
  Nani asiyeona vyombo vya Usalama vinavyoibeba CCM? Nani asiyeona Upendeleo wa Wazi ? Nani asiyeona Ulinzi anaopewa Salma Kikwete? Kwa Nini Mke Wa Lipumba na wake wa Wagombea wengine wa Urais hawapewi ulinzi ili wawapigie kampeni waume zao? Kwa hili Mtuma Message ni Punguani. Kwa hiyo alitaka Slaa avisifu vyombo vya Ulinzi kwa kuipendelea CCM? Nnachomwomba Slaa...Endelea Hivyo hivyo Rais wangu.Asiyewajibika na kutenda haki mpe 'DOZI' yake hapohapo

  ATI SLAA ANATAKA DAMU IMWAGIKE ILI AINGIE IKULU

  Kweli mtuma sms ni Mtumwa wa Kiakili ama hajasoma au nikichaa. Nani alikuambia Demokrasia ina vunja Amani. Hebu angalia Marekani enzi za Kampeni za Kina Obama.. Damu ilimwagika? Najua atasingizia Kenya au Zanzibar Miaka ya Nyuma pasipo kujua kuwa 'DAMU HUMWAGIKA HAKI IKIPINDISHWA NA KURA KUIBIWA!! Nani asiyejua kuwa Raila Odinga aliibiwa kura? Nani asiyejua kuwa Maalim Seif aliibiwa kura na Kudhulumiwa Urais.....Namtahadharisha mtuma sms kuwa iwapo Chama chake kitaiba Kura na Kumdhulumu Slaa haki ya kuwa Rais inawezekana kweli Damu Ikamwagika.. Sipendi Tufike Huko kwa kumwagika Damu.. Kimsingi nnachosema ni Kuwa HAKI Ikitendeka siku zote Hakuna damu inayomwagika. Labda sijamwelewa mtuma sms..Ana maana Slaa akiiingia Ikulu Damu Inamwagika? Ina maana Chama cha mtuma sms (CCM) Kimejiandaa kumwaga Damu Slaa akiingia Ikulu??? Kwani Nchi Hii ni ya CCM?
  Ndiyo maana nikamwita mtuma sms kuwa ni Punguani na Mtumwa wa Mawazo .Watu kama hawa ni Pazia la kukua kwa Demokrasia...Hawatakiwi nchi hii.

  ETI SLAA ATAGEUZA NCHI KUWA SOMALIA
  Kuna watu humu Duniani wanahitaji Kufanyiwa Neurological Surgery. Huyu Jamaa hajui hata Historia ya Somalia. Hajui Hata Historia ya Tanzania. Hajui kwa nini Tanzania haiwezi kuwa na machafuka kama Somalia. Naomba arudi Darasani akasome historia vizuri.

  HITIMISHO
  Ni vema tusianze kuwatisha watanzania kupitia Sms na badala yake tuwaeleze Sera za vyama vyetu na jinsi ya kuzitekeleza na siyo kutuma sms zenye kuwaponda wagombea, Kwa mfano mtuma sms alidhani ameikampenia CCM kumbe ndiyo ameipunguzia CCM Kura yangu.
  Watanzania Tuache Uoga na tuachane na Vitisho.
  Ni KAMA VILE WATU WANAVYOSEMA ELIMU BURE KWA WOTE HAIWEZEKANI?? Nakumbuka Profesa wangu alinifundisha kuwa 'FEAR OF FAILURE IS A FAILURE ITSELF'
  Watu wanaogopa na hawasomi SERA Vizuri..Tuanze Kubadilika mawazo na Kuamini kuwa kila kitu Kinawezekana. Mbona Tunaamini kuwa 'TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA? Wakati tunajua Ukimwi ni Chronic Infection na Kwamba ili tuwe na Tanzania Isiyo na Ukimwi ni Lazima Wagonjwa wote wa Ukimwi wauwawe?.. Lakini Bado Tunaamini tu Kuwa Tanzania Bila Ukimwi Inawezekana..Tena tunasimama na Kuimba Majukwaaani....Tanzania Bila UKIMWI Inawezekana!!!! Sasa kama Tanzania bila Ukimwi Inawezekana na tuna Mamililioni ya Wagonjwa wa Ukimwi na wengine maelfu wanaambukizwa kila siku na bado tunasema Bila Ukimwi inawezekana.. Je Kama Rasilimali zetu na Mafedha kibao yanayotumika Bungeni na Matumizi feki ya Serikali yakidhibitiwa hatuwezi Kuwa na ELIMU BURE KWA WOTE?
  Kila Mtanzania achambue Sera na aepuke Propaganda za Mapunguani
  wachache wanaotaka kuogopesha wengine
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwani bado wanaendelea kutuma hata baada ya kukemewa....
   
 3. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kwani hata hao wanaowakemea si wameshiriki kuandaa hizo sms?
   
Loading...