Acheni Siasa: Serikali yaiambia TUCTA

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
651
853
Imeripotiwa kwamba, serikali imewaambia TUCTA kuacha siasa.

Binafsi, sioni usiasa wa TUCTA kwa hili, ila naona usiasa kuitaja CHADEMA kuhusishwa kusambaza hicho ambacho leo hii tunaaminishwa sicho kilichosemwa na Mheshimiwa sana kuliko wote.

Ila na nyie TUCTA, mbona kuna mambo mengine mnajifanya hamuyaoni wakati mnayaona kupitia malalamiko ya watu (wafanyakazi)....Hivi suala la fao la kujitoa mmelisahau au ikoje? Mbona mnajifanya wema machoni petu wakati mnashindwa kupigania haki zetu? Nicolas Mgaya na TUCTA yake walilianzisha hili la fao la kujitoa hata kutishia kuiburuza serikali mahakamani, ila nyie mmekula bati tu, mnataka tuwaeleweje kuhusu hili.

Ni kwa nini TUCTA mnajifanya kutokuliona hili wakati kila siku mnasikia malalamiko ya watu kuumia mitaani kutokana na ugumu wa maisha na wakati pesa zao za mafao zimezuiwa na hii mifuko ya jamii for no apparent reason.
 
Tucta wote ni ccm, rejea katibu wa tucta taifa bwana msigwa ni kiongozi wa ccm iringa, so ccm ndo adui mkubwa kwa watanzania.
 
Back
Top Bottom