Msajili wa vyama vya Siasa aungana na CCM na Serikali kudai kuenguliwa kwao ni uzembe wao wafuate kanuni

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
NAIBU Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza
Na GRACE SHITUNDU -DAR ES SALAAM

NAIBU Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza amesema malalamiko yanayotolewa na vyama vya siasa kuhusu kuenguliwa wagombea wao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yamesababishwa na wao wenyewe.

Nyahoza alitoa kauli hiyo baada ya kutafutwa na MTANZANIA Jumapili lililotaka kufahamu kauli ya Ofisi ya Msajili kama mlezi wa vyama vya siasa nchini kuhusu malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya vyama vya upinzani, hususani Chadema na ACT Wazalendo, vikidai wagombea wao kuenguliwa kwa hujuma na hata kufikia hatua ya kujitoa kushiriki uchaguzi huo.

Miongoni mwa malalamiko ambayo yalitolewa na vyama hivyo, ni pamoja na wagombea wao kuenguliwa au kuwekewa pingamizi kwa sababu ya kukosa sifa kutokana na kukosea kujaza fomu zao.

Mengine ni wagombea kuenguliwa kwa sababu ya kujaza jina la chama kwa kifupi mfano, Chadema badala ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo au ACT Wazalendo badala ya Alliance for Change and Transparency.

Akizungumza na gazeti hili, Nyahoza alisema matatizo na malalamiko mengi yanayovikumba vyama vya upinzani katika uchaguzi huu, yanatokana na kutozingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

“Hivi vyama mara kwa mara tunaongea nao kuhusu kuzingatia sheria na kanuni, sasa kama watakuwa hawazisomi na kuzifuata watakuwa wanalalamika mara kwa mara,” alisema Nyahoza.

Kuhusu fomu inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya mgombea mmoja ambaye amekatwa baada ya kuandika kwa kifupi ACT Wazalendo na kuelezwa na msimamizi wa uchaguzi huo kwamba chama hicho hakipo kwenye orodha ya msajili, alisema chama hicho kimesajiliwa kwa jina la Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) na sio ACT Wazalendo, hivyo hilo ni kosa.

“Hiyo wanayosema ni kifupi ni kama ilivyo CCM kwa Chama Cha Mapinduzi, lakini huwezi kuandika CCM tu kwani inaweza ikawa inamaanisha kitu kingine.

“Sisi kama walezi siku zote tumekuwa tukiwasisitiza kuzisoma na kuzingatia sheria, lakini kama baba unasema na mtoto hafuati matokeo yake ndiyo hayo,” alisema Nyahoza.

Alisema kuwa vyama vyote vya siasa vina wanasheria na watu waliobobea kwenye mambo hayo, ambao wana uwezo wa kuwaongoza wanachama wao katika mambo hayo muhimu.

Wakati Naibu Msajili akisema hayo, siku moja baada ya Chadema kutangaza kujiondoa katika uchaguzi huo, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo alitoa kauli ya kushangazwa kwake na hatua hiyo iliyofanya na Chadema.

Aidha alikiri ni kweli kuna fomu zina makosa katika kujaza, lakini mchakato wa rufaa upo kwani kanuni haijamfunga mtu yeyote kudai haki ya kukata rufaa.
 
Huyu bwana anatoa maelezo ya kipumbavu anasema CCM,CUF,CHADEMA,ACT inaweza kuwa na maana tofauti.

Kwa muktadha wa siasa kifupi icho kinaeleweka maana yake huwez andika CCM,CHADEMA,ACT,CUF katika siasa ukatafsiri vingine kama anavyo taka kutuaminisha

Upumbavu tu kutaka kuhararisha ujinga
 
CCM walifundwa na msajili wa vyama?
Kama walipokea kanuni za uchaguzi huu mwèzi wa nne na wakapokea miongozo mwezi wa 7, kama walienda wakaziweka kwenye makabati hilo ni tatizo lao.
 
Sisiemu walifundwa na msajili wa vyama?
Kama walipokea kanuni za uchaguzi huu mwèzi wa nne na wakapokea miongozo mwezi wa 7, kama walienda wakaziweka kwenye makabati hilo ni tatizo lao.
Hilo mbona kama mnaliona kubwa na la watendaji kufunga ofisi za umma siku saba na kujificha mnaona ni dogo sana? Badibasketiboli π¥€¢
 
NAIBU Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza
Na GRACE SHITUNDU -DAR ES SALAAM

NAIBU Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza amesema malalamiko yanayotolewa na vyama vya siasa kuhusu kuenguliwa wagombea wao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yamesababishwa na wao wenyewe.

Nyahoza alitoa kauli hiyo baada ya kutafutwa na MTANZANIA Jumapili lililotaka kufahamu kauli ya Ofisi ya Msajili kama mlezi wa vyama vya siasa nchini kuhusu malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya vyama vya upinzani, hususani Chadema na ACT Wazalendo, vikidai wagombea wao kuenguliwa kwa hujuma na hata kufikia hatua ya kujitoa kushiriki uchaguzi huo.

Miongoni mwa malalamiko ambayo yalitolewa na vyama hivyo, ni pamoja na wagombea wao kuenguliwa au kuwekewa pingamizi kwa sababu ya kukosa sifa kutokana na kukosea kujaza fomu zao.

Mengine ni wagombea kuenguliwa kwa sababu ya kujaza jina la chama kwa kifupi mfano, Chadema badala ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo au ACT Wazalendo badala ya Alliance for Change and Transparency.

Akizungumza na gazeti hili, Nyahoza alisema matatizo na malalamiko mengi yanayovikumba vyama vya upinzani katika uchaguzi huu, yanatokana na kutozingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

“Hivi vyama mara kwa mara tunaongea nao kuhusu kuzingatia sheria na kanuni, sasa kama watakuwa hawazisomi na kuzifuata watakuwa wanalalamika mara kwa mara,” alisema Nyahoza.

Kuhusu fomu inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya mgombea mmoja ambaye amekatwa baada ya kuandika kwa kifupi ACT Wazalendo na kuelezwa na msimamizi wa uchaguzi huo kwamba chama hicho hakipo kwenye orodha ya msajili, alisema chama hicho kimesajiliwa kwa jina la Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) na sio ACT Wazalendo, hivyo hilo ni kosa.

“Hiyo wanayosema ni kifupi ni kama ilivyo CCM kwa Chama Cha Mapinduzi, lakini huwezi kuandika CCM tu kwani inaweza ikawa inamaanisha kitu kingine.

“Sisi kama walezi siku zote tumekuwa tukiwasisitiza kuzisoma na kuzingatia sheria, lakini kama baba unasema na mtoto hafuati matokeo yake ndiyo hayo,” alisema Nyahoza.

Alisema kuwa vyama vyote vya siasa vina wanasheria na watu waliobobea kwenye mambo hayo, ambao wana uwezo wa kuwaongoza wanachama wao katika mambo hayo muhimu.

Wakati Naibu Msajili akisema hayo, siku moja baada ya Chadema kutangaza kujiondoa katika uchaguzi huo, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo alitoa kauli ya kushangazwa kwake na hatua hiyo iliyofanya na Chadema.

Aidha alikiri ni kweli kuna fomu zina makosa katika kujaza, lakini mchakato wa rufaa upo kwani kanuni haijamfunga mtu yeyote kudai haki ya kukata rufaa.
Huyo ni mjinga mwingine. Amesikiliza tu ngonjera za polepole halafu amezibeba kama zilivyo. Tuna hasara kubwa, wajinga wanawaongoza wenye akili!

Kwa mtu makini kwanza angefanya utafiti na kujiuliza kama ni kweli wagombea wameondolewa kwa sababu za msingi, na zinazotajwa.

Wajinga wengi, kwa kadiri ya utafiti wa TWAWEZA, wamejaa CCM. Inakuwaje chama kilichojaa wajinga, wagombea wake wote wajaze fomu vizuri halafu walio na akili washindwe kujaza?

Na watendaji walifunga ofisi na kujificha wakati wa kutoa fomu na kurudisha, ni makosa ya vyama vya upinzani? Huyu mama nadhani ana uwendawazimu fulani.
 
Kuna "AUDIO" ambazo zilirekodiwa jinsi walivyokua wanapewa "MAAGIZO" hao watendaji (Si maagizo kikweli, ni amri). Sasa hawa wapuuzi wanavyo ongea ongea hivi waweke akiba ya maneno. Wataaibika.
tapatalk_1573287976466.jpeg
 
Kama ulisikiliza press ya polepole haina tofauti na haya aliyosema huyu jamaa. Kumbuka pale aliposema wametumia AKA badala ya jina kamili.
Hugo mfadhili gani wa kufuatilia chama kimoja tu? Mlishawahi sikia anamwandika barua mrema?
 
Hahah CCM mabingwa wa kujamba na kuwasha feni, nyoko kweli hawa! Wamejamba tangu juzi na Jafo wao Leo wanakuja kuwasha feni.....
 
Akizungumza na gazeti hili, Nyahoza alisema matatizo na malalamiko mengi yanayovikumba vyama vya upinzani katika uchaguzi huu, yanatokana na kutozingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

“Hivi vyama mara kwa mara tunaongea nao kuhusu kuzingatia sheria na kanuni, sasa kama watakuwa hawazisomi na kuzifuata watakuwa wanalalamika mara kwa mara,” alisema Nyahoza.
Inasikitisha kwa mtu mwenye nyadhifa kama hiyo badala ya kuchunguza ajue ukweli yeye mojamoja anawalaumu wapinzani. Yaani kichwani kwake haoni kama TAMISEMI wanaweza kuwa ndio wameleta tafrani. Yeye na Mutungi wana agenda tofauti na ile ya kusimamia vyama na kuhakikisha wote wanatendewa haki. Hawa ni wa kutoa au sivyo mwakani tutakuwa na majanga makubwa zaidi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom