Acheni kutoa siri zenu za unyumba,mnaharibu ndoa zenu

Wanawake hawajui kutunza kitu,ukiwa vizuri utawala sana shoga zake maana habari zinafikishwa kama zilivyo,ila ukiwa vibaya ujue mtaani unachorwa tu.Ukiona hujatongozwa na shoga wa mkeo basi habari Walizonazo kutoka Kwa mkeo sio nzuri..Chukua hiyo.
 
Kugongwa nje ya ndoa hili jambo linatawala mitandao kadhaa, ikiwemo JamiiForums. Dawa ya jambo hili kila mwanandoa atimize wajibu wake, pili kila wanandoa jengeni tabia ya kuongea matatizo yenu kwa upole kabisa, ongeeni kila kila kitu, msifichane na wala msiongopeane.

kusameheana pia ni muhimu sana, msitoe ruhusa ya kutoongea na kupeleka matatizo yenu kwa watu baki. Ndoa ni kitu kizuri mno, kitamu mno na kina faida kubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka kujua shida ipo wapi nenda madawati ya jinsia kwenye vituo vya polisi kaa na afande wa kike akuelezee shida wanazokutana nazo wakiwa wana solve migogoro inayoletwa.

Last time niligundua kuwa wanawake wetu wanauwezo mdogo sana wa kureason, ukikutana na mwanamke ambaye anauwezo wa kureason kwa logic then huwa ni zali sana.

Wengi wao huwa wana maamuzi ya kihisia yanayolenga kukomoa na kuonyesha hasira upande wa pili ili kujiridhisha wao (wanawake) na sio kusolve tatizo. Matokeo yake ni migogoro kizaliwa. Wanawake wakifunzwa namna nzuri ya kuwasiliana na wanaume na namna nzuri ya kuwasilisha changamoto zao kwa wanaume na mipaka ya namna nzuri ya kuishi na mwanaume then itapunguza migogoro kwa asilimia kubwa.
 
Back
Top Bottom