Uso wa nyoka
JF-Expert Member
- Mar 17, 2014
- 4,791
- 2,381
Ulichokisema ni sahihi na mimi ni shahidi. Ukiwa na pesa,hata kulia kwako si kama kwa asie nazo, ni rahisi kurecover. Mtu akikutibua,unajipa likizo ya siku 7 unaenda mbugani au nchi jirani kuzurura,ukirudi uko timamu maisha yanaenda. Au ukiona haifai kutumia pesa nyingi, kwa sisi wenye watoto,unawapeleka shopping ya nguvu watoto, kuona furaha yao tu usoni ni faraja tosha. Sasa umwagwe ukiwa huna hela, huna mipango ya kupata pesa halafu sharobaro, ndio wale tunaowasikia wakiingia kwenye kampeni ya kumtangaza mwanamke ubaya wake kwa kila mtu ili nafsi zao ziridhike kwa hiyo leverage. Nimegundua pia,kilio kikubwa na reaction anayokuwa nayo mtu baada ya kumwagwa,huwa ni indication ya namna alivyomthamini huyo mpenzi aliemwacha na kumtegemea kihisia. Kwa maneno mengine ni kuwa, mtu ambae alikuwa anaamini kuwa mpenzi wake ndie anaemkamilisha kwa kila kitu, siku akiachwa,huwa anajiona kama ukamilifu wake umekwisha na hata kama atajibaraguza kuwa hajaumizwa, matendo yake yataashiria hayo bila hata yeye kujua kuwa matendo yake yanaakisi namna ambavyo hajitoshi bila mpenzi aliemwacha. Hata kwa wanawake,utasikia wanatangazia ushoga ma ex wao au uathirika ili mradi tu wawachafue na wao wapate nafuu. Wengine watasingizia mimba ili wasiachwe. Lakini kwa mtu alie na msimamo na maisha yake, hutamwona akitetereka sana na kulialia ovyo na huwa ni wepesi wa kusamehe.
Tafuteni pesa, mapenzi yapo tu.
Tafuteni pesa, mapenzi yapo tu.