X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,344
- 14,120
Nasikitishwa na tabia ya vijana wengi ambao nawaona wakiwa na miili iliyodhohofika ukimuuliza eti kwa kuwa ametoswa na msichana aliempenda oh! Kamfumania mpenzi wake akiduu na mvulana mwingine, mapenzi yapo waliyakuta babu zetu na sisi tumeyakuta na tutayaacha.
Mbaya zaidi vijana wengi ndio waathirika wa kubwa wa tatizo hili la kulilia mapenzi,wanaacha kazi zao za maana,wanagombana na ndugu zao wanatengana na marafiki zao kisa mapenzi,msingi mkubwa wa kuyafurahia maisha ya mapenzi ni kufanya kazi kwa juhudi kujimudu kimaisha na kutokuyapa kipaumbele sana mapenzi,mimi naamini ukiwa na fedha utapata msichana yeyote unaye mpenda.
Ukiwa na pesa ata ukiamua kumiliki wasichana mamia kwa mamia na wote ukawaweka sehemu moja hakuna anayeweza kukupinga ukiyaendekeza sana mapenzi utajikuta unapoteza muelekeo wa maisha utaishi maisha mabovu mithiri ya teja alieathiriwa na madawa ya kulevya mbaya zaidi ata wazee wetu pia walilizwa sana na mapenzi lakini walisahau wakafanya mambo mengine wakaweza kutufikisha hapa tulipo.
Kitu cha msingi ili kuondoa uchungu ingia bafuni vua nguo zote lia hadi machozi yakauke najua utakua na uchungu sana sasa hakikisha unamaliza uchungu wote ulio nao kisha chukua maji oga jipe moyo anza maisha mapya,maisha ya kufanya kazi kwa bidii,maisha ya kuwa karibu na ndugu na marafiki maisha ya kuwasaidi wazazi maisha ya kuacha starehe zote.
Naamini matunda ya kufanya kazi kwa juhudi yatakupa familia bora na mke unae muhitaji utapata msichana mzuri ambae atakupenda, atakupenda sana utaiona dunia yote ni yako na hakuna anaeifurahia kama wewe.Sasa vijana tuamke tujifunze kupitia wenzetu wenye mafanikio ukifanikiwa kusahau maumivu ya mapenzi naamini mafanikio au ndoto zote ulizo nazo zitakuwa mbioni kutimia.
Anza kusoma vitabu tafuta marafiki wapya anza kufanya ibada mkumbuke Muumba wako na amini kuwa Mungu yupo na bila yeye usingefika hapo ulipo, omba msamaha kila ulie mkosea, fanya sana mazoezi,jifunze kutembelea sehemu ambazo hujawahi kutembelea kisha jipe muda mwingi wa kupumzika,achana kabisa na vilevi ukishindwa punguza,kisha iambie nafsi yako "sasa naamua kuwa mpya nayafuta yote yaliyopita nahitaji furaha, amani na mafanikio"
MUNGU AENDE AKAKUBARIKI WEWE UNAETESEKA NA KULILIA MAPENZI AMINI KILIO CHAKO KITAFIKA MWISHO utampata atakaejua na kuzithamini hisia zako utapata faraja ya moyo wako ila yote hayo yatatimia endapo utaanza upya sahau kila kilichopita, samehe kila aliekukosea na amini alikukosea ili akufikishe sehemu iliyo bora, akufikishe sehemu nzuri kimaisha na hakukukosea ili akudidimize.
...itaendelea...