Achaneni na mgogoro wa visiwani, acheni Zanzibar ijitenge

maramia

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2015
Posts
2,028
Reaction score
1,347
Naamini wengi wa wananchi, watanzania wa kawaida hatujui kwa dhahiri ni nini hasa kisa cha Tanganyika (Tanzania bara) kila wakati wa uchaguzi kuving'ang'ania visiwa vya Zanzibar na ni faida na manufaa gani hasa wananchi wa kawaida wa bara tunayopata kutokana na muungano huu?

Mgogoro wa visiwa hivi si wa leo, ni mgogoro ulioanza tangu enzi ya mwalimu. Katika awamu ya mwalimu tuliona Rais wa kwanza wa Zanzibar akipigwa risasi na kuuawa na kisha aliyemfuatia Sheikh Aboud Jumbe aking'olewa umakamo wa Rais na urais wa Zanzibar.

Mgogoro huo uliendelea kimya kimya ktk kipindi cha Rais Mwinyi na ktk awamu ya Mkapa watu wakauawa na kwa mara ya kwanza watanzania wenzetu wakawa wakimbizi huko Kenya, na sasa Rais Kikwete aliyeingia akaukuta mgogoro huo naye ameondoka ameuacha.

Najiuliza na nawauliza tu kwa upole wadau wenzangu wa JF na watanzania wenzangu swali moja kwamba, hivi tukiamua kuachana na hiyo faida tuipatayo kutoka muungano huo tukawaacha wazanzibar wawe huru nje ya muungano wawe majirani zetu wema,tutapata hasara gani kama taifa?
 
Ww watakutafuta kijana alafu Hizi siasa hizi ww unauhakika gani kama Karume aliuliwa na mambo ya muungano hebu tupe ushahidi
 
Umetimiza miaka mingapi leo siku ya MAGUFULI na SAMIA kuapihwa?
 
Ww watakutafuta kijana alafu Hizi siasa hizi ww unauhakika gani kama Karume aliuliwa na mambo ya muungano hebu tupe ushahidi

Wewe uko nchi gani? rejea mtazamamo wa SMZ mara baada ya mauaji yale, walioshukiwa kuwa nyuma ya mauaji yale walikuwa viongozi kutoka visiwani waliokuwa ktk JMT, mf Salim Ahmed Salim, Abdalahman Mohamed Babu, Kassim Hanga, Brigedia Mahfoudh, Kanali Seif Bakari n.k
 
Naamini wengi wa wananchi, watanzania wa kawaida hatujui kwa dhahiri ni nini hasa kisa cha Tanganyika (Tanzania bara) kila wakati wa uchaguzi kuving'ang'ania visiwa vya Zanzibar na ni faida hasa wananchi wa bara tunayoipata kutokana na muungano huo.

Mgogoro wa visiwa hivi si wa leo, ni mgogoro ulioanza tangu enzi ya mwalimu. Katika awamu ya mwalimu tuliona Rais wa kwanza wa Zanzibar akipigwa risasi na kuuawa na kisha aliyemfuatia Sheikh Aboud Jumbe aking'olewa umakamo wa Rais na urais wa Zanzibar.

Mgogoro huo uliendelea kimya kimya ktk kipindi cha Rais Mwinyi na ktk awamu ya Mkapa watu wakauawa na kwa mara ya kwanza watanzania wenzetu wakawa wakimbizi huko Kenya, na sasa Rais Kikwete aliyeingia akaukuta mgogoro huo naye ameondoka ameuacha.

Najiuliza na nawauliza wadau wenzangu wa JF na watanzania wenzangu swali moja kwamba, hivi tukiamua kuachana na hiyo faida tuipatayo kutoka muungano huo tukawaacha wazanzibar wawe huru nje ya muungano wawe majirani zetu wema,tutapata hasara gani kama taifa?

Hasara kwa sasa ipo kutokana na kuwa Ukawa ndiyo washindi wa Urais huko Zanzibar itawawia vigumu kutawala huko, lakini kama Muungano ungekufa kabla ya uchaguzi nina imani hakuna hasara ambayo ingekuwepo kutokana na hali harisi ulivyo sasa.
 
tukitengana na zanzibar tutapata hasara ya kugawana vyeo vya kisiasa.
 
Ujue Zanzibar ina watu million 1.5 tu na wengi hawaishi Zanzibar wapo nje ya Zanzibar ina maana waliopo kwa sasa ni kama million tu, wazanzibar wengi wamejenga Dsm na kwingineko hawataki kurudi Zanzibar kwani wanadai mzunguko wa pesa upo slow slow sana kupata pesa Zanzibar ni kazi ngumu labda uuze unga kwa watalii ndipo utapata pesa kwa kasi, lakini kinyume na hapo ni njaa kwa kwenda mbele ndiyo maana wengi wamehamia Tanga, Bagamoyo, pwani yote wamejaa, Serikali ya Zanzibar ni Serikali ya wajanja wengi wenye Akili nyingi sana kuliko Serikali ya Tanganyika, wao wametengeneza Utitiri wa watumishi wa umma, baraza lao wa wakilishi na mawaziri na wabunge kibao katika Ardhi ndogo kwa kutegemea pesa zinazotoka Hazina Dsm kuwalipa mishahara na kuendesha Serikali yao, ni visiwa vidogo lakini matumizi yao ni makubwa balaa na yamewekwa kuwa Siri kubwa maana Watanzania bara wakijua watakasirika sana, kutokana na pato kubwa la Taifa kupatikana Tanganyika lakini kwenye Mavuno Zanzibar wanakula sana wakati wao wapo million tu huku watanganyika wakiwa million 44 na ushei hivi. Zanzibar kwa kifupi ni wajanja wana kila kitu wana katiba Yao, Rais wao bendera zao, wimbo wao wa Taifa na sasa wanaandaa sarafu yao. Wao hawaogopi muungano kuvunjika kwani wanajua Oman watakuja kuwekeza pale hata America watakuja kuweka kituo cha kujeshi lakini kwa sasa Ukawa ndiyo washindi ni vyema wapewe Nchi yao Zanzibar ndipo wataamua cha kufanya wenyewe.
 
Wewe uko nchi gani? rejea mtazamamo wa SMZ mara baada ya mauaji yale, walioshukiwa kuwa nyuma ya mauaji yale walikuwa viongozi kutoka visiwani waliokuwa ktk JMT, mf Salim Ahmed Salim, Abdalahman Mohamed Babu, Kassim Hanga, Brigedia Mahfoudh, Kanali Seif Bakari n.k

kuongezea labda umesahau kuja mmoja jina lake halitajwi hujulikana Mr X ndio nani Mr X
 
Mola wangu! Mbona sababu zote hizi ni nyepesi? Minyoo anasema muungano ungekufa kabla ya uchaguzi, kusingekuwa na hasara, tpaulo naye eti tutapata hasara ya kugawana vyeo, kweli?
 
Ww watakutafuta kijana alafu Hizi siasa hizi ww unauhakika gani kama Karume aliuliwa na mambo ya muungano hebu tupe ushahidi

Ushahidi tokea lini ukawa na maana hapa Tanzania?
 
Mola wangu! Mbona sababu zote hizi ni nyepesi? Minyoo anasema muungano ungekufa kabla ya uchaguzi, kusingekuwa na hasara, tpaulo naye eti tutapata hasara ya kugawana vyeo, kweli?

Mie nahisi ccm wana Ajenda yao pengine wanataka kuua muungano kijanja ili wasipate hasara wasingizie kuwa Ukawa ndiyo wamevunja muungano.
 
Kuna kisingizio kinatengenezwa sasa ili kiletwe kwa wananchi kisha wabebeshwe zigo ukawa waonekane wanataka kuvunja muungano. Ukawa wanapaswa waongeze speed ya kudai Ushindi wa maalim Seif wakilemaa nina hakika itakula kwao.
 
Maramia nadhani leo umetoa wazo zuri sana.
Ebu tuwaachie wazanzibari nchi yao wajiendeshe wenyewe tuone kama watauana, ama watakufa kwa njaa potelea mbali who cares? Ni bora tukawaachia nchi yao wenyewe kuliko kujenga hizo consipiarcy theories. Huku kuendelea kuwang'ang'ania wazanzibari kwa kweli hatuwatendei haki hata kidogo. Hivi muungano huu unafaida gani kwani???
 
Sijawahi kuona faida ya muungano. Nimeishi huko zaidi ya miaka 3. Bado sijaona faida yake.
 
Naamini wengi wa wananchi, watanzania wa kawaida hatujui kwa dhahiri ni nini hasa kisa cha Tanganyika (Tanzania bara) kila wakati wa uchaguzi kuving'ang'ania visiwa vya Zanzibar na ni faida gani hasa wananchi wa kawaida wa bara tunayoipata kutokana na muungano huu?

Mgogoro wa visiwa hivi si wa leo, ni mgogoro ulioanza tangu enzi ya mwalimu. Katika awamu ya mwalimu tuliona Rais wa kwanza wa Zanzibar akipigwa risasi na kuuawa na kisha aliyemfuatia Sheikh Aboud Jumbe aking'olewa umakamo wa Rais na urais wa Zanzibar.

Mgogoro huo uliendelea kimya kimya ktk kipindi cha Rais Mwinyi na ktk awamu ya Mkapa watu wakauawa na kwa mara ya kwanza watanzania wenzetu wakawa wakimbizi huko Kenya, na sasa Rais Kikwete aliyeingia akaukuta mgogoro huo naye ameondoka ameuacha.

Najiuliza na nawauliza tu kwa upole wadau wenzangu wa JF na watanzania wenzangu swali moja kwamba, hivi tukiamua kuachana na hiyo faida tuipatayo kutoka muungano huo tukawaacha wazanzibar wawe huru nje ya muungano wawe majirani zetu wema,tutapata hasara gani kama taifa?

Last edited by a moderator:
Ww watakutafuta kijana alafu Hizi siasa hizi ww unauhakika gani kama Karume aliuliwa na mambo ya muungano hebu tupe ushahidi
Zanzibar ni yetu! Mkristo ukija wakati wa ramadhani utafuata sheria za mfungo wa saumu!
 
Wewe uko nchi gani? rejea mtazamamo wa SMZ mara baada ya mauaji yale, walioshukiwa kuwa nyuma ya mauaji yale walikuwa viongozi kutoka visiwani waliokuwa ktk JMT, mf Salim Ahmed Salim, Abdalahman Mohamed Babu, Kassim Hanga, Brigedia Mahfoudh, Kanali Seif Bakari n.k

ikiwa hamjuwi historia msitake kupotosha waloshtakiwa kumuuwa karume ni comrade umma party aliyemuuwa karume ni lutein humud Mohamed kulipa kisasi cha babake aliyeuliwa jela kwa sababu alikuwa hizbu. kassim hanga kauliwa jela kabla ya karume kuuliwa around 1970. ali mahfoudh abdulrahman babu, salim ahmed salm wote comrade walifungwa daressalam isipokuwa salim ahmed salim alikuwa ubalozini .seif bakari hayumo kabisa
 
Hasara kwa sasa ipo kutokana na kuwa Ukawa ndiyo washindi wa Urais huko Zanzibar itawawia vigumu kutawala huko, lakini kama Muungano ungekufa kabla ya uchaguzi nina imani hakuna hasara ambayo ingekuwepo kutokana na hali harisi ulivyo sasa.

= halisi
 
Back
Top Bottom