MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 19,288
- 39,974
“He Killed My Ma, He Killed My Pa… I'll Vote for Him”
Hiyo ilikuwa slogan ya wafuasi wa dikteta Charles Taylor wa Liberia mwaka 1997 kwenye uchaguzi mkuu baada ya kuisha kwa vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1996. Vijana walijitoa ufahamu na kudai hata kama Taylor aliwaua baba na mama zao watampigia kura. Na kweli Taylor alishinda kwa 75%. Mara baada ya kuwa Rais, ukatili wa Charles Taylor ukaongezeka mara dufu. Vijana waliompigia kura waliuwawa kama kuku. Baada ya muda mfupi Liberia ikaingia kwenye vita vya pili vya wenyewe kwa wenyewe.Hawa vijana wa Liberia hawana tofauti na hawa vijana wa CHADEMA wanaodai hata kama michango yao inatafunwa na viongozi wao watachanga tena. Ni vijana wa hovyo walioamua kujitoa akili. Nyie wafuasi wa CHADEMA hamuoni kuwa viongozi wenu wakipata madaraka nchini watakuwa wapigaji wasio na mfano? Kama pesa zenu kidogo wanazitafuna bila aibu wala woga vipi wakikabidhiwa hazina?
Ninawasihi vijana wa vyama vyote kutokuwa kama kondoo kukubali mambo ya hovyo kisa yamefanywa na kiongozi wa chama chako. Tumia akili ulizopewa na Mungu.