Acha niitwe mchochezi: Uchumi wa Tanzania ulijengwa na Mkapa, Kikwete akatuuza hivi na Magufuli naye Mhh

watanzania bahna tunataka shilongi ya miaka 30 ilio pita iwe shiling ya leo huu ni uongo mkubwaa zama zina badilika,na ukitzama thamani hio hio ya mkate kununuliwa kwa shilling 5 miaka 25 ilio pita ni sawa sawa na 1000 shilling ya leo kulingana na zama zinavo badilika kupitia teknolijia,

Ila sisi hutaka miaka nenda miaka rudi kila jambo liwe pale pale,ukitaka kumchafua mwafrika basi ukimpa hoja uanze na nambari za asilimia hata kama ninza uongo basi atakuona wa maaana pasi na kufikiria, hapa tumeletewa takwim lakn its just a number and figure, shiling haiwezi kukaaa miaka yote kwa thamani ile ile tu hata inch za magharibi uchumi uliko nawiri hali ndo iyo iyo.
 
Data zako za uwongo.
Kwanza aliekua hakopesheki ni Nyerere. Wazungu walimgomea naye akagoma kufata masharti. Nchi ikamshinda akaja Mwinyi.
Mwinyi alikuta mbali ya madeni makubwa pia alikuta n hi imejaa ufukara.
N hi haina chakula , ukulima wa ujima umefeli vibaya mno.
Viwanda vyote vimekufa...
Mabenki nayo yame filisika secta ninafsi hakuna
Hakuna hata bars bara moja ambayo ina lami na inapitika zote ni mashimo matupu.
Kutoka tanga mpaka Dar ilikua ni masaa 13 .
Jiji la Dar lote lilikua mahandaki matupu.
Barabara kuu ya samora , Ali hassana mwinyi pugu kilwa za kariakoo na city centre zote zilikua mashimo matupu na mahandaki.
Mwinyi alikua na sababu za kukopa.
Kwanza aliubadili mfumo wa uchumi kutoka ujima na kuwa uchumi huria ambao mpaka sasa ndio tunao ufata.
Hivyo aliachia wafanya biashara kufanya biashara na kuanzisha viwanda.
Akakopa kuanza kujenga barabara za mijini na mikoani.
Nyingi zili jengwa wakati wake sasa tunapanua tu.
Alikopa ili kutoa pembejeo kwa wakulima na hatukua na shida ya njaa tena...wakulima walizalisha chakula ch kutosha .
Pesa alokopa Mwinyi zipo justified kwani zilitumika kufufua uchumi ulokufa na kujenga miundo mbinu ilio kufa kabisa...

Mkapa alipo ingia alisha rahisishiwa kazi...akaninafsisha makampuni yote yanayo tia hasara na akaanzisha mfumo mzuri zaidi wa kodi...Alikopa sana na alifuja sana.
Mfano ununuzi wa ndege ya rais ni ufujaji na kununua rada kwa frdha nyingi za wizi ni ugujaji.
Lakini usimamizi wake wz uchumi ulisaidia kukubaliwa kufutwa kwa baadhi ya madeni na wadeni wetu . Ufutaji huu madeni nao ukazalisha scandal ya EPA.

Kwa ufupi Nyerere alikua kwenye try and error ..alipata urais akiwa kijana asie na ujuzi wa kuendesha nchi. Miaka 7 ya kwanza alikua ni capitalist hakubadiki mfumo wa uchumi nchi ilikua ikienda vizuri...1967 alipatwa na majini ya kisoshalisti akabadilili mfumo wa uchumi ambao ulikua ni mgeni na wa majaribio ...hatimae wajamaa wakaanguka dunia nzima akiwemo nyererena uchumi wake.
Mwinyi alifanya kazi kubwa ya ku turn the country upside down ikaelekea mahali pazuri ila walofata wamefeli

Mbona hujaongelea ya kikwete
 
Mkapa ??

Sera ya ubinafsishaji uchwara mashirika ya umma kwa bei chee

Kuingia mikataba ya madini kwa 3% ndio imeongeza pesa. Mikataba ya hovyo ndio ilikuza kdg ,bora tungekuwa na uchumi mbovu kuliko kusaini mikataba ya hovyo ya kinyonyaji

Kuuza nyumba za serikali ,pesa za wizi wizi tu

Mwinyi angeamua angechimba madini na kuwaleta acacia na kuuza banks ila good thing hakufanya hivyo

Mkapa ni worse than mwinyi ,income nyingi alipata kupitia wizi mikataba ya ki Mang'ungo,

Magufuli is the man only na atakuwa successful
 
Pamoja na hayo mazuri aliyoyafanya Mkapa, lakini mikataba ya aibu ktk sekta ya madini kwangu inamuondolea huo ushujaa!!! 3% kwa miaka 100 ?! Ahh HAPANA
Income yote hio aliipata through mikataba ya ki mangungo 3% sisi 97% acacia

Sera uchwara ya ubinafsishwaji kuuza NBC kwa bei chee na mashirika mengine

Mkapa ndio worse kuliko mwinyi ,mwinyi angeamua angechimba migodi na kupata pesa nyingi ila Mkapa pesa nyingi alipata baada ya Sera uchwara na mikataba ya hovyo ambayo inalalamikiwa mpaka Leo

Kuuza nyumba za serikali yaani pesa za wizi wizi

Bora asinge raise pesa kuliko kusaini mikataba ya kinyonyaji

Magu ndio pekee anaonyesha njia
 
Mleta mada haujui unachokisema wewe!
  • Bila Mzee Ruksa kukufungulia uchumi ungekuwa unavaa kaniki saa hizi
  • Hali ya nchi mwaka 1985 wakati Mwinyi anachukua nchi, uchumi ilikuwa unakua kwa Negative, yaani nchi ilikuwa hohehahe vibaya mno
  • Mwinyi kaingia madarakani nchi haina reserve ya mafuta hata ya mwezi mmoja
  • Alichokifanya Mwinyi ni kuwajengea uwezo watanzania angalau waanze ujasiriamali, akaamua kutowatoza kodi makusudi ili wajijengee base ya uchumi
  • Mwinyi kaondoka madarakani akiwa ametuachia Demokrasia, nchi imefunguka, vijana wana mitaji ya kwenda hata ng'ambo kama vile Dubai kuleta mzigo.

Mkapa
  • Aliimarisha ukusanyaji wa kodi, Mkapa kaondoka madarakani serikali ikikusanya Shilingi bilioni 166 kwa Mwezi
  • Alizisaidia sana taasisi za serikali kuwa na hadhi.
  • Aliucontrol vizuri mfumuko wa bei
  • Aliuza nyumba na mashirika ya serikali kwa bei ya chee
  • Aliuza madini kwa mikataba tunayohangaika nayo leo
  • Ishu nyingi zilizolalamikiwa bungeni kuhusu ufisadi za EPA, Kagoda, Ndege ya Raisi, Meremeta zilitokea wakati wake.
  • Aliuza benki ya NBC kwa bei ya kutupa
KIKWETE

  • Aliweka lami mtandao mkubwa sana wa barabara nchi nzima
  • Aliingiza kwenye gridi ya Taifa Kiwango kikubwa cha umeme kuliko umeme uliowahi kuwepo chini ya awamu zilizomtangulia combined
  • Alipandisha makusanyo ya mwezi ya serikali kutoka bilioni 166 mwala 2005 hadi bilioni 900 mwaka 2015, hii ikiwa ni ongezeko la 500%
  • Alijenga na kudahili wanafunzi katika vyuo vikuu vingi ikiwemo UDOM, Nelson Mandela, Chuo cha Kilimo cha JKN
  • Uchumi ulikuwa unakua kwa wastani wa asilimia 7 wakati wake, na mwaka 2014 katika quarter moja ya mwaka huo uchumi umewahi kukua kwa asilimia 8.6 ikiwa ni kiwango kikubwa kabisa kuwahi kutokea ktk historia ta Tanzania
  • Alifanya vizuri sana kidiplomasia na Demokrasia ilikua, kushamiri na uhuru wa maoni uliheshimiwa.
  • Hakupambana vya kutosha dhidi ya ufisadi, ni kipindi chake hata Twiga wetu walipandishwa ndege kutoroshwa nje!
  • Pia Hakusimamia vizuri public spending, watu walikuwa wanasafiri sana nje ya nchi na kuigharimu nchi sana.
JPM
  • Anafanya vizuri kupambana na Ufisadi
  • Anafanya vizuri kubana matumizi yasiyo na tija serikalini
  • Anafanya vizuri kuhakikisha nidhamu ya watumishi wa serikali
  • Anajenga Reli ya kisasa ya Standard Gauge hii ni kitu kizuri sana
  • Anafufua mradi wa kufua umeme wa Stieglers gorge hii pia itasaidia sana kwenye masuala ya umeme nchini
  • Anachopaswa kufanya, serikali ihakikishe kuna mzunguuko wa pesa za kutosha kiasi cha watu wakifanya kazi wapate pesa
  • Alinde aimarishe na aitetee Demokrasia kwa sababu ni demokrasia pekee itakayolinda mafanikio ya kiuchumi tutakayoyavuna, na ni demokrasia pekee itakayowapa tumaini watu pindi hali ngumu ya kiuchumi ikiwafika, yaani watu wataamini kuwa wana power ya kuwabadili ma CEO wa kuendesha nchi yao kupitia ushawishi wa kisiasa na sanduku la kura. Hope is a good thing.
  • Aachane na miradi ambayo kwa maoni yangu haina input kubwa ya kiuchumi kama vile uwanja wa ndege Chato, au move kama ile ya kuhamia Dodoma, binafsi sioni kama miradi hiyo ni muhimu sana katika ile equation ya " Kupanga ni kuchagua"
  • Atupe katiba bora ya wananchi na hili ndo kubwa sana litakalodefine legacy yake kuliko hata ujenzi wa flyovers!
 
Mkapa huyu huyu si ndie alieuza kila kitu....?

Unategemea angekosa ela kweli....?
Ni kama vile mtu auze Noah laki 2 ,flat inch 42 laki moja ,boxer laki 2

Pesa atakuwa nazo nyingi ila bora angekuwa na nothing kuliko kuuza huko na kupata pesa hzo ,
 
  • Thanks
Reactions: Oxx
Ukweli ni kwamba kikwete ametuaribia nchi na kina Nyalandu wake, kutwa marekani kupiga picha na chrisbrown, nani mshamba kati yake na Magufuli??

Maana ukikua una desire kununua sub woofer na hauna hela siku ukinunua utawasumbua wapangaji na loud music, na hapo ndo ushamba uonekana
Aisee we unaoneka una chuki binafsi na Kikwete au waislam, maana pamoja na yote uliyosema eti mikopo ya kikwete hakuna ilichofanya, hivi nani kaunganisha mikoa yote kwa rami, nani kasambaza umeme mpaka vijijini, nani kajenga mradi wa maji kutoka Victoria, nani kajenga chuo kikuu cha dodoma, nani kasomesha wanafunzi wengi elimu ya juu. tuache roho mbaya na udini tuwe wakweli udhaifu wa kikwete ufisadi ila kwa maendeleo hakuna kama yeye.
na kingine hakuna raisi aliejenga demokrasia kama yeye. Acha udini wewe
 
Mleta mada haujui unachokisema wewe!
  • Bila Mzee Ruksa kukufungulia uchumi ungekuwa unavaa kaniki saa hizi
  • Hali ya nchi mwaka 1985 wakati Mwinyi anachukua nchi, uchumi ilikuwa unakua kwa Negative, yaani nchi ilikuwa hohehahe vibaya mno
  • Mwinyi kaingia madarakani nchi haina reserve ya mafuta hata ya mwezi mmoja
  • Alichokifanya Mwinyi ni kuwajengea uwezo watanzania angalau waanze ujasiriamali, akaamua kutowatoza kodi makusudi ili wajijengee base ya uchumi
  • Mwinyi kaondoka madarakani akiwa ametuachia Demokrasia, nchi imefunguka, vijana wana mitaji ya kwenda hata ng'ambo kama vile Dubai kuleta mzigo.

Mkapa
  • Aliimarisha ukusanyaji wa kodi, Mkapa kaondoka madarakani serikali ikikusanya Shilingi bilioni 166 kwa Mwezi
  • Alizisaidia sana taasisi za serikali kuwa na hadhi.
  • Aliucontrol vizuri mfumuko wa bei
  • Aliuza nyumba na mashirika ya serikali kwa bei ya chee
  • Aliuza madini kwa mikataba tunayohangaika nayo leo
  • Ishu nyingi zilizolalamikiwa bungeni kuhusu ufisadi za EPA, Kagoda, Ndege ya Raisi, Meremeta zilitokea wakati wake.
  • Aliuza benki ya NBC kwa bei ya kutupa
KIKWETE

  • Aliweka lami mtandao mkubwa sana wa barabara nchi nzima
  • Aliingiza kwenye gridi ya Taifa Kiwango kikubwa cha umeme kuliko umeme uliowahi kuwepo chini ya awamu zilizomtangulia combined
  • Alipandisha makusanyo ya mwezi ya serikali kutoka bilioni 166 mwala 2005 hadi bilioni 900 mwaka 2015, hii ikiwa ni ongezeko la 500%
  • Alijenga na kudahili wanafunzi katika vyuo vikuu vingi ikiwemo UDOM, Nelson Mandela, Chuo cha Kilimo cha JKN
  • Uchumi ulikuwa unakua kwa wastani wa asilimia 7 wakati wake, na mwaka 2014 katika quarter moja ya mwaka huo uchumi umewahi kukua kwa asilimia 8.6 ikiwa ni kiwango kikubwa kabisa kuwahi kutokea ktk historia ta Tanzania
  • Alifanya vizuri sana kidiplomasia na Demokrasia ilikua, kushamiri na uhuru wa maoni uliheshimiwa.
  • Hakupambana vya kutosha dhidi ya ufisadi, ni kipindi chake hata Twiga wetu walipandishwa ndege kutoroshwa nje!
  • Pia Hakusimamia vizuri public spending, watu walikuwa wanasafiri sana nje ya nchi na kuigharimu nchi sana.
JPM
  • Anafanya vizuri kupambana na Ufisadi
  • Anafanya vizuri kubana matumizi yasiyo na tija serikalini
  • Anafanya vizuri kuhakikisha nidhamu ya watumishi wa serikali
  • Anajenga Reli ya kisasa ya Standard Gauge hii ni kitu kizuri sana
  • Anafufua mradi wa kufua umeme wa Stieglers gorge hii pia itasaidia sana kwenye masuala ya umeme nchini
  • Anachopaswa kufanya, serikali ihakikishe kuna mzunguuko wa pesa za kutosha kiasi cha watu wakifanya kazi wapate pesa
  • Alinde aimarishe na aitetee Demokrasia kwa sababu ni demokrasia pekee itakayolinda mafanikio ya kiuchumi tutakayoyavuna, na ni demokrasia pekee itakayowapa tumaini watu pindi hali ngumu ya kiuchumi ikiwafika, yaani watu wataamini kuwa wana power ya kuwabadili ma CEO wa kuendesha nchi yao kupitia ushawishi wa kisiasa na sanduku la kura. Hope is a good thing.
  • Aachane na miradi ambayo kwa maoni yangu haina input kubwa ya kiuchumi kama vile uwanja wa ndege Chato, au move kama ile ya kuhamia Dodoma, binafsi sioni kama miradi hiyo ni muhimu sana katika ile equation ya " Kupanga ni kuchagua"
  • Atupe katiba bora ya wananchi na hili ndo kubwa sana litakalodefine legacy yake kuliko hata ujenzi wa flyovers!

nafurahishwaga sana na koment za hiv zisizokua na ushabiki shabiki, umeongea fact kabisa.

kunywa soda hapo kwa sanga nakuja kulipia........
 
kwa takwimu hizi za uongo wanazotoa na kukopa kwa siri tena mikopo yenye riba kubwa eti mnamsifia analipa madeni akili zakushikiwa
 
Deni la Taifa kwa sasa ni trillion 41 ambako uchunguzi unaonesha kwamba kila awamu ina mchango katika deni la Taifa , lakini awamu ya kikwete ilitia fora

1.Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 3 trillions
Huyu mzee deni lake limekuja mwaka 1979 wakati wa vita lakin kipindi cha nyuma alikuwa na.clean sheet
Nitaanzia kumchambua Mwinyi Mkapa na Kikwete, Maana ubovu wa mwinyi alirekebisha Mkapa , Kikwete akaturudisha kwa Mwinyi

2.Ali Hassan Mwinyi 18 trillions

Inamaana mwinyi amekopa Trillions 15

3.Mkapa huyu mr clean alipokuja alifuatiliwa na sana na mwalimu nyerere na kumpa maelekezo kurekebisha ya mwinyi kupitia aliyofanya Mkapa utagundua yapi yalikuwa madhaifu ya Mwinyi

Mkapa alipokuja akalipa na kushusha deni la Taifa mpaka 10 trillions,

Mkapa amepokea nchi mwaka 1995, huku ukuaji wa uchumi ukiwa asilimia 4.2. Alipoondoka madarakani uchumi ulikuwa asilimia 6.7

mwaka 1995 mfumko wa bei ulikuwa asilimia 21 lakini mwaka 2005 kipindi chote cha Mkapa mfumko huo ulishuka mpaka asilimia 4.

Mkapa alipokea serikali riba ya benki ikiwa asilimia 30 hadi 26 mwaka 1995. Mwaka 2005 riba ya benki ilishuka hadi asilimia 14.

Mkapa kapewa nchi ikiwa haikopesheki mwaka 1995. Mwaka 2005 deni la taifa lilikuwa Sh 10 trioni. Leo miaka 10 katika utawala wa Rais Kikwete, deni lilifika Sh. 35 trioni. Ziada ya Sh. 25 trioni na kilichofanywa na deni hakionekani

wakati Mkapa anaingia madarakani mwaka 1995, akiba ya fedha za kigeni zilikuwa za miezi miwili; hadi mwaka 2005, akiba hiyo ilifikia ya miezi nane.

4.Jakaya kikwete amekopa mpaka 35 trillions inamaana trillions 25 amekopa kikwete

chini ya utawala wa Kikwete, riba ya benki imepanda hadi asilimia 18.

ukilinganisha na Mkapa alipewa nchi ikiwa haikopesheki mwaka 1995. Mwaka 2005 deni la taifa lilikuwa Sh 10 trioni. Lakin miaka 10 katika utawala wa Rais Kikwete, deni lilifika Sh. 35 trioni. Ziada ya Sh. 25 trioni

Mkapa aliacha nchi ikiwa inakusanya mapato ya ndani zaidi ya asilimia 14 ya pato la taifa mwaka 2005. Kwa kwa kikwete, kodi iliyokusanywa ni asilimia 12 ya pato la taifa.

KWA UPANDE WA MAGUFULI
5. Mpaka sasa Magufuli kakopa trillions 6, kwa miaka 2 aliyoingia

Bongonewz Magazine: MMH!! SERIKALI YA KIKWETE YAONGOZA KWA KUKOPA: DENI LA TAIFA LAFIKIA TRILIONI 21

RICHARD KAMNDE: DENI LA TAIFA LAFIKIA TRILION 40 IMF YAIONYA SERIKALI

Deni la taifa Tz laongezeka hadi trilioni 40

Kafulila: JK kavunja uchumi aliouweka Mkapa

Angalia kuporomoka kwa shillingi tokea tumepata Uhuru
Umenikumbusha netgroup solution, Anben, Kiwira coal mine, EPA!
Duh! Yaani unadiriki kumsifia kajenga uchumi!
Ni heri ungesema alitengeneza njia ya wezi kupita (mikataba)
 
Umenikumbusha netgroup solution, Anben, Kiwira coal mine, EPA!
Duh! Yaani unadiriki kumsifia kajenga uchumi!
Ni heri ungesema alitengeneza njia ya wezi kupita (mikataba)

hixo kampuni zote ukichunguza utakuta alifanya miaka ya mwisho ofisini. sijuhi ilikuaje aka kengeuka mwishomwisho cha ajabu ajawahi kutuomba msamaha kwa matendo yake.
 
Back
Top Bottom