Acha kuzubaa, watu wanapiga tu fedha kila mwaka

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
WATU wanapambana kila siku kuhakikisha wanatoka kimaisha. Wale wasiokuwa na kitu wanajitahidi kufanya liwezekanalo ilimradi tu mwisho wa siku wafanikiwe. Waitwe wafanyabiashara wakubwa, mabilionea na majina mengine mengi ambayo yatawatafsiri kama watu matajiri.
Wakati wewe unalala usiku au mchana, kuna mtu amekaa mahali fulani anatafakari ni kwa jinsi gani anaweza kutengeneza fedha.
Wakati wewe ukila bata kwa kutumia fedha kibao zaidi ya unazoingiza kwa wiki, kuna jamaa mahali fulani anafikiria ni kwa jinsi gani akaunti yake iendelee kuingiza kiasi kikubwa cha fedha.
Wakati wanamuziki wa Bongo wanategemea muziki tu kuingiza fedha, wasanii wengi wa Marekani na Ulaya wanaanzisha biashara za kuwapa fedha nje ya muziki ili wawe matajiri wakubwa.

Wakati wasanii wa Marekani wakikosa usingizi kusaka utajiri, baadhi ya wale wa Bongo wameridhika, gari na nyumba vinatosha! Mwishoni mwa wiki iliyopita walitangazwa wasanii wenye mkwanja mrefu duniani.
Ni listi ya watu ambao hawategemei muziki tu bali wanapiga dili zao nyingine nyingi kutengeneza fedha ndiyo maana leo hii wamekuwa hapo walipo. Wafuatao ni baadhi ya wasanii wanaoongoza kwa kutengeneza fedha nyingi kwa mwaka huu.


P DIDDY
P-Diddy.jpeg
Anaitwa Sean Combs Almaarufu P Diddy. Ni mwanamuziki namba moja katika listi yetu hii ya wanamuziki wanaoongoza kwa kuwa na mkwanja mrefu. Mwaka jana P Diddy alikuwa na utajiri wa dola milioni 750 (zaidi ya Sh. Trilioni 1.6) ila kwa sasa mkwanja umeongezeka na kufi kia dola milioni 820 (zaidi ya Sh. Trilioni 1.9).
Si muziki tu ambao unamuingizia jamaa mkwanja bali ana mishemishe nyingine kabisa. Kumbuka jamaa ana nguo zenye nembo ya Sean John. Kumbuka jamaa ana pombe iitwayo Ciroc. Jamaa huyuhuyu ana televisheni iitwayo Revolt na vitu vingine vingi. Hata asipoimba mwaka mzima, bado fedha zitakuwa zinaingia tu.

JAY Z
jay-z-2.jpg
Kuna mengi ya kumuelezea ila kwa kifupi jamaa anaitwa Shawn Corey Carter lakini anajulikana zaidi kama Jay Z.
Mwaka jana alikuwa na utajiri wa dola milioni 610 (zaidi ya Sh. Trilioni 1.2) huku akishika nafasi ya tatu ila kwa mwaka huu utajiri wake umeongezeka na kuwa dola milioni 810 (zaidi ya Sh. Trilioni 1.6) huku akishika nafasi ya pili. Huyu jamaa hategemei muziki tu kutengeneza fedha. Anafanya ishu nyingine kibao.
Anamiliki Lebo ya Roc Nation, anauza nyimbo mtandaoni kwa kutumia Mtandao wa Tidal ambao una wasanii wengi akiwemo Kanye West, jamaa ana shampeni yake iitwayo Armand de Brignac ambayo chupa yake moja inauzwa kwa dola 850 (zaidi ya Sh. milioni 1.6).
Ila kubwa kuliko zote ni kwamba jamaa ana hisa katika Kampuni ya Uber ambayo inahusika na usafi rishaji nchini Marekani. Inasemekana kuwa, kampuni hiyo ndiyo imemuingizia zaidi fedha hadi kufika alipo.


DRE
eminem-and-dr-dre.jpg
Ingawa jamaa ameshuka, lakini utajiri wake umeongezeka kulinganisha na mwaka jana. Kwa sasa ana utajiri wa dola milioni 740 (zaidi ya Sh. trilioni 1.4), wakati mwaka jana alikuwa na utajiri wa dola milioni 710 (zaidi ya Sh. Trilioni 1.2).
Kinachomuingizia fedha nyingi ni lebo zake alizokuwa nazo, anazo sita zikiwemo Death Row, Aftermath Entertainment, Interscope Record na nyinginezo. Ila mbali na hilo, kitu kilichomfanya kupata fedha zaidi ambazo mpaka sasa zinambeba ni zile alizouza headphone zake za Beat kwa Apple kwa dola bilioni 3 (zaidi ya Sh. Trilioni 6) mwaka 2014.


BIRDMAN
toni-braxton-birdman-42279bc0-71bc-425c-bc95-fbcbe50af323.jpg
Kwa jina anaitwa Bryan Williams ila ni maarufu kama Birdman. Utajiri wake umebaki palepale, mwaka jana (2016) alikuwa na utajiri wa dola milioni 110 (zaidi ya Sh. bilioni 220) sawa na mwaka huu japokuwa mwaka juzi alikuwa na utajiri wa dola milioni 140 (zaidi ya Sh. bilioni 280). Amebaki nafasi ya nne kama alivyokuwa. Utajiri wake unaingizwa na lebo yake.
Kumbuka kwamba wanamuziki kama Lil Wayne, Nick Minaj, Drake, Tyga na wengine wengi walichangia kumpatia jamaa mkwanja wa maana. Kidogo watu hao walivyojiondoa, ndipo utajiri wake uliposhuka kutoka dola milioni 140 hadi milioni 110.


DRAKE
rs_1024x759-160904075431-1024.drake-tattoo.cm_.9416.jpg
Kwa mara ya pili mfululizo, jamaa huyu raia wa Canada, Drake Aubrey anaendelea kushika nafasi ileile ya tano japokuwa utajiri wake umeongezeka. Mwaka jana alikuwa na utajiri wa dola milioni 60 (zaidi ya Sh. Bilioni 120) ila kwa sasa ana utajiri wa dola milioni 90 (zaidi ya shilingi bilioni 180).
Kilichompa utajiri huo mwaka huu ni ziara yake ya kimuziki aliyofanya duniani iliyokwenda kwa jina la Boy Meets World ambayo alikwenda kutumbuiza sehemu mbalimbali na kumfanya kuwa hapo alipo. Kwa nchini Marekani, alipiga majimbo kama Nevada, New York, Washington DC na sehemu nyingine.

YEEEEZY.jpg



TUNAJIFUNZA NINI?

Wote hao ni wanamuziki, lakini ukiangalia, hawaingizi fedha kupitia muziki pekee.
Wana mambo mbalimbali wanayoyafanya. Wanamuziki wa Bongo ni lazima wajue kwamba ili wawe matajiri hawatakiwi kufanya muziki peke yake.
Wanatakiwa kuanzisha vitega uchumi vingine kwani wakifanya muziki tu, hawatapata fedha zaidi ya hizo wanazozipata. Ili uwe bilionea ni lazima uwe na vyanzo mbalimbali vya mapato, vinginevyo, hutapiga hatua, kila siku utaendelea kuwa palepale ulipo.
 
Nikajua unaelezea jinsi wewe unavyopiga hizo pesa kumbe unawaelezea wanaume wanavyopiga pesa!! Acha mimi niendelee kuzubaa tu.
 
Back
Top Bottom