Da Vinci XV
JF-Expert Member
- Dec 7, 2019
- 3,871
- 6,468
Naam
Naam yeye ni zawadi ya kimwambao, binti wa pwani. Sijui nimuite malaika wa kibantu, kihabeishia au kiajemi sielewi nimuweke kundi lipi hata
Unaweza kuuona uzuri wa wake pia kwa kuitazama tu ngozi yake, laini yenye mvuto usiomithilika usio wa dukani ambao umetunzwa vyema mara nyingi huonekana kupitia mikono yake, sura na miguu tu.
Sauti yake ya upole yenye aibu tele , si nyembamba sana wala si ya kukwaruzaa , nadhani haitokuwa tofauti na kinubi cha Mfalme Daudi au ndege mzuri wa mwituni.
Ni rahisi sana ,kuubaini na kuutambua uzuri wake kwa kutazamaa macho yake makubwa na maangavu yenye "haya" nyingi mno.
Marafiki zake wachache tuliowafahamu, hawakuacha kunadi kwamba nafasi ya kuushinda moyo wa mwali huo ni kama vile wazungu waitavyo kwa lugha yao eti " GOLDEN CHANCE" ni kama kuishinda Medali ya dhahabu katika michezo ya OLYMPIC.
Mitindo ya nywele zake imefichwa katika hijabu kama ilivyo mila na desturi za watu wa mwambao, lakini tabasamu lake jepesi na zuri muda wote , lilichokonoa hisia za wanaume wengi wakwere na wasio wakwere, wahuni kwa wastaarabu
Nadhani hata wanawake wenzie muda mwingine walitamani kuwa wanaume ili japo kidogo wapate nafasi ya kumchombeza mwanamwali huyo.
Tukiwa katika Chuo X hapa Nchini cha Afya bidada yule akiwa anachukua kada ya Uuguzi katika ngazi ya Degree,mimi nikiwa katika kada X , mara yangu ya kwanza kumuona nlibahatika kukutana naye wakati wa Masomo ya Vitendo (hospitalini) hapa, haswa sikutaka kujiuliza mara mbili kama binti yule ni mzuri haikuhitaji hata Ujuzi wa Veta kubaini binti yule alikuwa mrembo kuliko wengi niliowahi kuwaona.
Nlitamani nimsimamishe mara kadhaa wa kadhaa japo nimsabahi au japo nimkonyeze ,hayo yote nayo sikuyaweza labda ni kutokana na uwoga wangu kutoka kwa hawa mabinti wavutiao.
Nilitamani japo nimsikie hata kwa bahati mbaya akinisemesha lakini sikuambualia chochote zaidi ya mfadhaiko na mawazo mithili ya mfa maji asiyeisha kutapatapa., nilibahatika ,kumsikia tu alipokuwa anahudumia wagonjwa au akiwa anazungumza na marafiki zake bado sauti yake ni ile ile ya upole na huruma.
Kama kijana niwaye Rijali , nikaanzisha utaratibu uliojenga tabia kama si mazoea popote pale nitakapomuona ningelimsalimia naye pasi na kusita basi angelijibu kwa uchangamfu usiokera kana kwamba tumejuana miaka 6 au 7 nyuma
Naam, huu ndo upekee mwingine nlioupenda, kwa binti huyu wakimwambao, kingine kinachovutia zaidi ni ile rafudhi tamu ya Kizanzibaari. Nikajiapiza basi katika utaratibu huu, nijaribu kuomba hata Meeting amabayo ingeniwezesha, kimjua zaid kiundani bidada yule.
Sikutegemea
Lilikuwa pigo la ghafla na la kipumbavu, kwa mwanaume mwerevu, nikajilaumu kwa kutaka meeting bila ya kufanya mbinu zinginezo za kijemedari nizifanyazo wakati ninapowinda wadada wenye haiba kama ya kwake na huzaa matunda , kwa huyu binti nilijilaumu kwa kukurupuka , nikajikuta nikiyalaumu maamuzi yangu kuliko hata nlivyomlaumu Nyoka kumshawishi , Eva na Mumewe kula Tunda.
Wakati huo wote nikiitupia lundo la matusi akili yangu kwa maamuzi yangu, nlikuwa nikisubiri majibu ya bidada huyu huku nikitamani hata kwamba nisingeomba makutano yale... baada ya kuwasilisha ombi la meeting, nlizunguka wodi kadhaa nikiwa bize na yakwangu lakini akili yangu haikuwa pale , nliwaza kama bibie yule angereact vipi na maombi yangu ya kipumbavu na ya gafla.
Nikiwa sina hili wala lile nmejiinamia mara nikaskia sauti ya kike kutoka nyuma yangu ikiita "Dr. D" Sikutaka kugeuka nilitaka kubaini kwanza ni nani aliyeita hivyo, nilitamani awe yule bibie mrembo lakini hapa nikajisahihisha kwamba hata jina langu hakuwa akilijua basi pengine hawa ni wahudumu wa pale hospitalini au wanafunzi wenzangu.
Wakati nikisubiri sauti hiyo irudie mara ya pili mara nikagutuka alieniita yuu mbele yangu , ikimaanisha alishanikaribia na kuja mbele yangu
Hamaad! alikuwa yule bibie , akanisogelea na kuachia tabasamu lake jepesi lisirokera, akasema naona meeting yetu iwe after work time, muda tutakaochia shift , tena cafteria mda wa kupata Lunch.
Kabla hata sijajibu alishaanza kugeuka kuchepukia wodini ambako pengine nadhani alikuwa anamuwahi mgonjwa kwa ajili ya kumhudumia,
Akili yangu ikajawa na furaha isiyo kifani mtoto huyu kukubali japo kutenga muda wake kwa ajili wa kuniskiliza kijana ambaye mpaka muda huo nlikuwa sijui nitaongea nini na bibie huyu.
Furahaa hii ilizidi hata nikasahau, kujiuliza jina langu alilijulia wapi, nikagundua upekee wa binti huyu ni ule moyo wake wa dhati tofauti na warembo wengine wengi ambao hata salamu yako inaweza isijibiwe popote unapojaribu kufanya jambo la namna hiyo kwake.
Nikaelekea ofisini , kujiandaa kana kwamba nlitakiwa kuhutubia taifa, nikjitizama mara kwa mara kwenye vioo vya hospital , na kupanga maneno kadhaa wa kadhaa wakati wa meeting.
Zilibaki kama dakika 42 au 43 kuufikia muda huo , mara ya mwisho kuitazama saa yangu.
NGOJA NIVUTE PUMZI KIDOGO THEN NIENDELEE