BCOM ni bachelor of commerce, so ni mambo ya biashara, ila kama wenzangu walivyosema hapo juu kuwa bcom imegawanyika kwenye nyanja nyingi kama vile bcom finance
, accounting, management marketing, enterpreneur ship na kadhalika. Na pia ujue bcom ya chuo kimoja mathalan udsm mtaala na content yake ni tofauti na vyuo vingine kama mzumbe, saut na vinginevyo. So kwanza inavidi wewe uwe na malengo ya kutaka kuwa nani ukimaliza chuo kisha unasoma koz itakayokufikisha kwenye lengo au malengo yako. Mfano mimi nilipenda kuwa mfanyabiashara so nikachagua koz ya business administration, kuhusu kumajor accounting niliona kuwa ukibobea kwenye accounting kaz zake ni nyingi zaid kuliko major zingine kama marketing, management, human resources au enterpreneurship. So have a plan, stick to your plan, focus and work hard kijana...