msafiri.razaro
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 1,241
- 735
Hujanielewa. Jiulize wewe ni nini? Ni Mwili? Au Ni Roho? Mungu amemuumba binadamu kwa mfano wake. Je huo mfano ni Kama Mwili? Au kama Roho? Kukusaidia Binadamu ni Roho inayotumia akili kupata Busara na yakutumikisha mwili kutenda na ayatakayo. Mwili unaumbwa na mwanadamu kuanzia mimba na kuendelezwa kuumbwa na mwenye mwili kwa kula chakula, Kuvuta hewa na kunywa Maji, unabadilika ukubwa na unazeeka kutoka Mimba, Utoto, Ujana, Mpaka Uzee na hufa baada kuachwa na Roho. Kama vile Roho ilivyoingia kwenye mimba ndivyo inavyotoka siku mwili unapokufa. Roho haifi bali mwili unakufa. Sasa kama binadamu ni Mwili basi anakufa lakini kama Roho hafi. Kwa jibu la mtoa mada kuwa kifo fake, its true on Self(Roho) side. Yaano kwa Roho itajikuta kama imetoka ndotoni lakini kwa kiulimwengu (wafiwa) wataona ndugu yao amekufa kwani hawana uwezo wa kuiona Roho. Sasa pale niliposema ukitaka kumjua mungu anza kumjua binadamu na anza na wewe nilikuwa na maana in English, If you want to know God start by finding your true identity. Ukiweza jua wewe ni Roho, na ukaweza kuwa Rohoni kwako, utaweza kujua nini Roho yako inataka katika uhai wake ndani ya mwili wako, na mahusiana yako na viumbe vingine na ulimwengu kwa ujumla, Asili yake nini?, umetoka wapi na nini kitafuata baada kuwacha mwili yaani kifo.Binaadamu tunaishi nao mkuu ila ni tofauti na Mungu,hakuna anayeishi nae wala aliyewahi kumfanyia uchunguzi huko aliko na kuja na mrejesho.
Sent using Jamii Forums mobile app