Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,292
Tunaishi katika nchi ambayo hakuna aliye juu ya sheria, yeyote yule ambaye anataka dhamana ya utumishi kusema kweli uaminifu ni kigezo kikuu.
Sababu hii ndiyo iliyopelekea serikali yetu kuhakiki vyeti katika zoezi lililofanyika nchi nzima.
Hata hivyo zoezi hilo halijafanyika kwa watumishi wa kisiasa, Je kwa nini tuwe na standard mbili tofauti, kwa viongozi wa kisiasa na watumishi wengine wa serikali?
Zimepita taarifa mirandaoni juu ya viongozi waliosemwa kughushi elimu, japo hili halijathibitika lakini ni.muhimu kama hawa wangesafishwa kupitia uhakiki ili umma ujiridhishe zaidi kwamba hakuna uvunjifu wa uaminifu kutoka kwa hao.
Laiti uhakiki ungefanyika tuhuma hizi zinazozagaa kwa kasi mitandaoni kuhusu mkuu mmoja wa mkoa kutumia jina na cheti ambacho si chake zingepata majibu mujarabu.