Acacia Options to Pay U$300m

Acacia Options to Pay U$300m

aisee wazungu wanahangaika balaa!
kila siku press release!
Hii ni dalili ya mfa maji.
magufuli amewashika pabaya sana!
yule mkalimani nasikia aliwekwa kando wazungu wasijetambua walichokuwa wanaelezwa watanganyika !!
 
PM aliwahi kukurupuka na kusema eti kuna kampuni itajenga mtambo kuchenjua Chunya.....pale pale nikamdharau PM wetu ambae awamu hii ni kama hayupo anazidiwa nguvu....na RC mmoja na pia anazidiwa info toka juu na RC mmoja!!
 
Mara mgawano wa 50 fifty mara migodi inafungwa! Mara mitambo italetwa? Hivi hiyo dhahabu imebakia kiasi gani?
 
Hivi hakuna habari zingine za watu kuongiza pesa mkawa mnazirusha humu kuliko haya ya kampuni hiyo kila sekunde.. maana mnaboa sasa.

Kuna mengi mnaweza kuelimishana na watu nchini wakaanza kupata pesa ndefu na kuongea kama hao mnawaongelea kama vile nyie bado watumwa wa hao watu...
Nani kakwambia ugunguw hiyo thread?? Unaboa wewe unayewashwawashwa
 
From Day 01 Acacia walishasema kwao not economically viable kufanya uchenjuaji nchini! By the time, tulikuwa tunasafirisha wastani wa tani 50K za mchanga!!!

Kwa shehen kama hiyo, economical investment ilikuwa USD 500M !! Tulipoleta hii hoja hapa tukaambiwa vibaraka wa Acacia na kwamba tumelipwa kuja kuwatetea!

Tulipotoa changamoto ya ni kwanini basi serikali isiyo ya vibaraka isijenge hizo smelters; hakuna aliyewahi kutoa jibu la maana zaidi ya wale wanaoingia Google na ku-Google Copper Concentrates Smelters bila kufahamu not all copper concentrates smelters are the same!!!

Ukifanya Google ya bila kujua unatafuta nini hasa, ndani yake utakutana na smelters za hadi USD 25K na ndizo hizi ambazo watu wanaamini unaweza kuzitumia pale Buzwagi na Bulyanhulu wakati it's not!!!

Mkuu Pascal Mayalla, kuna thread yako ya majuzi bado sijapata muda wa kuitafakari lakini ulitaja kuhusu smelters moja somewhere in US! Unaweza kunipa link au enough info kuhusu hiyo smelter niangalie kama ndiyo hasa tunayohitaji?! Manake kama ni yenyewe basi itafaa sana kwa sababu mgodi mmoja wapo unaozalisha makinikia unafungwa soon na kwahiyo capacity itafaa!!!

However, it's not all about capacity but economic viability of a given smelter!!!
Mkuu Chige, hii thread yangu, ilitokana na thread yako
Wataalamu Hawa Wachunguzwe!,Jee Kuna Posibility Walihongwa ...
kuna smelter ndogo za hadi ya tani 30 tuu kama ile ya Stillwater Mining ya nchini Marekani inayogharimu dola milioni 300 tuu!.

Paskali
 
chige nashukuru sana kwa ufafanuzi mkuu.
Tuliingia kwenye haya majadiliano tukiwa tayari tumeshaamua tunataka mwisho uweje hata kama hauna uhalisia.

Ndio maana mkubwa alipoambiwa mazungumzo mazito, akaendelea kulazimisha waendelee na haya ndio matokeo yake sasa.

Inabidi siasa, mihemko na ushabiki uwekwe pembeni. Utaratibu wa kupitia sheria na mikataba ya madini ifanykushirikisha wadau wenye sifa. Kama hatuwezi, bora hata tulipe pesa ya consultancy.
 
Pascal Mayalla hapo wamesema wanalipa ila kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa chini ya hiyo kampuni mpya na kuzingatia terms watakazokubaliana. Hapo kwenye hizo terms za ulipwaji wa hizo USD 300 M bado napo kuna kitendawili.
 
Mkuu Samaritan, lugha ni tatizo, ndio aana hata mtoa mada hii ameshindwa kutafsiri, walichosema ni kwanza wamekubali, lakini kwenye kulipa hizo milioni 300, they don't have the capacity to pay upfront, jamaa akasema ili hizo pesa zipatikane, kwanza ni lazima zile conteiners zitoke, ziuzwe, wadungulize ndipo walipe. Hivyo suala sio kulipa bali ni terms of payments na amounts, ila zitalipwa.

Tatizo langu hapa ni hawa jamaa tunawadai kutokana na kutuibia kwenye mchanga, sisi tumepiga mahesabu ya makisio ya tunachowadai, hesabu zimekuja ni trilioni 450. Acacia akatugomea kata kata kuwa hakuna kitu kama hicho. Baba mtu Barrick, kaingilia kati, tumekubali kukaa nao mezani kujadiliana. Jee msingi wa majadiliano ni nini?, nilidhani ni Add to dictionary kwanza kuhusu hizi trilioni 450, kisha tuzungumze namna ya kuthibitisha kuwa tulikuwa tunaibiwa kwa kuuchenjua mchanga uliopo, na tatu ni kuzuia kuibiwa kwa kuchenjua wenyewe, halafu haya mengine yote ni ziada.

Watu wamekaa siku 80, wametupa walichokubalia, hakuna hata hoja moja katika yale ya msingi, bali kubwa ni ahadi ya fedha za zawadi ya dola milioni 300 ambazo sii sehemu ya deni, wala deni halijazungumzwa chochote, hakuna chochote kuhusu uchenjuaji, wala kutaka kuthibitisha deni, wala kutambua tunaibiwaje.

Tafsiri yangu kuhusu hiki kishika uchumba ni hongo tuu kwa jina zuri la good faith, ili turuhusu mchanga uondoke, bila kujua kilichomo!.

Time will tell.

Paskali
 
Mkuu Bams kwanza asante sana kwa hii kitu especially the voice note ila naomba nikurekebishe kidogo, hiyo hesabu ya vat receivable has nothing to do na ile kishika uchumba chetu cha dola milioni 300, wamesama cash hiyo ya kulipa kwa mara moja ndio hawana, ila kidogo kidogo, watalipa.
  1. In principle, Acacia wamezikubali hoja zote za makubaliano ya serikali na Barrick.
  2. Itaundwa kampuni mpya ambayo serikali itakuwa na 16% shares na mgowanyo wa 50/50 ni kwenye economic benefits and not on profits.
  3. Watalipa hiyo dola milioni 300 ila sio upfront but in instalments kwa sababu hawana hiyo cash
  4. Lengo ya yote haya ni mchanga wa dhahabu uruhusiwe kuondoka.
My Take.
The borne of contention ni tunaibiwa kwa sababu hatujui kilichomo kwenye ule mchanga. Kama kufuatia ahadi ya kishika uchumba hiki tutaruhusu mchanga uondoke tena bila kujua kilichomo, kiukweli Tanzania tutakuwa ni nchi ya ajabu sana!.

Kwenye press conference hiyo ya 30 minutes hakuna popote wamezungumzia kutujengea uwezo kuchenjua na kwenye makubaliano hayo hakuna lolote kuhusu uchenjuaji hivyo it's official mchanga utaondoka!. Swali la kujiuliza ni tuliuzuia mchanga ule ili kupata nini?. Nilidhani tuliuzuia ili kujua kilichomo!. Na hiki kishika uchumba ni cha nini?, sio kisika uchumba ili mwali wetu aondoke bila kulipiwa mahari?.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Mkuu mchanga kuondoka kwa muda huu lazima uondoke. Kuhusu kuibiwa si kama ilivyokuwa kabla ya makubaliano na itakuwa kwa kupenda kwetu au kujiibia wenyewe. Sasa hivi kwenye mchanga wao chao ni dhahabu tu madini mengine ni yetu hivyo kujua yamo lazima tuyapime na tuyafuate huko wanakotoa dhahabu na sisi kutoa ya kwetu. Pia dhahabu ya ndani ya mchanga imo kwenye hesabu ya mgaona malipo mengine. Muhimu ni kuwapo kwa watanzania waaminifu wa kusimamia michakato yote. Kwenye muhutasari wa Prof Kabudi haya maelezo yamo je hukuyasikia? Au umeyasikia isipokuwa hujayatia maanani na kuona kama ni porojo tu. Ungeyatia maanani mashaka yako yangelenga humo.
 
aisee wazungu wanahangaika balaa!
kila siku press release!
Hii ni dalili ya mfa maji.
magufuli amewashika pabaya sana!
Acha kuweweseka soma kwanza
Mnatuumiza vichwa hatuwezi kupanga bajeti hivi .
Kutoka NOAH@ hadi m300$ sasa mnatuletea hii habari eti m125$ baada ya VAT
😕 😕 😕
 
Following the Agreement made between Barrick and the Government of Tanzania, Acacia Management in its yesterday briefing, clarified few items. Below is the summary:
  • The Agreement is in principle framework between Barrick and the government of Tanzania
  • A few elements of it will involve formation of a Tanzanian operating company
  • Economic benefits from this company will be shared 50/50 which includes the 16% government free carried shares
  • Acacia to make a payment of of 300m dollars. Terms of the payments will be reviewed by the working groups
  • Those working groups will also review the conditions for the lifting of the concentrates export ban
  • It is frustrating for every one
  • Cash position continue to fall with net cash $24m
  • Total VAT receivable now stands at $175m
  • Acacia is a UK PLC company, will require presence in London
  • Barrick are aware of our balance sheets
Kwa maelezo ya Acacia, ni kuwa upo uwezekano wa kufikia maafikiano ya dola milioni 175 wanazoidai serikali kuwa sehemu ya malipo ya dola milion 300. Kama hilo likikubalika ina maana cash tutakayoisubiria itakuwa dola milioni 125.

upload_2017-10-23_9-29-23.png
 
Hivi hakuna habari zingine za watu kuongiza pesa mkawa mnazirusha humu kuliko haya ya kampuni hiyo kila sekunde.. maana mnaboa sasa.

Kuna mengi mnaweza kuelimishana na watu nchini wakaanza kupata pesa ndefu na kuongea kama hao mnawaongelea kama vile nyie bado watumwa wa hao watu...
Unanjaa kiasi hiki kumbe?
 
Acha kuweweseka soma kwanza
Mnatuumiza vichwa hatuwezi kupanga bajeti hivi .
Kutoka NOAH@ hadi m300$ sasa mnatuletea hii habari eti m125$ baada ya VAT
😕 😕 😕
upload_2017-10-23_9-30-0.png
 
Unanjaa kiasi hiki kumbe?

Ha ha haaaaa
Na wewe umefurahia kuniquote eeeh

Jione sasa unafikiria njaa kama vile unanifahamu.. fikiria utakavyo.. ukweli umepenya. Nipo hapa nasaga mawe nipike ugali kwa unga wake.

Mnasikitisha na msipobadilika mnalo.
 
Following the Agreement made between Barrick and the Government of Tanzania, Acacia Management in its yesterday briefing, clarified few items. Below is the summary:
  • The Agreement is in principle framework between Barrick and the government of Tanzania
  • A few elements of it will involve formation of a Tanzanian operating company
  • Economic benefits from this company will be shared 50/50 which includes the 16% government free carried shares
  • Acacia to make a payment of of 300m dollars. Terms of the payments will be reviewed by the working groups
  • Those working groups will also review the conditions for the lifting of the concentrates export ban
  • It is frustrating for every one
  • Cash position continue to fall with net cash $24m
  • Total VAT receivable now stands at $175m
  • Acacia is a UK PLC company, will require presence in London
  • Barrick are aware of our balance sheets
Kwa maelezo ya Acacia, ni kuwa upo uwezekano wa kufikia maafikiano ya dola milioni 175 wanazoidai serikali kuwa sehemu ya malipo ya dola milion 300. Kama hilo likikubalika ina maana cash tutakayoisubiria itakuwa dola milioni 125.
Tooobaaa yaani tumeshushwa kutoka 450 trillion?
 
Back
Top Bottom