Watanzania wenzangu,tujiulize maswali magumu.ustadi huu mkuu wa kung'oa watu kucha ,macho,na meno kisha kutesa na kutelekeza mtu akiwa kufani kipo wapi.
Mkuu wa chuo hicho ni nani na anadhaminiwa na nani? na kwa mwaka anasajili wanachuo wangapi?
Yaliompata ABSALOM KIBANDA,NA MTANGULIZI WAKE DOCT. STEVEN ULIMBOKA yanatisha.ni lazima hapa kuna genge la watu ambao wamefunzwa vilivyo kudhuru watanzania wenzake.
Nini hasa mwandishi huyu alichokifanya mpaka haya yanamfika? na laani kwa nguvu zote,MUNGU AMREHEMU MWANDISHI HUYU.
.......
Natumaini kuwa CHADEMA wamesikia na watakujibu. wakati wanamtesa Dr Ulimboka, kulikuwa na mgomo wa madaktari na tukio hilo waliliibua ili kuchochea mgogoro huo.
Walitegemea kuwa baada ya tukio hilo, makali ya mgomo yataongezeka na wao wachukue nchi kilaini kutokana na shinikizo la wananchi kama ilivyotokea libya, tunisia na misri.
Walisahau kuwa Tanzania si nchi ya Kiarabu. mgomo uliisha na Dr Ulimboka amepona. Sanasana wanamfanya ulimboka aishi kwa kificho kutokana na kumsingizia mambo mengi ya aibu ikiwa ni pamoja na kulawitiwa na kuharibiwa nyeti zake. Leo hii kila anakopita anaitwa shoga.
kuhusu hili tukio la bwana kibanda, huyu mtu alikuwa mhimili mkubwa sana kwa CHADEMA wakati akiwa mhariri mkuu wa gazeti la Tanzania Daima.
Walimtumia katika mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na propaganda dhidi ya ccm na serikali yake. bila shaka anayo mengi moyoni.
kuondoka kwake Tanzania Daima hakukuwa kwa heri. CHADEMA wakati wote wana hofu kuwa siri zao zitavuja kama wanavyofanya vijana akina SHONZA na MWAMPAMBA. kwa vile kibanda anazo taarifa nyeti kifuani kwake, suluhisho waliloliona ni kumteka ili wamuue.
Pia wamempofua macho ili asiendelee kutumikia katika ajira yake ndani ya New Habari Corporation. Mungu hajataka hayo.
Na hilo walilifanya kwa kuamini kuwa hawataguswa tena kama ilivyokuwa kwa ulimboka kwa vile Kibanda ana kesi dhidi ya serikali na kwa hiyo serikali ndiyo itakayolaumiwa tena.
hizo ni mbinu mbaya za kutaka madaraka na ni mbinu chafu dhidi ya raia wasio na hatia. Halafu lazima watanzania tuhoji uadilifu wa hawa viongozi wa CHADEMA, pamoja na kulelewa na kufanya kazi za kanisa, wamekosa huruma dhidi ya viumbe wasio na hatia.
Wana visasi ambavyo havina mfano wake. Si watanzania mnakumbuka tukio la kifo cha wangwe? tafakari na chukua hatua.