Aboubakar Mzuri wa BSS akiri kutumia madawa ya kulevya, apelekwa sober

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,137
Katika hali ya kushangaza kabisa, mshiriki wa Shindano la Bongo Star Search (BSS) 2008, Abubakar Mzuri, amepelekwa katika kituo cha udhibiti wa matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’ cha Pilli Missannah Foundation (Soba) kilichopo wilayani Kigamboni jijini hapa baada ya kujitumbukiza kwenye matumizi ya madawa hayo, Uwazi limebaini.

Akizungumza na Uwazi kwa masikitiko makubwa mwishoni mwa wiki iliyopita, Mzuri alisema kuwa alianza kujiingiza kwenye matumizi ya unga mwaka 2013 kutokana na kufuatana na marafiki mbalimbali aliokuwa anakutana nao mitaani, wakiwemo wabaya.

Akiendelea kuzungumza Mzuri, alisema kuwa kabla ya kujichanganya kwa marafiki mbalimbali hakuwahi kabisa kufikiri kama ipo siku atajiingiza kwenye madawa ya kulevya kitu ambacho kwa sasa kinamfanya ajione hana thamani tena kwenye jamii yake kama alivyokuwa huko nyuma.

ANAJUTA, AWALAUMU MARAFIKI
“Najuta sana kutumbukia kwenye matumizi ya unga kwa sababu marafiki ndiyo walinidanganya na kujikuta najiingiza kwenye kitu ambacho kimeharibu kabisa maisha yangu, mwelekeo wangu na kuzima ndoto zangu zote.

Mwanzo nilikuwa napewa sigara na shisha na marafiki zangu, sikuwa nimegundua ila baadaye ndio nikajua, kumbe walikuwa wakinichanganyia na unga. Kutumia madawa ya kulevya kumeniharibia maisha,” alisema Mzuri.

Mwanamuziki huyo aliongeza kuwa, tangu alipojiingiza kwenye matumizi ya unga amekuwa si mtu wa upendo kama zamani, pia amekuwa si mtu hata wa kuwa karibu na watu kama walivyo binadamu wengine kitu ambacho kinamuumiza sana kwa sasa.

“Nilibadilika, siyo mtu wa upendo kwa watu kama ilivyokuwa huko nyuma. Naumia sana, najiuliza kwa nini nilitumbukia kwenye matumizi ya madawa haya ya kulevya ambayo yamezima ndoto yangu ya muziki na vitu vingine vya kifamilia,” alisema Mzuri.

Mwanamuziki huyo alipenda kuwashauri wanamuziki wenzake waepuke na vishawishi mbalimbali kutoka kwa marafiki kwani mara nyingi vinawapoteza na kuzima ndoto zao za kusonga mbele.

KUHUSU BSS
Shindano la BSS lilianza nchini mwaka 2006, mwaka 2008, Mzuri aliingia kwenye Tano Bora ambapo mshindi wa kwanza alikuwa Misoji Nkwabi.
Kutokama na uimbaji wake, Mzuri alikuwa akifananishwa na Mbongo Fleva, Abubakar Shaban Katwila ‘C-Chillah’ akiaminiwa kuwa angevuma sana.

Alishawahi kuimbia Top Band ya jijini Dar ambayo kwa sasa haipo tena. Mwaka 2016, Mzuri alikumbwa na madai ya kufumaniwa na mke wa mtu katika nyumba moja iliyopo Magomeni jijini hapa na mwenyewe kusema kuwa, fumanizi lake lilitengenezwa na wabaya wake ili kumchafulia jina.

Tazama video....
 
Inauma Sana.. Tuungane Jamani kutokomeza haya mambo mimi mwenyewe Shahid nimewahi kutumia mara mbili madawa ya kulevya sitaki kukumbuka Ila marafiki sio Mpango.. Tuungane sote
 
"Alishawahi kuimba Top Band" ya akina (Q chillah na TID myama a.k.a Paka according to Steve Nyerere Bashite)

"Marafiki wabaya"
 
Back
Top Bottom