"Abortion" inayokubalika kimaadili ni hii tu!

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,261
1,222
Wana JF abortion(utoaji mimba) inayokubalika kimaadili ni moja tu. kwa ufupi zipo aina kuu 2 za abortion:

1. Spontaneous or Natural abortion wakati mwingine inaitwa miscarriage hapa mimba imetoka yenyewe bila mtu kuifanya itoke. hii haina shida kimaadili.

2. Induced Abortion, hii pia ina sehemu kuu mbili:

a) indirect abortion or theraupetic abortion. hii inafanywa ili kuokoa uhai wa mama iwapo kuna tishio la mama kufa mimba ikiendelea. haina shida kimaadili ila isitokee mimba itolewe kwa lengo la kumtibu mama ugonjwa ambao hauwezi kusababisha kifo cha mama.

b) direct abortion. hapa mimba inatolewa kwa sababu yoyote isiyo na uhusiano wa kuokoa uhai wa mama mf. mimba isiyotarajiwa au isiyotakiwa au inaonekana mtoto atakayezaliwa atakuwa mlemavu au wa jinsia wasiyoitaka au mimba imepatikana kwa mtu kubakwa n.k. abortion hii haikubaliki hata kidogo kimaadili.

Kutoa mimba katika hatua yoyote ya ukuaji ni KUUA. mimba inaanzia pale inapotungwa yaani at 'conception'.

TUTUNZE NA KUULINDA UHAI NDUGU ZANGU.
 
Hiyo direct abortion inawezekana ndio inaongoza kufanywa na hawa ndugu zetu.
 
Hiyo direct abortion inawezekana ndio inaongoza kufanywa na hawa ndugu zetu.
japo cjajua ndugu zetu umemaanisha nini, ila hiyo ndo inayoongoza kufanywa navwengi. hao wote WAMEUA viumbe wasioweza kujitetea na wasio na hatia
 
Punyeto na abortion by my side are the same thing being done in different ways.
punyeto na abortion sio sawa. abortion ni kuua kiumbe kilichotokana kuungana kwa mbegu za kiume na kike. punyeto inahusu mbegu za upande mmoja tu na hakuna mimba hapo. ila zote hazikubaliki kimaadili, kwani punyeto inaashiria ubinafc na inazuia mpango wa Mungu wa uumbaji
 
Hivi kabla hujani~quote umenielewa?
 
Mpango wa mungu wa uumbaji si kwenye science haupo? Na haya mambo..direct abortion ni science ya binadamu katika kupambana na mazingira yake
 
Back
Top Bottom