Abood yapata Ajali!!!

Twilumba

Platinum Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
13,581
Reaction score
16,450
MZIMU wa ajali unaendelea kuisumbua kampuni ya mabasi ya Abood! Mchana wa leo basi lake lingine limepata ajali eneo la Mtego wa Simba, nje kidogo ya mji wa morogoro. Basi hilo, lenye namba za usajili T453 AES, lilikuwa likitoka Morogoro kuelekea jijini Dar es salaam. Limegonga kwa nyuma Trekta aina ya Masey Ferguson (pichaji juu) lenye namba za usajili T 583 ALK, na baade kumgonga mzee mmoja laiyekuwa akiendesha baiskeli akitoka kuchota maji kisimani. Katika ajli hiyo hakuna mtu aliyekufa lakini hali ya dereva wa trekta na yule wa baiskeli, zimeelezwa kuwa ni mbaya sana na wako hospitalini.

Source: Dastan Shekidele, Morogoro
 

Attachments

  • Abood Bus 2.JPG
    44.3 KB · Views: 301
  • Abood Basi.JPG
    35.4 KB · Views: 308
Mkuu mbona picha ya global publishers hii?
 
Alituma huko, ameshindwa kuweka humu kwanza coz sio member wa JF!!!
 
Pole kwa majeruhi, ahsante kwa taarifa.
 




Tatizo ni kutokuwa na viwango mbadala vya barabarani i.e. Signs, speed limit at certain area etc .... ..

Watanzania wataendelea kufa tu kama Inzi hadi pale watakapojua Serikali yao haiwajali. RIP waliopata ajali.
 
abood,abood,abood,hata mwez haujaisha,dah!ntaendelea kupanda HOOD
 
Aluuuuuuh!!!very serious....................................
 
miundo mbinu ya barabara inachangia sana kwa ajali hizi
 
Hivi ni kwa nini ajali Bongo hazipungui kama kwa wenzetu?
 
Oh pole sana walopata ajali, haya mabasi ya huyu bwana huwa nayaita machinjachinja kama rangi yao. me kwenda moro natumia Hood badala ya haya. Mwenye nayo yuko busy na mihadhara kwenye redio yake badala ya kuangalia usalama wa wasafiri!
 




Tatizo ni kutokuwa na viwango mbadala vya barabarani i.e. Signs, speed limit at certain area etc .... ..

Watanzania wataendelea kufa tu kama Inzi hadi pale watakapojua Serikali yao haiwajali. RIP waliopata ajali.
mkuu RIP ya nini tena akati ushaambiwa hakuna mtu aliefariki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…