Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,092
- 53,568
mmmhhh!!bibi hakuzimia....?!!!
Atutajie shirika la ndege na sisi tukapande huko basi.
Halafu nakaa na wewe, unanibagua sawa?
Namuomba muhudumu anipeleke festi klasi.
mmmhhh!!bibi hakuzimia....?!!!
Hao watu wanatuonea tu wivu na ngozi zetu na rangi nawanajua kwa hakika hawawezi kuipataNilikuwa nipo kwenye misafara yangu ya kikazi nikipanda ndege ya shirika moja maarufu la duniani kwa usafiri wa vyombo vya angani (jina tutalistahi), nikisafiri toka jiji moja la taila la ulaya kuelekea jiji jengine.
Ndani ya ndege kama kawaida kunakuwa shwari kwa mazungumzo ya chini kwa chini kwa wenye kujuana, au mizunguko ya wahudumiaji wa ndege (flight attendants) ambayo huwa wenyewe huifanya kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba hiyo mizunguko yao huwa haifanyi usumbufu kwa msafiri yeyote aliyekuwemo humo ndani.
Vile tunaonyeshwa mahala pa kuketi kwenye behewa la economy kutokana na tiketi zetu, tukasikia sauti ya kufoka na hasira kutoka kwa bibi mmoja mwenye umri wa makamo, asilia ya kizungu. Bibi huyo alieyekuwa amevaa nguo za kupendeza na kujiweka katika hadhi ya kung’ara kwa namna aluvyojivika na kulijikuta ameekwa kwenye siti iliyo pembeni na msafiri mwenye ngozi nyeusi. Yule bibi kwa kufoka akamwita mhudumu wa ndege kulalamika.
“Ni nini tatizo lenye kukusumbua madam” .. Aliuliza mhudumu wa ndege.
“Ina maana huoni?”... alijibu kwa hasira.. “Mmeniweka kwenye siti iliyo karibu na huyu nyani. Siwezi kabisa kukaa karibu na huyu binaadamu wa ajabu. Nitafutieni sehemu nyengine ya kukaa!”
“Tafadhali madam, punguza sauti na utulize hasira” … alijibu mhudumu … “ndege leo imejaa sana, lakini usihofu, nitajaaribu kuangalia kama kuna nafasi zilizo wazi”. Yule bibi wa kizungu kwa jeuri akabinua mdomo na matako na kukaa chini huku akiegemea upande upande kujiweka mbali na yule abiria mweusi kama vile yule abiria kapakwa na kinyesi mwili mzima.
Sote kwenye behewa tumepigwa na butwaa na tukio lile huku wengi abiria tukitikisha kichwa kwa masikitiko pamoja na hasira, akiwemo yule abiria mweusi mwezetu mtuhumiwa, lakini tukakaa kimya.
Muda mfupi baadae yule mhudumu wa ndege akarudi na good news kwa yule bibi ambae kipindi hicho jeuri ilimjaa mpaka mashavu kuvimba.
“Madam, kwa bahati mbaya economy class imejaa. Vile vile nimeangalia katika cabin service director na club nako vile vile kumejaa. Lakini bahati kuna siti moja tu imebaki katika first class”… Yule bibi tabasamu likamchomoka toka pande zake za mdomo.
Kabla hajafunua mdomo kusema neno, yule mhudumu wa ndege akaendelea “Ni vigumu sana kubadilisha tiketi ya ndege na kufanya mabadiliko ya mpangilio wa kuketi kwa wasafiri wakati tiketi za ndege zishatolewa, ila nimejadiliana na Captain wa ndege na kupata ruhusa yake . Kwa kuwa safari hii tumekupa tiketi iliyokulazimu ukae karibu na binaadamu wa namna hii mwenye sifa za ajabu”… ..hapo akamgeukia yule jamaa mweusi mtuhumiwa aliyekuwa ameketi pembeni mwa yule bibi wa kizungu, na kusema … “tafadhali tunaomba ukusanye mizigo yako, mheshimiwa, tushakuwekea seat yako katika behewa la first class”…
Basi ndege nzima ilipasuka kwa vifijo na shangwe kutoka kwa abiria wenzangu tuliokuwa tukishangilia pale yule abiria mtuhumiwa mweusi alipokuwa akielekea kwenye behewa la first class…
Ni kweli au ni stori tu mkuu, maana sio kwa ubaguzi huo jamani
Kwa hiyo kipi kiliwafrahisha nyie wengine? mtu kwenda daraja la kwanza au bibi kufanikiwa lengo lake la kukaa mwenyewe?
Lakini, Kama umebuni waraka huu, basi jihesabu ya kuwa wewe ni mchochezi namba moja wa ubaguzi Duniani.
Unapenda biskuti eeh heheh.
Safi sanaa,huyo mbaguzi hata sahau aibu hiyo aliyoipata maishani mwake.Nilikuwa nipo kwenye misafara yangu ya kikazi nikipanda ndege ya shirika moja maarufu la duniani kwa usafiri wa vyombo vya angani (jina tutalistahi), nikisafiri toka jiji moja la taila la ulaya kuelekea jiji jengine.
Ndani ya ndege kama kawaida kunakuwa shwari kwa mazungumzo ya chini kwa chini kwa wenye kujuana, au mizunguko ya wahudumiaji wa ndege (flight attendants) ambayo huwa wenyewe huifanya kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba hiyo mizunguko yao huwa haifanyi usumbufu kwa msafiri yeyote aliyekuwemo humo ndani.
Vile tunaonyeshwa mahala pa kuketi kwenye behewa la economy kutokana na tiketi zetu, tukasikia sauti ya kufoka na hasira kutoka kwa bibi mmoja mwenye umri wa makamo, asilia ya kizungu. Bibi huyo alieyekuwa amevaa nguo za kupendeza na kujiweka katika hadhi ya kung’ara kwa namna aluvyojivika na kulijikuta ameekwa kwenye siti iliyo pembeni na msafiri mwenye ngozi nyeusi. Yule bibi kwa kufoka akamwita mhudumu wa ndege kulalamika.
“Ni nini tatizo lenye kukusumbua madam” .. Aliuliza mhudumu wa ndege.
“Ina maana huoni?”... alijibu kwa hasira.. “Mmeniweka kwenye siti iliyo karibu na huyu nyani. Siwezi kabisa kukaa karibu na huyu binaadamu wa ajabu. Nitafutieni sehemu nyengine ya kukaa!”
“Tafadhali madam, punguza sauti na utulize hasira” … alijibu mhudumu … “ndege leo imejaa sana, lakini usihofu, nitajaaribu kuangalia kama kuna nafasi zilizo wazi”. Yule bibi wa kizungu kwa jeuri akabinua mdomo na matako na kukaa chini huku akiegemea upande upande kujiweka mbali na yule abiria mweusi kama vile yule abiria kapakwa na kinyesi mwili mzima.
Sote kwenye behewa tumepigwa na butwaa na tukio lile huku wengi abiria tukitikisha kichwa kwa masikitiko pamoja na hasira, akiwemo yule abiria mweusi mwezetu mtuhumiwa, lakini tukakaa kimya.
Muda mfupi baadae yule mhudumu wa ndege akarudi na good news kwa yule bibi ambae kipindi hicho jeuri ilimjaa mpaka mashavu kuvimba.
“Madam, kwa bahati mbaya economy class imejaa. Vile vile nimeangalia katika cabin service director na club nako vile vile kumejaa. Lakini bahati kuna siti moja tu imebaki katika first class”… Yule bibi tabasamu likamchomoka toka pande zake za mdomo.
Kabla hajafunua mdomo kusema neno, yule mhudumu wa ndege akaendelea “Ni vigumu sana kubadilisha tiketi ya ndege na kufanya mabadiliko ya mpangilio wa kuketi kwa wasafiri wakati tiketi za ndege zishatolewa, ila nimejadiliana na Captain wa ndege na kupata ruhusa yake . Kwa kuwa safari hii tumekupa tiketi iliyokulazimu ukae karibu na binaadamu wa namna hii mwenye sifa za ajabu”… ..hapo akamgeukia yule jamaa mweusi mtuhumiwa aliyekuwa ameketi pembeni mwa yule bibi wa kizungu, na kusema … “tafadhali tunaomba ukusanye mizigo yako, mheshimiwa, tushakuwekea seat yako katika behewa la first class”…
Basi ndege nzima ilipasuka kwa vifijo na shangwe kutoka kwa abiria wenzangu tuliokuwa tukishangilia pale yule abiria mtuhumiwa mweusi alipokuwa akielekea kwenye behewa la first class…
Ina video kabisa.. nafikiri mtoa mada ameitoa huko.Hii story nilishawahi kuisoma mahali fulani mwaka Jana au juzi na lilitokea nadhani ulaya au marekani... inawezekana mleta mada naye kaisoma kama mimi..
Ina video kabisa.. nafikiri mtoa mada ameitoa huko.
Mleta mada ni mwongo,hili tangazo linalopinga ubaguzi lilirushwa na TV flani majuuHii story nilishawahi kuisoma mahali fulani mwaka Jana au juzi na lilitokea nadhani ulaya au marekani... inawezekana mleta mada naye kaisoma kama mimi..
Mleta mada ni mwongo,hili tangazo linalopinga ubaguzi lilirushwa na TV flani majuu
Najua ubaguzi upo sana tuu ila nimekuuliza ni kweli au ni stori MkuuUbaguzi upo mkuu. Upo kupita huu. Tembea uone... ila tuombe mungu ukuepuke maana sio jambo la kufurahisha
Sasa nije na coffee "Starbucks" au africafe yangu?
Unaona eeh? Huyu kiumbe kwa biskuti hawezekani..