Abiria m-baguzi

Abiria m-baguzi

Waterlemon

Senior Member
Joined
Sep 2, 2016
Posts
143
Reaction score
199
Nilikuwa nipo kwenye misafara yangu ya kikazi nikipanda ndege ya shirika moja maarufu la duniani kwa usafiri wa vyombo vya angani (jina tutalistahi), nikisafiri toka jiji moja la taila la ulaya kuelekea jiji jengine.


Ndani ya ndege kama kawaida kunakuwa shwari kwa mazungumzo ya chini kwa chini kwa wenye kujuana, au mizunguko ya wahudumiaji wa ndege (flight attendants) ambayo huwa wenyewe huifanya kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba hiyo mizunguko yao huwa haifanyi usumbufu kwa msafiri yeyote aliyekuwemo humo ndani.

Vile tunaonyeshwa mahala pa kuketi kwenye behewa la economy kutokana na tiketi zetu, tukasikia sauti ya kufoka na hasira kutoka kwa bibi mmoja mwenye umri wa makamo, asilia ya kizungu. Bibi huyo alieyekuwa amevaa nguo za kupendeza na kujiweka katika hadhi ya kung’ara kwa namna aluvyojivika na kulijikuta ameekwa kwenye siti iliyo pembeni na msafiri mwenye ngozi nyeusi. Yule bibi kwa kufoka akamwita mhudumu wa ndege kulalamika.


“Ni nini tatizo lenye kukusumbua madam” .. Aliuliza mhudumu wa ndege.

“Ina maana huoni?”... alijibu kwa hasira.. “Mmeniweka kwenye siti iliyo karibu na huyu nyani. Siwezi kabisa kukaa karibu na huyu binaadamu wa ajabu. Nitafutieni sehemu nyengine ya kukaa!”

“Tafadhali madam, punguza sauti na utulize hasira” … alijibu mhudumu … “ndege leo imejaa sana, lakini usihofu, nitajaaribu kuangalia kama kuna nafasi zilizo wazi”. Yule bibi wa kizungu kwa jeuri akabinua mdomo na matako na kukaa chini huku akiegemea upande upande kujiweka mbali na yule abiria mweusi kama vile yule abiria kapakwa na kinyesi mwili mzima.


Sote kwenye behewa tumepigwa na butwaa na tukio lile huku wengi abiria tukitikisha kichwa kwa masikitiko pamoja na hasira, akiwemo yule abiria mweusi mwezetu mtuhumiwa, lakini tukakaa kimya.

Muda mfupi baadae yule mhudumu wa ndege akarudi na good news kwa yule bibi ambae kipindi hicho jeuri ilimjaa mpaka mashavu kuvimba.

“Madam, kwa bahati mbaya economy class imejaa. Vile vile nimeangalia katika cabin service director na club nako vile vile kumejaa. Lakini bahati kuna siti moja tu imebaki katika first class”… Yule bibi tabasamu likamchomoka toka pande zake za mdomo.


Kabla hajafunua mdomo kusema neno, yule mhudumu wa ndege akaendelea “Ni vigumu sana kubadilisha tiketi ya ndege na kufanya mabadiliko ya mpangilio wa kuketi kwa wasafiri wakati tiketi za ndege zishatolewa, ila nimejadiliana na Captain wa ndege na kupata ruhusa yake . Kwa kuwa safari hii tumekupa tiketi iliyokulazimu ukae karibu na binaadamu wa namna hii mwenye sifa za ajabu”… ..hapo akamgeukia yule jamaa mweusi mtuhumiwa aliyekuwa ameketi pembeni mwa yule bibi wa kizungu, na kusema … “tafadhali tunaomba ukusanye mizigo yako, mheshimiwa, tushakuwekea seat yako katika behewa la first class”…


Basi ndege nzima ilipasuka kwa vifijo na shangwe kutoka kwa abiria wenzangu tuliokuwa tukishangilia pale yule abiria mtuhumiwa mweusi alipokuwa akielekea kwenye behewa la first class…
 
Malizia vizuri msafiri mwenzetu. Mhhh! Bibiye kafanyaje? Hakumzaba kibao yule Mhudumu? Ningelikuwa ni miye, ningembusu kwa kheri Maamsap nkielekea First class! Oh! What a story.
 
Ingekuwa mimi saa nahama namtemea kohozi uyo bibi
 
wana busara sana hao wahudumu hebu taja jina tuwa acknowledge
 
Lakini, Kama umebuni waraka huu, basi jihesabu ya kuwa wewe ni mchochezi namba moja wa ubaguzi Duniani.
 
Ni kweli au ni stori tu mkuu, maana sio kwa ubaguzi huo jamani
 
Kwa hiyo kipi kiliwafrahisha nyie wengine? mtu kwenda daraja la kwanza au bibi kufanikiwa lengo lake la kukaa mwenyewe?
 
Bibi ni mmoja wa wenye hisa kwenye hiyo ndege na alikuwa akifanya tangazo indirect.
 
Mimi nadhani ningekuwa polisi nina kesi ya kujeruhi mtu hapo!
 
Back
Top Bottom