GM7
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 492
- 24
Wakati Tanzania kukiripotiwa matukio mbalimbali hasa ya ajali za moto, leo nimenasa tukio lingine majira ya saa 8:50 mchana (2:50PM) katika eneo la Iyunga karibu na kituo cha garimoshi cha TAZARA Mbeya ambapo basi la abiria aina ya Hiace liliwaka moto kama linavyoonekana kwenye picha.
Kwa mujibu wa walikuwa karibu kabisa na tukio abiria wote wamenusurika na hakuna aliyejeruhiwa.
Muda mfupi kabla ya kupatwa na tukio hilo basi hilo lilisimamishwa na trafiki waliokuwa eneo la TAZARA Mbeya na baada ya tu kuruhusiwa kupita gari lilienda mbele kama mita 100, na kusimama pembeni na kuamriwa kutelemka mara moja na ndipo baada ya dakika chache gari likashika moto na kuanza kuungua.
Mwenye swali anaweza kuniuliza kuhusiana na tukio hili maana nilikuwepo karibu kabisa na tukio.
Tumwombe Mungu atuepushe na majanga haya na mengine yote. Amina