Abiria kadhaa wanusurika kuungua baada ya gari kuwaka moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abiria kadhaa wanusurika kuungua baada ya gari kuwaka moto

Discussion in 'Jamii Photos' started by GM7, Oct 7, 2009.

 1. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wakati Tanzania kukiripotiwa matukio mbalimbali hasa ya ajali za moto, leo nimenasa tukio lingine majira ya saa 8:50 mchana (2:50PM) katika eneo la Iyunga karibu na kituo cha garimoshi cha TAZARA Mbeya ambapo basi la abiria aina ya Hiace liliwaka moto kama linavyoonekana kwenye picha.

  Kwa mujibu wa walikuwa karibu kabisa na tukio abiria wote wamenusurika na hakuna aliyejeruhiwa.

  Muda mfupi kabla ya kupatwa na tukio hilo basi hilo lilisimamishwa na trafiki waliokuwa eneo la TAZARA Mbeya na baada ya tu kuruhusiwa kupita gari lilienda mbele kama mita 100, na kusimama pembeni na kuamriwa kutelemka mara moja na ndipo baada ya dakika chache gari likashika moto na kuanza kuungua.

  Mwenye swali anaweza kuniuliza kuhusiana na tukio hili maana nilikuwepo karibu kabisa na tukio.

  Tumwombe Mungu atuepushe na majanga haya na mengine yote. Amina


  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Poleni sana ndugu zetu
   
 3. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  duh humo ndani ya basi kulikua na abiria? kama wamenusurika wakachinje kuku na kufanya ibada kumshukuru mungu wao kwa kuwanusuru na kifo kibaya cha moto
   
 4. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Abiria wote wamenusurika. Na bahati nzuri gari lilianza kuwaka likiwa limesimama, sijui lingekuwa kwenye mwendo sipati picha ingekuwaje. Kwa kweli wamshukuru Mungu na wafanye ibada ya kushukuru Mungu akiwemo na dereva mwenyewe ambaye mara baada ya kugundua tatizo kwenye gari lake aliamua kusimamisha gari pembeni na kuamuru abiria wote kushuka mara moja.
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kila kukicha majanga nini kilisababisha moto huo??
   
 6. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sina hakika sana na chanzo cha moto huo, ila baadhi ya mashuhuda wanasema maji ya kupoozea injini hiyo yalikwisha na wengine wanasema iliishiwa mafuta hivyo dereva alikuwa anaikaanga.
   
 7. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  madereva jamani, pls kagueni magari kabla ya kuanza safari, msiyaweke rehani maisha ya watu, chonde chonde,
   
Loading...