Abel Magembe Lugimba acha siasa za maji taka

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Kuna mtu kutoka Sumbawanga anaitwa Abel magembe lugimba. Bwana huyu anaonekana anautaka ubunge na ukuu wa wilaya kwa namna yoyote ile ila ameamua kutumia mtandao wa facebook kutukana watu mashuhuri kwa kisingizio cha siasa za maji taka.

Nilidhani Bw. Abel kama anatafuta uongozi ni vema hata heshima kwa viongozi waliomtangulia na wakubwa kwake akawapa. Bw. Abel amekuwa anaeneza uzushi na uongo kwa matukio kwa mfano juzi Mh. rais alitangaza kumsimamisha kazi Bw.Kabwe kuwa mkurugenzi wa jiji la Dsm lakini Bw. Abeli akatuma post kuwa Bw. Kabwe amefukuzwa kazi.

Bw. Abeli amekuwa anawatukana viongozi wa upinzani kitu ambacho kitamgharimu endapo hatua za kisheria zitachukuliwa ukizingatia sheria ya mitandaoni. Tayari Arusha kuna kijana katiwa nguvuni na kufikishwa mahakamani kwa kumtukana Mh. rais.

Bw. Abel kumbuka kuna watu unawatukana ni wakubwa kama baba yako hebu wape heshima siasa sio matusi .Kidumu chama cha mapinduzi, hapa kazi tu.
 
Huyo atakuwa kizazi cha zamani,kaibukia fab,mwambieni fb imebaki ya ma house girls na ma house girls,wajanja typo jf.
Aje haiku kama Ana guts za kujenga hoja za msingi,
 
Mbona hueleweki unasimamia nini mkuu au ndo umetoka mtoni kunywa maji
 
Kila mtu na bahati yake anataka kutembelea nyota ya makonda hizi siasa za maji taka wanazofanya hawa vijana zitawaghalimu sana maana ishakuwa fasheni wakijua mkubwa hampendi fulani au kafukuza fulani basi wanatafutia kick hapo hawahangahiki kwenda chuo cha uongozi
 
Yaani kusema Kabwe kafukuzwa kazi na rais ni kutukana.
 
Na wewe Ritz kwaakili zako Kwa Rais kamfukuza Kazi Kabwe au kamsimamisha? Usishabikie uongo
 
Na wewe Ritz kwaakili zako Kwa Rais kamfukuza Kazi Kabwe au kamsimamisha? Usishabikie uongo
Hivi kwa akili yako unadhani Rais atamrudisha kazini Kabwe? Haya endelea kusubiri.

Kabwe ana tuhuma nyingi za ufisadi mkuu kuna na namna nyingi za kufukuzwa kazi.

Unategemea Rais Magufuri atamrudisha Kabwe kuwa tena mkurugenzi wa Jiji?
 
Ule mkoa wamekumbatia sana ccm ndo maana maendeleo ni zero...huwa nikiendaga home laela pale najisikia vibaya mno...tuko nyuma sana mkoa wa rukwa kwa sababu ya kuendekeza kuipenda ccm...kibaya wabunge wa mkoa wa Rukwa na katavi huwa wanawanunulia pombe za kienyeji tu (chimpumu..komoni) wanalidhika ...Elimu pia ni tatizo sana huko
 
Huyu si ndo yule aliyekuwa anamuunga mkono Edward Lowassa kwa nguvu zote katika kinyang'anyiro!
Kweli siasa ni kamchezo ka ovyoo sana
 
Nyumbu ni nyumbu tu siku zote huwa hawajielewi, mtoa post haana akiri kwani mtu akisema fulani kufukuzwa kazi kuna matusi hapo?. Nashauri aliyeleta post hii apelekwe Milembe ili akapimwe akiri yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom