PreGE2025 Abdul Nondo: Kwanini tusidhani 'waliosusa' Uchaguzi wanatumika na CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
522
Reaction score
827
Andiko hili limechapishwa Abdul Nondo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuambatanishwa na video

------------------------------
👇

"Sisi ACT Wazalendo tunajua kwamba chaguzi zetu ni za hovyo ,Sheria ni za hovyo ,Polisi wanalazimiahwa kuwa upande wa CCM ,wasimamizi wa uchaguzi wanatumika na CCM ,tunaelewa tunapambana na Dola sio CCM.".

"Ila Suluhu nini ? . Suluhu sio kususa ,suluhu ni kupambana,sababu usipopambana hakuna kitakacho badilika zaidi tutaendelea kuumia hivyo nendeni mkafanye maamuzi na kulinda kura."

"Waulizeni wanaosusa ,walifanya tafiti wapi kwamba kususia uchaguzi (Election boycott) ina manufaa . Kwanini tusidhani wanaosusa uchaguzi wanatumika na CCM ili kuipa nafasi kupita bila kupingwa ,kwanini tusiamini kwamba wamehongwa na CCM ili kuifanya CCM kupita bila kupingwa."

"Huu Mkoa wenu wa Shinyanga ni Mkoa Maskini sana ,ila ndio Mkoa wenye rasilimali za kutosha na ni Mkoa wa nne unaochangia pato la Taifa baada ya Dar es salaam,Mwanza ,Mbeya alafu Shinyanga.Ila mna umaskini , huduma mbovu za jamii ,Barabara mbovu, ukosefu wa ajira." .

"Oktoba nendeni mkapige kura,nendeni mkalinde kura zenu. Inawesekana kwa nguvu na uwezo wetu ".

Hayo yamezungumzwa na mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa ,ndug.Abdul Nondo akiwa Mkoa wa Shinyanga ,Jimbo la Shinyanga Mjini, Jana tarehe 6/07/2025 .
 
Chaguzi zilizopita ambazo ccm walikua wanajipitisha bila kupingwa kwani walikua wana muhonga nani hadi huyo mjinga aanze kuongea huo ujinga wake? Kanuni walizo saini zinamtaka mpira kura kuondoka eneo la kupigia kura mara amalizapo kupiga kura, sasa watu watalinda vipi kura zao wakiwa mbali na kituo cha kupigia kura? Kwa Tanzania njia pekee ya kulinda kura ni kukaa nayo tuu, sasa huyo mpumbavu akipigwa vizuri na akapatiwa dawa atapona vizuri tuu huyo
 
"Waulizeni wanaosusa ,walifanya tafiti wapi kwamba kususia uchaguzi (Election boycott) ina manufaa . Kwanini tusidhani wanaosusa uchaguzi wanatumika na CCM ili kuipa nafasi kupita bila kupingwa ,kwanini tusiamini kwamba wamehongwa na CCM ili kuifanya CCM kupita bila kupingwa."
Dogo ajue ya kuzingatia ili aachane na yasiyomuhusu.

Kusimanga Chama ambacho hakihusiki na uchaguzi wao haiwezi kumsaidia wala kumjenga. NI GUILTY inawatesa na tamaa zao za kutaka vyeo bila kuzingatia maslahi mapana ya Nchi.

Apige kampeni, aache kelele na visingizio.
 
Unakuwa umeahidiwa majimbo mangapi mpaka ufike kiwango cha kujitoa akili
 
Dogo ajue ya kuzingatia ili aachane na yasiyomuhusu.

Kusimanga Chama ambacho hakihusiki na uchaguzi wao haiwezi kumsaidia wala kumjenga. NI GUILTY inawatesa na tamaa zao za kutaka vyeo bila kuzingatia maslahi mapana ya Nchi.

Apige kampeni, aache kelele na visingizio.
 
Hawa wajinga wanataka watu walindaje kura?kanuni tu walizo saini zinakataa mtu muwa kituoni baada ya kupiga kura. Unalindaje hizo kura ukiwa nyumbani???
Waulize: Zanzibar miaka yote ya uchaguzi Maalim Seif alikuwa anashinda. Kwa mfano mwaka 2020 alishinda kabisa na idadi ya kura zilijulikana na kila mtu. Kwa nini ''hawakulinda'' hizo kura na badala yake wakaacha Mwinyi akatangazwa?
 
Andiko hili limechapishwa Abdul Nondo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuambatanishwa na video

------------------------------
👇

View attachment 3397351
"Sisi ACT Wazalendo tunajua kwamba chaguzi zetu ni za hovyo ,Sheria ni za hovyo ,Polisi wanalazimiahwa kuwa upande wa CCM ,wasimamizi wa uchaguzi wanatumika na CCM ,tunaelewa tunapambana na Dola sio CCM.".

"Ila Suluhu nini ? . Suluhu sio kususa ,suluhu ni kupambana,sababu usipopambana hakuna kitakacho badilika zaidi tutaendelea kuumia hivyo nendeni mkafanye maamuzi na kulinda kura."

"Waulizeni wanaosusa ,walifanya tafiti wapi kwamba kususia uchaguzi (Election boycott) ina manufaa . Kwanini tusidhani wanaosusa uchaguzi wanatumika na CCM ili kuipa nafasi kupita bila kupingwa ,kwanini tusiamini kwamba wamehongwa na CCM ili kuifanya CCM kupita bila kupingwa."

"Huu Mkoa wenu wa Shinyanga ni Mkoa Maskini sana ,ila ndio Mkoa wenye rasilimali za kutosha na ni Mkoa wa nne unaochangia pato la Taifa baada ya Dar es salaam,Mwanza ,Mbeya alafu Shinyanga.Ila mna umaskini , huduma mbovu za jamii ,Barabara mbovu, ukosefu wa ajira." .

"Oktoba nendeni mkapige kura,nendeni mkalinde kura zenu. Inawesekana kwa nguvu na uwezo wetu ".

Hayo yamezungumzwa na mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa ,ndug.Abdul Nondo akiwa Mkoa wa Shinyanga ,Jimbo la Shinyanga Mjini, Jana tarehe 6/07/2025 .
"Kulinda kura katika uchaguzi kwa kutegemea Majabali,marungu na Majambia bila Katiba au Sheria au Kanuni na Tume yenye Uhuru wa kutosha ni sawa sawa na kuwa na Mlinzi Kipofu kwenye ghala lako la dhahabu.Hapo Usalama wa dhahabu zako ni kwa kudra za Mungu au huruma za kaka Jambazi."
In Mwabukusi voice!
 
Kwani chaguzi ya 2025 ndio ya Kwanza ACT wanashiriki? Wanasema wanaka tafiti ya manufaa ya kususia,.sawa. Kwani tafiti/ majaribio ya kushiriki na kulinda kura kwenye chaguzi zilizopita ziliacha maswali? Binafsi sioni haja ya pande hizi kukinzana, wote
wanalinda kura, wenzao wameamua kuzilindia makwao ambapo wana control na usalama wake.
 
Sijui kwanini ACT wanawananga sana CHADEMA, wajikite kujitangaza wao kama wao..mbona CHADEMA hawatoi dongo bali wanaongea sera yao kwa watu

Cheki anavyokaza mishipa yote kuongea utumbo
 
ACT Wazalendo ambao wanajiona sio machawa wa ccm, wakati wa uchaguzi Mkuu 2020 Tanzania Bara walipata wabunge wangapi!? Jibu ni hakuna hata Mbunge MMOJA!

Kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, walipata Wenyeviti wangapi!?

Idadi iliyo patikana inalingana na uhalisia wa kukubalika kwa ACT Wazalendo kwa Jamii ya Watanzania!?

Kukubalika kwa ACT Wazalendo Tanzania Bara, kunalingana na idadi 0 ya wabunge kutoka Bara katika Bunje la JMT!?
 
Back
Top Bottom