Abdelhak Nouri staa wa Ajax aliyelazimika kustaafu soka akiwa na miaka 20

Teko Modise

JF-Expert Member
May 20, 2017
1,914
6,033
Mwanzoni mwa mwaka 2017 katika shule ya soka ya Ajax kulikuwa na kipaji maridhawa ambacho mtendaji mkuu wa Ajax ndugu Edwin Van Der Sar alikuwa ana uhakika baada ya miaka miwili mitatu watapata pesa ndefu kutokana na mauzo ya kinda huyo hatari ambaye si mwingine bali ni Abdelhak Nouri.

Abdelhak Nouri alikuwa anacheza kama kiungo mshambuliaji ila wakati mwingine akicheza kama winga. Baada ya kufanya vizuri kwenye akademi ya Ajax msimu wa 2016/2017 akapandishwa timu ya wakubwa.
33CAA8BD-3E63-47A9-B68A-BE03D57AB1CC.jpeg

Msimu ukaisha akiwa amecheza mechi 8 kwenye timu ya wakubwa, tayari benchi la ufundi wakawa wana matumaini makubwa kwa msimu unaofata.

Wakiwa katika maandalizi ya Pre-Season kwa ajili ya msimu wa 2017/18 Ajax walikuwa na mechi ya kirafiki na Werder Bremen, Nouri alikuwepo uwanjani wakati mechi ikiendelea akanguka na kupoteza ufahamu. Akapelekwa ICU akakaa huko kwa wiki muda wote hakuwa na fahamu. Baada ya wiki akaruhusiwa. Akarudishwa nyumbani lakini alikuja kutoka kwenye coma baada ya mwaka mmoja kupita. Mwaka 2018 alirudishwa tena hospitali baada ya kurudi kwenye coma, akaja kuzinduka mwaka 2020 na kupata nafuu na kupewa ruhusa ya kurudi nyumbani.

Baadae Ajax wakautangazia umma kuwa Nouri amepata changamoto kubwa katika mfumo wake fahamu na ubongo na litakuwa ni tatizo la kudumu. Hivyo hatoweza tena kuendelea kucheza soka. Ikawa ni habari mbaya kwa wapenda kandanda, ukizingatia nyota ndio ilikuwa inaanza kung'aa.

Uchunguzi ulifanywa na kubainika kuwa huduma ya kwanza aliyoipata akiwa uwanjani haikuwa nzuri, familia ikafungua kesi dhidi ya Ajax kwenye shirikisho la soka la Uholanzi.

Mwaka 2020 Ajax wakatangaza kuvunja mkataba wa Nouri baada ya kuonekana hatoweza tena kurudi uwanjani. Wakastaafisha jezi iliyokuwa inavaliwa na Nouri ambayo ni jezi namba 34.

Mwaka 2022, Ajax ikailipa fidia familia ya Nouri ya Euro Milioni 7.85 na klabu hiyo itafidia gharama zote za matibabu kwa muda wote Nouri atakapohitaji matibabu.

Pia Ajax katika kumuenzi Nouri, tuzo ya mchezaji bora chipukizi inaitwa Nouri's Trophy.

Wachezaji wengi waliocheza na Nouri huko Ajax ya vijana na ya wakubwa baada ya kuondoka wamekuwa wakivaa jezi namba 34 kwa heshima ya Mshkaji wao Abdelhak Nouri. Wachezaji hao kama Van de beek, Amrabat, Veltman nk

Je, umejiuliza kibongobongo ikitokea kama hili hali itakuaje? Au yule mchezaji wa polisi aliyeumia anapata stahiki kama hizi? Jibu kaa nalo.
D8D5FF46-B369-40D6-B136-A6983756F461.jpeg
 
Mwanzoni mwa mwaka 2017 katika shule ya soka ya Ajax kulikuwa na kipaji maridhawa ambacho mtendaji mkuu wa Ajax ndugu Edwin Van Der Sar alikuwa ana uhakika baada ya miaka miwili mitatu watapata pesa ndefu kutokana na mauzo ya kinda huyo hatari ambaye si mwingine bali ni Abdelhak Nouri.

Abdelhak Nouri alikuwa anacheza kama kiungo mshambuliaji ila wakati mwingine akicheza kama winga. Baada ya kufanya vizuri kwenye akademi ya Ajax msimu wa 2016/2017 akapandishwa timu ya wakubwa.View attachment 2589656

Msimu ukaisha akiwa amecheza mechi 8 kwenye timu ya wakubwa, tayari benchi la ufundi wakawa wana matumaini makubwa kwa msimu unaofata.

Wakiwa katika maandalizi ya Pre-Season kwa ajili ya msimu wa 2017/18 Ajax walikuwa na mechi ya kirafiki na Werder Bremen, Nouri alikuwepo uwanjani wakati mechi ikiendelea akanguka na kupoteza ufahamu. Akapelekwa ICU akakaa huko kwa wiki muda wote hakuwa na fahamu. Baada ya wiki akaruhusiwa. Akarudishwa nyumbani lakini alikuja kutoka kwenye coma baada ya mwaka mmoja kupita. Mwaka 2018 alirudishwa tena hospitali baada ya kurudi kwenye coma, akaja kuzinduka mwaka 2020 na kupata nafuu na kupewa ruhusa ya kurudi nyumbani.

Baadae Ajax wakautangazia umma kuwa Nouri amepata changamoto kubwa katika mfumo wake fahamu na ubongo na litakuwa ni tatizo la kudumu. Hivyo hatoweza tena kuendelea kucheza soka. Ikawa ni habari mbaya kwa wapenda kandanda, ukizingatia nyota ndio ilikuwa inaanza kung'aa.

Uchunguzi ulifanywa na kubainika kuwa huduma ya kwanza aliyoipata akiwa uwanjani haikuwa nzuri, familia ikafungua kesi dhidi ya Ajax kwenye shirikisho la soka la Uholanzi.

Mwaka 2020 Ajax wakatangaza kuvunja mkataba wa Nouri baada ya kuonekana hatoweza tena kurudi uwanjani. Wakastaafisha jezi iliyokuwa inavaliwa na Nouri ambayo ni jezi namba 34.

Mwaka 2022, Ajax ikailipa fidia familia ya Nouri ya Euro Milioni 7.85 na klabu hiyo itafidia gharama zote za matibabu kwa muda wote Nouri atakapohitaji matibabu.

Pia Ajax katika kumuenzi Nouri, tuzo ya mchezaji bora chipukizi inaitwa Nouri's Trophy.

Wachezaji wengi waliocheza na Nouri huko Ajax ya vijana na ya wakubwa baada ya kuondoka wamekuwa wakivaa jezi namba 34 kwa heshima ya Mshkaji wao Abdelhak Nouri. Wachezaji hao kama Van de beek, Amrabat, Veltman nk

Je, umejiuliza kibongobongo ikitokea kama hili hali itakuaje? Au yule mchezaji wa polisi aliyeumia anapata stahiki kama hizi? Jibu kaa nalo.
View attachment 2589655
Wazungu wako fair sana

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom