Abdallah Mtolea alianza zamani kujipendekeza CCM

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,305
33,924
Wakati mwingine huwa nawalaumu sana viogozi wa vyama vya upinzani kuwa na huruma na kila mtu anayekwenda kwenye vyama vyao na kujifanya anapingana na CCM.

Wengi wa wale wanaorudi CCM walikuwa upinzani kwa kuwa njia za kupanda ngazi za kisiasa kupitia CCM zilikuwa zimefungwa. Ni watu wanaofanana na kila aina ya tabia zilizoko CCM. Kuwa kwao upinzani ilikuwa ni bahati mbaya na hiyari yao.

Kuwa upinzani kwa nchi kama Tanzania ni wito na ni kujitoa mhanga. Kuna watu wako upinzani kwa kuwa wanayakimbizia maslahi yao, na siko wakiahidiwa na kuhakikishiwa kwamba maslahi yao yatatimizwa wakienda CCM, huwa hawafikirii mara mbili mbili kabla ya kukimbilia CCM.

Wakati Mbunge wa Kinondoni Said Maulid Mtulia akijiondoa CUF na kujiunga CCM, kulitolewa maelezo ya kusikitisha sana toka kwa Abdul Kambaya aliyekuwa msemaji wa CUF. Kambaya alisema Mtulia alikuwa hataki kugombea kupitia CUF lakini walimbembeleza agombee!!

Picha ya hapo chini kuhusu mabango ya aliyekuwa Mgombea wa CUF Jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea kuchanganywa na mabango ya wagombea wa CCM, imenifikirisha sana!!

1544971474161.png
 
Lowasa kawekeshwa ili 2020 siku chache kabla ya kura ajitoe CDM ghafla,CDM hawajashtuka
 
ilijulikana mapema kuwa Executive waliona kuwa huyu ni mwanaccm lakini kwa rushwa iliyotanda kwenye kura za maoni ndani ya ccm mtolela akaonekana ccm sio chaguo lake,na cuf alienda kwa kuwa no way out.cuf walifanya makosa kumpitisha huyu kibaraka wa wanyanyaji.
 
Siasa za kishabiki hazina tija hata siku moja, hao viongozi wa upinzani walikuwa na huruma, au ni viongozi wabovu wasiojua kufanya utafiti, ama watakuwa wala rushwa au wapendeleaji.

Kijana kuwa mkweli, ulichokiona ni kweli kilitokea na ni kosa kubwa sana.
 
Back
Top Bottom