Abbas Tarimba muogope muumba wako,acha uchu wa madaraka!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abbas Tarimba muogope muumba wako,acha uchu wa madaraka!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mchajikobe, Nov 4, 2010.

 1. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,400
  Likes Received: 681
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu wana JF,kutokana na matokeo ya uchaguzi kuchakachuliwa naona hii imekuwa kero na mkatisho wa tamaa kwa wapenda mabadiliko wote.Hapa namzungumzia diwani wa kata ya hananasif ndugu Tarimba ambaye alishindwa dhahili kwenye uchaguzi huo,kilichowashangaza wananchi wa kata hii ni kile kitendo cha diwani huyu ambaye kila raia wa kata hii alikuwa ameshamchoka na kukinai uongozi wake kurudi tena madarakani,kila mradi wa kata ameshindwa kuuendeleza kama ujenzi wa shule ya kata ambayo imechukua takriban miaka miatatu na bado haina hata dalili yakumalizika, pamoja na kujengwa kwenye uwanja wa michezo ambapo kuna majengo mawili yaliyosimamishwa ambayo yapo ndani ya eneo la shule,badala ya kujenga kwenye hilo eneo lenye hayo majengo,ameamuru shule ijengwe kwenye uwanja wa michezo,kingine amekuwa mtu wa kutoa hela kila mara anapotaka wadhifa,baada ya zoezi la upigaji kura tulishangazwa na kuona bw.Tarimba kahamishia makazi yake pembezoni mwa kituo cha kupigia kura,huku akiwa mtu mwenye wasiwasi mwingi,matokeo ya awali yalipotangazwa yalionyesha kuwa Tarimba ameshindwa dhidi ya mpinzani wake mama Mosha wa CHADEMA kitendo ambacho Tarimba alikataa kusain matokeo,huku akiendelea kuganda kwenye kituo kama ndipo yalipo makazi yake,siku ya pili tunashangazwa kutangaziwa Tarimba kuwa ameshinda kiti cha udiwani,hivyo kumlazimu mama Mosha kukataa kusain matokeo kwa kuhujumiwa.Kilichowashangaza wengi ni kwamba pamoja na kutangazwa mshindi bado Tarimba alikuwa mnyonge kama aliyepigwa na baridi kali,hakukuwa na shamra shamra za ushindi kama tulizoziona waliposhinda uchaguzi wa serikali za mitaa.Kinachosikitisha watu hapa ni kwanini ung'ang'anie kuongoza watu ambao hawataki kuongozwa nawe?,kwanini udhurumu haki za wengine?Inatakiwa ikumbukwe kuwa unaoenda kuwaongoza ni viumbe wenye utashi(binadamu)na si wanyama,hivyo siku wakichoka kuswagwa kama mlivyozoea,inaweza ikatokea hatari kuu,hiyo amani ya Tanzania iko wapi ktk mazingira kama haya?
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  mkuu Kumbe tunakaa maeneo mamoja kabisa?, pole mkazi mwenzangu wa hananasif
   
 3. doup

  doup JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Mama Mosha aende mahakamani kudai haki yake; tunajua atahonga lakini hatapata amani; kwanini watu wang'ang'ania hivyo?
   
 4. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  nikaribishe nami wiki ijayo nahamia hapo. Nimepata makazi apo hananasifu,kama uko chadema itabidi tutafutane tujenge nchi.
   
Loading...