mchajikobe
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 2,652
- 1,238
Ndugu zangu wana JF,kutokana na matokeo ya uchaguzi kuchakachuliwa naona hii imekuwa kero na mkatisho wa tamaa kwa wapenda mabadiliko wote.Hapa namzungumzia diwani wa kata ya hananasif ndugu Tarimba ambaye alishindwa dhahili kwenye uchaguzi huo,kilichowashangaza wananchi wa kata hii ni kile kitendo cha diwani huyu ambaye kila raia wa kata hii alikuwa ameshamchoka na kukinai uongozi wake kurudi tena madarakani,kila mradi wa kata ameshindwa kuuendeleza kama ujenzi wa shule ya kata ambayo imechukua takriban miaka miatatu na bado haina hata dalili yakumalizika, pamoja na kujengwa kwenye uwanja wa michezo ambapo kuna majengo mawili yaliyosimamishwa ambayo yapo ndani ya eneo la shule,badala ya kujenga kwenye hilo eneo lenye hayo majengo,ameamuru shule ijengwe kwenye uwanja wa michezo,kingine amekuwa mtu wa kutoa hela kila mara anapotaka wadhifa,baada ya zoezi la upigaji kura tulishangazwa na kuona bw.Tarimba kahamishia makazi yake pembezoni mwa kituo cha kupigia kura,huku akiwa mtu mwenye wasiwasi mwingi,matokeo ya awali yalipotangazwa yalionyesha kuwa Tarimba ameshindwa dhidi ya mpinzani wake mama Mosha wa CHADEMA kitendo ambacho Tarimba alikataa kusain matokeo,huku akiendelea kuganda kwenye kituo kama ndipo yalipo makazi yake,siku ya pili tunashangazwa kutangaziwa Tarimba kuwa ameshinda kiti cha udiwani,hivyo kumlazimu mama Mosha kukataa kusain matokeo kwa kuhujumiwa.Kilichowashangaza wengi ni kwamba pamoja na kutangazwa mshindi bado Tarimba alikuwa mnyonge kama aliyepigwa na baridi kali,hakukuwa na shamra shamra za ushindi kama tulizoziona waliposhinda uchaguzi wa serikali za mitaa.Kinachosikitisha watu hapa ni kwanini ung'ang'anie kuongoza watu ambao hawataki kuongozwa nawe?,kwanini udhurumu haki za wengine?Inatakiwa ikumbukwe kuwa unaoenda kuwaongoza ni viumbe wenye utashi(binadamu)na si wanyama,hivyo siku wakichoka kuswagwa kama mlivyozoea,inaweza ikatokea hatari kuu,hiyo amani ya Tanzania iko wapi ktk mazingira kama haya?