Aamua Kumuoa Dada Yake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
4945322.jpg

Wednesday, September 15, 2010 12:23 AM
Mwanaume wa nchini Ireland ambaye alimpachika mimba dada yake na kuzaa naye mtoto kabla ya kugundua kuwa ni ndugu yake, anafunga ndoa na dada yake huyo mwishoni mwa mwezi huu. James na Maura, ambao ni kaka na dada ambao wamezaa mtoto mmoja, wanategemea kuvalishana pingu za maisha mwishoni mwa mwezi huu.

Ndugu hao ambao wameamua kubadilisha majina yao halisi ili wasijulikane na jamii, waliangukia kwenye penzi zito bila ya kutambua kuwa wamezaliwa kutokana na baba mmoja.

"Itakuwa ni harusi ndogo, tuna mashahidi wawili tu ambao tunawafahamu vizuri na wanaelewa hali tuliyo nayo", alisema James

"Hatujui kama baba yetu atakuja kwenye harusi au kama mama zetu watahudhuria harusi yetu".

"Mtoto wetu wa kiume anasubiria kwa hamu harusi yetu na anaelewa kinachoendelea, hatujali kuoana mtu na dada yake", aliongeza James.

James na Maura walizaliwa kutokana na baba mmoja na walikuwa wakiishi miji miwili tofauti iliyo mbali kwa kilomita 160.

James na Maura ambao hivi sasa wana umri kati ya miaka 20-28, Walikutana miaka michache iliyopita kwenye ukumbi wa starehe katika mji mwingine wa tatu na kuangukia kwenye penzi zito na walipata mtoto wa kiume miaka miwili baadae.

Waligundua kuwa ni ndugu mwaka jana wakati wa krismasi wakati mama yake James alipomuambia James kuwa baba yake wa kweli siyo mwanaume aliyemlea miaka yote.

Mwezi wa nne mwaka huu walithibitisha kuwa ni mtu na dada yake baada ya vipimo vya DNA kuthibitisha kufanana kwa DNA zao.

James na Maura walielezea jinsi wanavyoisubiria kwa hamu harusi yao pamoja na kwamba wanajua kuwa sheria za nchi haziwaruhusu kufunga ndoa.

Kutokana na kwamba kitambulisho cha James kinaonyesha jina la baba yake kuwa ni Vincent ambalo ni jina la mwanaume aliyemlea, kipingamizi cha kisheria cha kuzuia ndoa yao kinakuwa kimeepukika kwani majina ya baba kwenye vitambulisho vyao yatakuwa tofauti.
 
Kwanza walikutana kwenye ukumbi wa starehe....Hii tu inatosha kupelekea jambo lolote la hatari!
 
Wale wazee wa infidelity muwe mnasema kama mmeacha kopi sehemu maana hii ni hatari mtu na dada yake lol sasa mtoto hapo atawaitaje wazazi wake :confused2:
 
Duh hii noma kweli, yaani mficha maradhi kweli kifo humuumbua, miaka yote mama hajasema leo anaropoka watu washamegana mpk wamezaa..!! Kha tuwe makini jamani na mizungukoya nje.
Kuna familia moja ya askari polisi ilipatwa na mshangao kwenye msiba wa huyo polisi ilipokuja familia nyingine inalia yani mama na watoto watatu jamaa kazaa nje lakini hata ndg zake hawajui ila polisi wenzake wanajua kuwa jamaa ana nyumba nyingine sasa siku ya mazishi ndi ilikuwa tabu tupu.'yapasa tuwe wawazi kwa masuala kama haya.
 
Maji yameshamwagika ni bora waoane tu maana wamezini mpaka wamezaa sioni cha kuwazuia wasioane, ingekuwa hawajaaa kidogo ingweza kuwa siri lakini mtoto ni kitibitisho kuwa wao walizini, wapo wengi wanaotembea na ndugu zao lakini kama hawajazaa huwa inabaki kuwa mioyoni mwao, na kila mmoja anaweza kuoa na kuolewa na wakasahau yaliyopita.
 
namuonea huruma tu huyo mtoto wao, kwasababu ataishi kwa majonzi maisha yake yote, kwasababu atajiona yeye siyo mtu wa kawaida kama wenzie, ataona yeye ni specie ingine kabisa si sawa na za wenzie kwasababu yeye kazaliwa na wazazi ambao ni kaka na dada ambayo ni laana ya ajabu. Mungu amsaidie tu huyo mtoto, na kwa hao wanaojidai kuisubiria kwa hamu ndoa haramu, Mungu na awaadibishe kwa fundisho la kutosha! hadi watakapoishiwa kabisa na kiburi chao cha kishetani!imefika mahali tumwogope Mungu, kama tumeshindwa kuwaogopa wanadamu, kama tumeshindwa kuona aibu mbele za wanadamu, basi tumwonee aibu na kumwogopa Mungu.
 
Back
Top Bottom